Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 15June 2016
KAULI YA MAALIM SEIF NI, "WANACHAMA WASUBIRI MAAMUZI YA VIKAO".
Kumekuwa na taarifa zikienea kwenye mitandao ya kijamii na kwenye
vyombo vya habari kwamba Mkurugenzi wa mambo ya Nje CUF, Ismail Jussa amemnukuu Katibu mkuu wa CUF Maalim Seif akisema kwamba Prof.Lipumba asahau uenyekiti CUF.
Taarifa hii ni uongo na Katibu mkuu hajatoa .Hii ni miongoni mwa propa ganda zinazotengenezwa na watu wasio na malengo merna kwa cha ma,wakijua fika kwamba maamuzi ya chama hayafanywi na mtu bali vikao vya chama.
Hata hivyo maoni na masimamo wa Katibu Mkuu Maalim Seif ambaye yu ko Marekani ni kwamba wanachama wasubiri maamuzi ya vikao vya cha ma vitaamua mambo mbalimbali yanayoendelea na yatakayo tokea na vitatangaza maamuzi yake kwa wote.
Chama kinatoa rai kwa wanahabari wawe makini sana na vyanzo vya taa rifa mbalimbali wanavyotumia kupata taarifa hasa mitandao ya kijamii. Pia ni muhimu wafuate maadili ya uandishi wa habari kwa kuandika habari kutoka kwenye vyanzo cha uhakika visivyo na shaka.
CUF inatoa angalizo kwa wanachama wake wote wawe makini na taarifa wanazopokea na wazithibitishe kwa umakini ili kuwa na uhakika na kuepuka kupotoshwa.
HAKI SAWA KWA WOTE
Salim Bimani Mkurugenzi
Habari na Uenezi-Taifa