MWANAWILE
JF-Expert Member
- Oct 4, 2014
- 277
- 135
Wakuu,
Chama cha Walimu (CWT) katikati ya mwezi Oktoba 2016 kupitia Rais wake Gration Mukoba ilitoa siku 15 kwa serikali iwe imelipa madeni mbalimbali ya walimu wanayodai kama kupandishwa vyeo, likizo na kulipwa malimbikizo ya mishahara vinginevyo watafanya maamuzi magumu.
Siku 15 zilizotolewa na Ndg. Mukoba zimekwishwa na hakuna tamko lolote lililotolewa. Kama amesitisha hayo maamuzi magumu ajitokeze tena hadharani kuwatangazia walimu na umma kwamba ameghairi kama alivyojitokeza awali kutangaza juu ya maamuzi magumu.
Vinginevyo itaaminika kuwa chama hiki hakina meno na uwezo wa kutetea wanachama wake.
Nawasilisha.