CHADEMA yambeba Odinga

Kubwajinga

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2008
Posts
2,193
Reaction score
299
Chadema yambeba Odinga

JUMATATU, MACHI 04, 2013 06:21 NA ARODIA PETER, NAIROBI


Chama cha Demokrasia na Maendeleo

*Kilimtumia magari, wasanii kuzunguka nchi nzima

WAKATI wananchi wa Kenya leo wanatarajia kupiga kura kumchagua rais wa nchi hiyo, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeonekana kumbeba mgombea urais kupitia Chama cha ODM ambacho kimo ndani ya Muungano wa CORD, Raila Odinga, kwa kupeleka magari na timu ya wasanii kumsaidia wakati wote wa kampeni zake.

CHADEMA ambao wanadaiwa kuwa rafiki mkubwa wa Odinga, kilituma magari mawili aina ya Fuso kwa ajili ya kumpigia kampeni ambazo zimedumu kwa mwezi mmoja.

Mbali ya kutuma magari hayo, CHADEMA walituma kikundi cha wasanii kikiongozwa na mwimbaji maarufu wa chama hicho, Fulgance Mapunda 'Mwanakotide'.


Habari kamili: CHADEMA yambeba Odinga



MY TAKE

  1. Hivi huu ni mchezo mzuri kwa CHADEMA na Tanzania kwa ujumla kujiingiza katika siasa za mataifa mengine?
  2. Je kuna faida gani na hasara zipi za vitendo kama hivi?
  3. Ni nani anayefaidika na uingiliaji huu, (a) CHADEMA, (b) Odinga au (c) viongozi wa CDM?
  4. Je hii haihatarishi usalama wa mataifa yetu yote kwa kushabikia <50% ya waKenya?
  5. Je vyama vya siasa, kwa mfano, Iran, Pakistan, China, Venezuela n.k. navyo vikiamua kuingilia kifedha na mali kwenye chaguzi zetu, waTanzania tutajisikiaje?
  6. Je wana CHADEMA wanakubaliana na hili?
 
Odinga atashinda uchaguzi ila awezi kuwa Rais. Ni kama Dr Slaa
 
Acheni udaku jaman kila kukicha CHADEMA,ama kweli imewashika....
 
Namwona odinga akiwa rais wa kenya kwa ushirika na martha karua. Sijajua athari za urafiki na cdm ila nakumbuka pia kuwa odinga alishakuja tz kwa mwaliko wa magufuli. Magufuli alishahudhuria pia kampeni za odinga huko kenya
 
I support Uhuru Kenyatta hata kama me ni chadema damu
 
Namwona odinga akiwa rais wa kenya kwa ushirika na martha karua. Sijajua athari za urafiki na cdm ila nakumbuka pia kuwa odinga alishakuja tz kwa mwaliko wa magufuli. Magufuli alishahudhuria pia kampeni za odinga huko kenya

Urafiki wa watu binafsi ni mzuri, lakini wa chama au serikali nafikiri sio mzuri na unaweza kuwa hatari kwa mahusiano ya nchi zetu, ambazo ni jirani na zinazojaribu kuwa karibu zaidi kiuchumi.
 
Hata JF inashabikia Kenya, na ndio maana kuna Kenyan Forum hapa JF. je una lingine?

Nafikiri JF sio mbaya wakishabikia, lakini chama cha siasa au serikali inaposhabikia, hapo linakuwa suala la kitaifa.
 
Kama habari hii ni ya kweli, CHADEMA wamefanya kitu cha kipuuzi na kipumbavu.
 
Mkuu Kubwajinga!! Ha ha ha!!! Mbona nyie mnatoa hela na mbinu za kuiba kura kwa nchi nyingine? Kwa usalama wa maisha yangu ngoja nisizitaje? Tena tuipongeze CDM kwa kushabikia wazi kwa msaada wa magari na msanii!! Nyie mipango ya mafia ya uchakachuaji si mnaenda kufundisha!!! Hivi wakati ule lile Gari la TOT lienda malawi likitumwa na Chama lilienda kufanya nini vile!!!?? Fanya utafiti kwanza mkuu!!
 
Hakuna tatizo katika hilo. Hicho Chadema ni chama cha siasa na haiwakilishi serikali. Iwapo serikali ingejitokeza na kumsaidia au kuonyesha support kwa mgombea fulani hapo kungekuwa na tatizo.
 
Odinga ni mtu tajiri sana hahitaji msaada wa mafuso, magari yake ya kampeni ninayajua vizuzri na aliagiza yote kutoka UK
 
CCM mlipopeleka kikundi chenu cha TOT kumsaidia Bakili Muluzi kule Malawi ilikuwa sawa tu eeh??Kunya anye kuku,akinya bata kaharisha!

Joseph,
Kama walienda kusaidia Muluzi ashinde, hilo nalo halikuwa jambo sahihi. Lakini kama walienda tu kama wasanii, hiyo ni tofauti kidogo. Lakini CDM wanapotuma rasilimali, hapo nafikiri tunavuka mipaka.

Je tutamlaumu vipi Kikwete kwa kupewa pesa na Iran wakati CDM nao wanajifanya kuwa ka-Irani kadogo nchini Kenya?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…