CHADEMA yataka Dar ipimwe upya kuepuka bomoabomoa

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimeiomba serikali kupitia Wizara ya Ardhi kupima upya ramani ya jiji la Dar es salaam ili wananchi waweze kuelewa maeneo gani yanafaa kwa makazi na yapi yasiyofaa, ili kuepuka bomoa bomoa.

Mratibu wa chama hicho Kanda ya Pwani Casmir Masino ametoa rai hiyo mara baada ya kumtembelea Meya wa Manispaa ya Ilala Charls Kuyeko ofisini kwake na kusema kuwa changamoto wa wananchi kubomolewa makazi yao imekuwa kero na inaathiri maendeleo ya wananchi hao.

Aidha Masino amemkabidhi Meya ilani ya chama pamoja na katiba ya chama na kumtaka Meya asimamie ilani hiyo hasa katika sekta ya elimu ili kuboresha mazingira ya kujifunzia ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa madawati na wanajenga madarasa ya kutosha.
 
Tatizo sisi sio wafuatiliaje ata wakipima nchi nzima kama huna tabia yakwenda kuuliza municipal unapouziwa kiwanja au kujenga ish itakua ni vile vile
 
Hiyo ndo inaitwa urasimu (bureaucracy) sasa,kwanini maswala muhimu kama hayo kuyapata mpaka uwaone manispaa?ramani za miji na majiji zinapaswa kuwafikia hata watendaji wa kijiji hasa wenyeviti wa vijiji kwavile wapo karibu zaidi na wananchi.

Ndio wozo wa ccm wa zamani huo
 
Hivi Jiji la Dar halina Master Plan hadi sasa? Mbona baadhi ya miji huku mikoani wanazo!
 
Back
Top Bottom