CHADEMA walipanga kushindwa Kinondoni pamoja na Siha

sawa.Ila lazma MJUE CCM HAIKUBALIKI
NA NDO MAANA. NEC NA POLISI WANA SAIDIA KUIBA KURA.
kama ccm wanakubalika HAKUNA SABABU za kuiba kura na kufanya udanganyifu.

Haya Mbowe kashakusoma Asante kwa ushauri wako
 
Nilikuwa naona wachagga ni watu wenye akili sana lakini baada ya kuona post yako nimegundua hata wachagga wapuuuzi mpo
 
Siyo tu zitaongzeka bali huenda akapata kura zote. Kama wasimamizi na wasaidizi wao ni makada kindakikindaki wa ccm, wakurugenzi wa halmashauri ni makada ambao ama walikuwa wana uvccm au walishagombea na ubunge, kama RC ni kada halafu ndiye mabosi wa polisiccm, kama mwenyekiti wa tume ni watu aina ya Kailima na kama wale waliopewa ole kwa kutangaza MTU wa upinzani mshindi ndiyo bado wapo, kama wakuu wa mikoa wanaoandika barua kuomba radhi endapo upinzani ueshinda hata kata wataendelea kuwepo basi tegemea huyo mkuu wenu kushinda kwa 100% lakini nisichokuwa na shaka nacho ni kwamba hiyo 100% itakuwa ni kura za watu wasiozidi milioni tano.

 
Strictly speaking Tanzania si nchi ya vyama vingi (hii ni tangu 1992), mfumo hauruhusu. Na sisi raia wa kawaida tujue siasa ni ajira tu kama zilivyo njia nyingine za kuendesha maisha, hivyo ni vema tusiweke matumaini makubwa sana kwao eti wapo kwa ajili ya kutusaidia. Hata wangeshinda wapinzani bado kwa mwananchi wa kawaida hali ingeendelea kuwa ileile.
Watu tunaowahitaji sana ni wajuzi ambao watatuelimisha kuhusu mifumo mizuri zaidi ya kupeleka nchi mbele, wale wanaoelewa vizuri nchi nyingine zinavyofanya mambo yao ambayo tunaweza kuiga. Hapa unapata watu wa elimu za aina zote, si wanasiasa peke yao.
Na huku ndiyo kuitoa nchi kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine, haitategemea awamu gani au chama gani kipo madarakani.
 
Chadema ni chama kinatafuta kura za huruma lakini ni chama very very disorganised na haifai kupewa dola.
Hawana hata organisation chart ndio maana viongozi wao hawajui majukumu yao
 
Si kuhangaika kusoma uliyoyaandika bali nimeona nikuulize swali.
Wasimamizi wa uchaguzi waliwanyima vibali/viapo kwa makusudi ili asubuhi ya tarehe hiyo walau kwa nusu saa vituoni kusiwepo na wakala yeyote wa upinzani.
Na ndivyo ilivyokuwa.
Madhara ya kutokuwepo mawakala na CCM wakawa ni wao peke yao vituoni,ni kuletwa kwa kura za bandia na kuingizwa katika masanduku.
Hapo wapinzani walitakiwa wafanye nini kushinda hiyo mbinu?

Watajipanga.
 
We endelea tu na "MBONA" zako hizohizo, ila alichokisema mtoa mada kina mantiki sana. Na msipobadirika, hizo Mbona zitaendelea kwa kipindi fulani tu cha wakati, kisha zitatoweka kwakuwa na Cdm haitakuwepo. Chama kipya chenye kujitambua kitashika usikani wa upinzani nchini na kinaweza ndicho kitakachokuwa mbadala wa Ccm kwenye dola... Mbona, Mbona na Mbona.
 
Halafu hizi hoja kama kununuliwa, kuibiwa kura, kuhongwa, Polisi nk ni zenye kufariji na kujipa moyo kiuzembe kabisa. Wanaacha kufikiria mbinu sahihi wanajificha kwenye machaka hayo. Nimeuliza humu, Kwanini watu hawakwenda kupiga kura?

Kuna mawili hapa, eidha hawana imani tena na upinzani au wana imani na utendaji wa serikali hata Bunge na vyama kwao si msingi tena.

