Peter Dafi
JF-Expert Member
- Apr 1, 2012
- 389
- 272
Chama changu Chama Cha Mapinduzi.....
Sasa tunayo kila sababu ya kutembea kifua mbele ingawa hatujafikia bado kiwango Cha kutembea kifua mbele...... Tulipo ni sawa na kadiri ya maandiko ya bibles......
Yohana 1:12 waliompokea walipewa uwezo wa kufanyika wana wa Mungu......
Hapa sasa tunaye Rais anayetupa nafasi ya kutembea kifua mbele.....
Lakini kwa kadiri ya maandiko katika Kitabu Cha Warumi, Yohana na Injili ya Luka, na barua za Paulo kwa Wakorinto na Waefeso, ni kwamba ile Yoh1:12 inakupa nafasi ya kuwa mwana lakini walio wana ni wale wanaoongozwa na Roho wa Mungu.....
CCM nafasi yetu ya kutembea kifua mbele itafika pale tutakapoanza kuishi na kutamka lugha moja kwa Maneno na matendo kama alivyo yeye atupaye nguvu hiyo sasa yaani Rais John Pombe Magufuli......
Yapo maamuzi anayofanya na maagizo anayotoa, kwa kiwango kikubwa haitufurahishi na inatufanya wakati mwingi kushangilia ilihali hatukubali maamuzi....
Tusiwe kama wayahudi waliokuwa wanamfuata Yesu kwa ajili ya mikate na alipowapa neno waliokota mawe na kutaka kumpiga......
Wanaccm tunapomshangilja Magufuli basi na tutende yale anayoyasema...... Maana Yesu alisema..... Ana heri yeye asikiaye Maneno yangu....... Ieleweke kuwa, CCM tunaweza jisifu kwa kumzaa na kumlea Magufuli tukajiona tuna heri, kumbe heri itawaendea wao aafuatao ayasemayo... Naam yeye afuataye njia za Magufuli hata kwa ugumu wake, ndiye atembee kifua mbele......
Wafarisayo na Masadukayo wote hawakukubali mafundisho ya Yesu ingawa walitofautiana wao kwa wao kwenye mafundisho ya uzima wa milele yaani maisha yanayoendewa baada ya hapa.....
Tunao wapinzani wa CCM na ambao hawamkubali Magufuli kwa kuona hana jipya..... Wapo UKAWA na ACT WAZALENDO...... Wakati Farisayo UKAWA anapinga kila neno la Magufuli, Sadukayo ACT anaamini katika Tanzania isiyo na ufisadi na kwa jinsi hii anakubaliana na jinsi Tanzania mpya inavyojengwa......
Na biblia inasema,...... Yesu aliwaambia wanafunzi wake, "Ikiwa haki yenu haitawazidi, Mafarisayo na Masadukayo, basi watoza ushuru na makahaba watawatangulia katika ufalme wa Mungu....."
..... Kwa jinsi hii,..... Ikiwa kupinga Ufisadi na rushwa na uhujumu kwa wanaccm hakutawazidi UKAWA na ACT, basi Mafisadi na wala rushwa watawatangulia katika kuwahudumia wananchi.......
Na tukiwa watu wa kumshangilia tu bila kutenda yale anayosema, itakuwa hakuna saburi au tunzo ya haki tutakayoipata kwa Tanzania.......
Je, unataka kutembea kifua mbele??????? Basi fuata na tenda yale kiongozi wetu anasema.........
1. Mwanachama wa CCM daima kuwa wa kwanza kujifunza na kuelewa sera mbalimbali za serikali na Chama....... Shughulika kutimiza wajibu wako kwa mujibu wa katiba ya Chama na ya nchi, fanya kazi yako halali, pata kipato chako na wakati wote jitolee kupiga vita ujinga maladhi na umaskini katika jamii yako...
2. Kiongozi wa CCM, Katibu, mwenyekiti na wajumbe wa vikao vya Chama...... Ondoeni dhana ya kujjfaidisha kwa nafasi zenu, fundisheni, onyeni, elekezeni, na zaidi sana fanyeni kazi ya Chama si kwa kuwagawa watanzania kwa sababu za kiitikadi bali waunganisheni........
3. Wabunge na madiwani...... Jifunzeni sana na muwe na uelewa mkubwa kwa masuala yanayolihusu taifa...... Fikirieni nje ya box kwa minajiri ya kulinda heshima ya taifa...... Msiishi kama kasuku tu kusema msiyoyajua....... Fanyeni tafiti, jiridhisheni na hoja zetu na za upinzani kabla ya kuziunga mkono au kuzikataa....... Jipimeni kiwango Cha uadilifu wenu usiwe na chembe ya Shaka kwa kujua au kuhisi...... Na la msingi....... Tumbueni majipu yaliyopo maeneo yenu kwa vikao au hata kwa kukosea maana Rais wa nchi anasema heri kukosea tutarekebisha kuliko kulea majipu.........
4. Mawaziri na wakuu wa serikali......... Fanyeni kazi mkimwangalia Rais Magufuli....... Msionee watu wala kupendelea wengine....... Lakini msiache Kutumbua majipu kwa sababu ya Hofu........ Jiepusheni na ufisadi, tamaa, wizi na ulevi wa madaraka......... Jichungeni vinywa vyenu, epukeni kufanya kazi kwa mashindano na kuweni watu wapore na wapenda watu wenye kuwahudumia watanzania pasipo ubaguzi wowote maana mumewekwa kutumikia watanzania kama Rais Magufuli anavyotumikia watanzania.....
Ilindeni haki, maana haki huinua taifa.......
MWALIMU KIBASSA