Chadema wanahoji ununuaji ndege ndogo bdl ya kubwa!!!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Kila siku naamini kwamba tatizo kubwa la chadema hakuna watu makini, sasa wanahoji kwa nini Serikali inaanza kununua ndege ndogo badala ya kuanza na kubwa? Hivi hii ni akili kweli?
Serikali inataka kufufua shirika la ndege hivyo ina maana tunaanza moja, sasa ni nani uliona alianza kuunda Shirika la ndege kwa kununua Air Bus 380 ukiacha labda nchi za Waarabu zenye utajiri wa mafuta?

Siku zote kwanza huanzia na safari za ndani, halafu unaanza ktk nchi jirani na ukitoka hapo ndiyo unaanza kwenda sasa masafa marefu kama Japani, Peru, Kanada n.k hakuna aliyevuka hii hatua na hili la safari za ndani hatuhitaji ndege kubwa ya kubeba watu 500 siyo economical, huwezi kurusha ndege ya kubeba abiria 300 ktk Dar kwenda Kigoma au Mwanza hii hailipi, hii ni simple physics ya kidato cha pili kwamba ukubwa wa ndege maana yake ukubwa wa injini, ukubwa wa injini maana yake uhitaji mwingi wa mafuta na pia uhitaji wa matengenezo ya gharama zaidi!

Jamani chadema shirika la ndege hukuwa organic yaani ni hatua kwa hatua kama wewe siyo Oil rich country hakuna aliyeruka hii hatua, hivyo ni sawa kabisa kwa Serikali kununua kwanza ndege ndogo ya abiria 70-100 kwa ajili ya kwanza soko la ndani na nchi jirani, halafu hapo pakikamilika ndiyo sasa kama kuna uhitaji wa kupeleka ndege Dar- Paris au Dar- Tokyo ndiyo tutaagiza ndege kubwa zenye uwezo wa kuchukuwa abiria wengi na kuhimili masafa marefu, ni kwa nini mnashindwa kuelewa jambo rahisi kama hili jamani???
 
Back
Top Bottom