Puma yetu
Senior Member
- Sep 23, 2016
- 111
- 125
Nakumbuka baada ya mkutano mkuu wa Chama kule DODOMA wa kumpata mgombea wa kiti cha urais kupitia Chama chetu 2020, baada ya kumpata mgombea ambaye binafsi nilitokwa machozi nikiamini kua tumepata katapila litakalokata mizizi yote ya majungu na fitna nje na ndani ya Chama. Tulijitoa kwa moyo mmoja tukidhani kua baada ya kampeni tungeshuhudia tabasamu la aina yake kwa kila mtanzania na maisha yake.
Kadri muda ulivyosogea na kufanikiwa kuwagaragaza kwa kipigo kitakatifu upinzani na safari ya kuelekea nchi ya ahadi nilijua ndiyo inaanza, nilikua na amani kuliko kipindi chichote nikiwa ndani ya chama changu.Nilijawa na furaha isiyo kifani, na kwakweli nilijitolea sana kuwahamasisha wenzangu kuumunga mkono Rais wetu.
Likaitishwa bunge, Mh Rais akalihutubia taifa kupitia chombo hicho kwa hotuba ambayo mimi niliamini haina hata Chembe za kisiasa, hotuba iliyowajawaza matumani wanaccm wenzangu na watanzania kwa ujumla.Nilifurahi sana kuona Mh akijiapiza kuwashughulikia bila huduma waliolihujumu taifa letu kwa muda mrefu huku akitanabaisha kua hakutakua na habari za kuunda tume au mchakato wowote kufanya uchunguzi juu ya jambo flani.
Baada tu ya serikali kuanza kazi tuliona teuzi mbali mbali hasa za makada wenzangu kwenye nyadhifa muhimu serikalini na wengi wao walikua ni watu wasomi na wenye nguvu mpya zisizotia shaka kabisa.
Kwakweli kilichokuja kuanza kunikatisha tamaa ni kuwepo kwa kauli mbalimbali za viongozi serikali ambazo zimekua zikitofautiana kabisa tofauti na awamu iliyopita, kila kiongozi amekua akitamka la kwake ilimradi tu mambo yasonge mbele bila kujali kua kila neno linalotamkwa na serikali linakua ni kama ahadi kwa wanachi.
Juzi juzi tu binafsi mwenyekiti Wangu alipowatembealea wahanga wa tetemeko la ardhi kule Kagera niliumia sana nilipomsikia wakati akitoa msimamo wa serikali juu ya tukio hilo, ilifikia mpaka nikajiuliza hivi ni kweli CCM tunawapenda watanzania? Ni kweli serikali ya chama chamgu bado tutahitaji kuja kusimama kufanya kampeni tena na tena na wanaKagera?
Mimi sikuamini mpaka hotuba ya Mh Rais Wangu alipomaliza kuwahutubia wana Kagera nikidhani huenda ulikua ni utani tu,Kwa bahati nzuri mke Wangu ni Mhaya pamoja na wakwe zangu wote, wakaniambia kua hawana hamu kabisa na maneno hayo na hata wanatamani kufunga stesheni za redio wakisikia sauti ya Mh JPM.
Naumizwa sana na kusikia kua kuna chombo cha habari kinapewa onyo kwa sababu ya kuripoti habari za njaa,sijui ni kwanini imekua hivi nje na mategemeo yangu? Kilikua kijijini juzi debe moja la mahindi ni elf 18 na mifugo haina bei najiuliza tukisema kuna tishio la njaa kuna dhambi gani ilihali njaa ni janga tu kama lile la Kagera?Nifanyeje na CCM bado naipenda?
Kwakweli mimi binafsi mpaka sasa naona ni kama niko njia panda hivi, sina kauli kabisa mbele ya marafiki zangu walio nje ya CCM na hata familia yangu.Maana hata kujigamba mimi ni mwanaccm mbele yao imenitia woga. Kwakweli naona ni kama nimesalitiwa hivi mimi pamoja na wananchi wengine.
Niwaombe wanaccm wenzangu tujaribu kutoa hata ushauri bila kuogopa mtu kwa cheo chake, liwalo na liwe ilimradi tu sauti zisikike.Ninachoshukuru ni kwamba nami sio kiongozi ndani ya serikali au ndani ya Chama changu nilishastaafu toka mwaka jana!sasa nitazungumza tu.