Wenye kufikiri kidogo utawapata. Ukweli ni kuwa cdm inavuna ikichopanda. Kumbuka hiyo ukawa haina hata mwaka. Lakini ni ukweli ulio wazi kwamba cdm ndio chama cha siasa kilichofanya kazi ya kisiasa zaidi kuliko vyama vyote ikiwemo ccm. Toka uchaguzi wa 2010 mpaka leo cdm ndicho kilichoenda kwa wananchi wengi na kufanya mikutano mingi ya wazi hasa kutoa elimu ya uraia kuliko chama chochote huo ndio ukweli ambao ccm, cuf, nccr nk wanaujua bila kujali wanaujubali ukweli huu ila ukweli ni ukweli. Hao cuf na nccr mnaojaribu kuwaprovoke ili ushirikiano huu uingie jinamizi wakicheza huo mziki wenu wa fitina tutawauliza kwa data walifanya mikutano mingapi hasa huku bara ambayo cdm imevuna bila kuvuja jasho? Vuja jasho kwanza ndio udai shibe kama aliyevuja jasho.