chamilo nicolous
JF-Expert Member
- Mar 10, 2016
- 2,081
- 1,437
Naomba kuwashirikisha katika mambo machache yalionikatisha tamaa, ndani ya chadema kwa mwaka 2016. Yapo mengi ya kisema katika kuboresha chama lakini ngoja nianze na haya 5;
1.Mipango na mikakati mibovu, mingi ikiwa ni ya kimatukio inayotokana na viongozi wakubwa wa serikali kwa kupinga sera za vyama vingine pasipo kutengeneza sera. Hii inatokana na mipango ya kukurupuka na kukogoga mioyo ya watu ambayo kimsingi haina tija katika chama. Mfano: UKUTA, kata funua etc.
2.Kukosekana kwa democrasia ndani ya chama. Licha ya chama kutimiza miaka 22 tangu kuanzishwa, bado hakuna demokrasia, nahii inapelekea misuguano na makundi katika chama.Mfano mwenyekiti kutawala pasipo ukomo, licha ya chama kuwa na wanachama wa kutosha bado chaguzi zinafanyika kwa kupendekezwa na mara nyingine ni jina vs kivuli.
3. Kukosekana kwa ukweli. Hoja nyingi za uongo na uzushi ambao mwisho wake unabakiza aibu katika chama na kutengana kwa wanachama. Mfano Hoja ya kupotea saa 8, maalim kugomea uchaguzi etc.
4.Nia ovu ya kutaka kukandamiza vyama vidogo vinavyo chipukia kwa kigezo cha UKAWA, huku ukawa haina kauli moja.Mfano 'ndani ya chadema kila mtu ni kambale' (Bab Duni) na nje ya hapo UKAWA wanajinasibu kuwa ni wamoja na wanania moja.
5.Baadhi ya viongozi wa chama kutafuta umaarufu kwa kukiuka sheria na taratibu za nchi. Mfano Tundu lissu kufukuzwa bungeni, kesi nyingi zisizo na msingi zinamuandama ambazo angeweza kuziepuka kwakuwa hazina faida kwake iwapo atazishinda zote.
Wito: japo tunataka mabadiliko, tunataka mabadiliko ya kiuchumi ambayo yatategemea usimamizi mzuri na sera zuri za uchumi sio kesi na maandamano.
Mwaka 2016 unaenda kuwa historia tu, tubadilike.