KUNANI; Magical Power habari yako, nimekuwa nakufuatilia kwa muda mrefu na mimi leo naomba unifanyie challenge kwa mume wangu amtaje huyo mwanamke mwingine nipate kaondoka nimechoka. Leo hii anatimiza wiki hayupo nyumbani, watu wananiambia wanamuona Sinza huko anaishi kwa mwanamke mwingine amefungiwa ndani huko sijui wanasema ni Jike Shupa kamfungia ama rafiki wa Jike shupa mimi sijui ila naumia.
MAGICAL POWER; Jike Shupa gani? Huyuhuyu wa nipeleke kwa Mganga nikasake wanga au?
KUNANI; Ndio ila sina uhakika mimi, nisaidie tu kumfanyia challenge ataje mwanamke anayempenda walau nipate ushahidi nikawaonyeshe nyumbani kwa sababu kwa wazazi wangu anajifanya mtakatifu, nikiwaeleza kwamba nateseka hata hawanielewi.
MAGICAL POWER; Pole sana, nipe mawasiliano yake na jina lake.
KUNANI; 07......... Anaitwa MUSTAPHA.
MAGICAL POWER; Haya sawa nakurejea.
π΄π΄π΄π΄
MAGICAL POWER; Habari kaka
MUSTAPHA; Safi, kwema?
MAGICAL POWER; Kwema, vipi umelala nini? Mbona sauti ipo chini sana au unaumwa?
MUSTAPHA; Nimelala tu, karibu
MAGICAL POWER; Asante, vipi tunaweza kuongea japo dakika mbili? (Hapo nikasikia kohozi la mwanamke akikohoa kwa uchovu pembeni yake)
MUSTAPHA; Sawa niambie
MAGICAL POWER; Asante kwa nafasi, bwana mimi naitwa Magical Power ni mshauri wa mahusiano na maisha, nimekutafuta kwa sababu kama dakika kadhaa zilizopita kuna mwanamke kanipigia simu ambaye amejitambulisha kama mpenzi wako...
MUSTAPHA; Sikia kaka sikiaaaa, tutaongea baadae nimechoka sana sasa hivi naumwa ile mbayaaaa siwezi hata kushika simu.
MAGICAL POWER; Iyeee!! wewe tena π³ lakini nimekuuliza kama una muda umesema unao, shida nini zaidi?
CHEPUKO; Honey!! pokea simu hiyooo
MUSTAPHA; Achana nae huyu mzinguaji tuuu
CHEPUKO; Pokea simu nakwambiaaa nimesikia kila kitu
MUSTAPHA; Achana nae bwanaaa!! We mbona unapenda kuanzisha ugomvi usio na maana!!! Huyu si ni mwanaume sasa unataka usikie nini!!
CHEPUKO; Ni mwanaume ndio ila nimesikia anasema ametumwa na mpenzi wako, huyo kaka yupo siriasi kabisa wala sio chizi mpaka akufate wewe, pokea simuuuu honey!!
MUSTAPHA; Sipokei sasa fanya unachotaka
CHEPUKO; Pokeaaa
MUSTAPHA; Sipokeiii
CHEPUKO; Pokeaaaaa nakwambia
MUSTAPHA; Baby come down please π π© π« π
CHEPUKO; Toka ndani kwangu tokaa!!! gerautiiiii
MAGICAL POWER; Jamani mgombane taratibu eeeh!!!
CHEPUKO; Nani amekutuma kaka niambie
MAGICAL POWER; Kuna mwanamke yuko Nzega huyo bwana kampa ujauzito sasa amefika Dar anampigia simu hapokei, ndio kanituma hapa nimpigie akampokee Ubungo. Alafu huyo bwana ana mke au wewe ndiye mke wake? Maana kwa maelezo ya huyu mchepuko wa Nzega anasema anajua kama huyo MUSTAPHA ni mume wa mtu lakini anachotaka yeye ni ujauzito kulelewa na amuoe ampangie chumba.
CHEPUKO; Anyiiiiiiii ππππ« anyiiiiπ anyiiiii π leo ndio mwanzo na mwisho kuja hapa nyumbani!!!! Una mke? Nakuuliza una mke?
MUSTAPHA; Sina mke bwana huyo anakudanganya hata simjui.
MAGICAL POWER; Mimi naenda zangu jamani, tulikuwepo πΆββοΈπΆββοΈ
π΄π΄π΄
MAGICAL POWER; Uko wapi sasa hivi?
KUNANI; Najiandaa nikaoge, umeongea nae?
MAGICAL POWER; Ndio, lakini nimekutana na kitu sio kizuri, sijui mapokeo yako yatakuwaje na binafsi nisingependa kukutumia ukiwa mwenyewe.
KUNANI; We nieleze tuuu nina watoto hapa
MAGICAL POWER; Nataka mtu mzima sio watoto
KUNANI; Sawa, ngoja nimuite rafiki yangu aje, ila si nitakuwa natoa siri za familia Magical Power.
MAGICAL POWER; Hilo nalo neno, watu hawaaminiki, nakutumia ila uwe ngangali na itafutika baada ya kumaliza kuisikiliza sitamani ukae nayo.
KUNANI; Magical Power mimi nataka kuondoka hapa nimechoka, nimelipia ili nipate ushahidi, mimi huenda nipo siriasi kuliko watu wote waliokuja kufanya challenge kwako, hii challenge kwangu ni muhimu kupita maelezo, ni muhimu mnooo. Naweza sema ni Mungu ameamua kusikia maombi yanguuuu ninayomuomba kila siku.
KUNANI; Sawa hamna shida, nakutumia.
KUNANI; Sawa baba.
π΄ BAADA YA KUSIKILIZA VOICE WHATSAPP ππ»
KUNANI; Ashukuriwe Mungu wa Majeshi, asante sana Magical Power, huyu ni Mungu ameamua kujibu ombi langu, nimemuomba nimelia sana, naomba usiifute kwa sababu anaweza kuja kukagua simu yangu akikutana nayo atanipiga ataifuta nitakosa ushahidi. Ila wanaume!! sasa kwanini ananizuia kuondoka na ananifanyia hiviii!!!? π ila asante sana, huu ni ushindi kwangu.
MAGICAL POWER; Pole sana, utanipa mrejesho kwa kitakachotokea baada ya hapa, ila naomba uwe ngangali usiumizwe na hiyo voice.
KUNANI; Sawa kaka nashukuru.
MAGICAL POWER; Haya asante. Bye
π