Wanasiasa wa Kitanzania, haswa wa upinzani, tusijidanganye, watz waliosoma kufikia levo za kujua maswala ya siasa haswa mfumo wa vyama vingi ni wachache sana, ndio maana akina Dr. Slaa walitumia hoja ya ufisadi, inaeleweka kwa wengi, lakini ukisema sijui serikali inabana demokrasia na ukaifanya kuwa ni hoja, kwa Tz bado sana hiyo. Watu wanataka kero zao za huduma za kijamii zitatuliwe, hawana haja na civil rights, hili liko wazi tu. Wachache sana wenye kuzijua na kuzihitaji haki za kiraia.
 
Uchaguzi ukiwa huru na haki ccm ijiandae kutoka ikulu
Wakati wewe unaendelea kuota uchaguzi huru na wa haki, (sijui hata uko nchi gani kama hata US kumefanyika sintofahamu) wapo ambao wanawaza usifanyike kabisa ama kipindi cha urais kiongezwe.

Watumishi wakiongezwa mishahara, ajira na stahiki zingine, zikiwa safi. Mzunguko wa fedha ukirejea nk hayo ya uchaguzi hayatakuwa na mashiko tena, narudia tena watz wana shida na social rights si civil rights?
 
Na wewe huna tofauti na Cdm kifkra, Aliyekuambia mkurugenzi ni wako nani? Aliyekuambia Polisi ni wako ni nani? Hivi ninyi Mnaishi nchi nyingine hamchangamani na watanzania? Fanyeni kazi, watanzania wanataka kuona matokeo si kelele za mbwembwe. Kizazi cha wafia vyama kishapotea nchini, mmebaki wachache sana.

Siasa zote, ziwe za upinzani ama chama tawala, kwa sasa ni lazima zibadili mifumo yake. We endelea tu kuwaamini wakurugenzi na mapolisi utadhani hao sio watu.
 
Endeleeni kuamini hayohayo, ili mbaki hivyohivyo.
 
sikia nikwambie.
CHADEMA SIO KAMA TUNAKATAA KUSHINDWA KWENYE UCHAGUZI.
BALI TUNATAKA TUSHINDWE KWA HAKI.
SASA MNASEMA MNAKUBALIKA KWANINI MNAIBA KURA?
Unaambiwa hiyo kauli ya kuiba kura, kununuliwa kwa watu ni kauli zenu za kujipa matumaini tu na kujifariji, hilo jambo halipo. Endelea hivyohivyo ubaki hivyohivyo.
 
Endeleeni kuamini hayohayo, ili mbaki hivyohivyo.
hamna JIPYA CCM.
CHADEMA HATUKATAI KUSHINDWA UCHAGUZI.
ILA TUNASHINDWA KWA NJIA GANI.
hamuwezi KUIBA KURA ALAFU MSEME WANANCHI WANAWAKUBALI.
 
Unaambiwa hiyo kauli ya kuiba kura, kununuliwa kwa watu ni kauli zenu za kujipa matumaini tu na kujifariji, hilo jambo halipo. Endelea hivyohivyo ubaki hivyohivyo.
hahaa.
ONA AIBU BASI.
UNAKUMBUKA MWAKA 2015 MASANDUKU YALIYOKAMATWA YAKIWA NA KURA ZA NDIO ZA MAGUFULI.
LABDA UMESAHAU.
JUZI KWENYE UCHAGUZI WA KINONDONI UNAKUMBUKA MWANDISHI ALIRIPOTI NINI KUHUSU WIZI WA KURA?
wewe kweli ni msahaulifu.
NARUDIA TENA HAKUNA UCHAGUZI HATA MMOJA AMBAO CCM WALISHINDA KIHALALI BILA KUFANYA UDANGANYIFU.
 
muache kelele zenu humu.
kutuambia mnakubalika HAPO HAPO MNAIBA KURA.
acheni mpambano upigwe kihalali na HAKI alafu muone.
Nikuambie kitu, siku uchaguzi utakapofanyika kama mnavyotaka, pande zote zitii sheria na kanuni, hapo mtajifunza jambo, kwamba watanzania sio vilaza.
 
Kwanza hukusoma post yake halafu unataka yeye ndiye akusome,,,, hivi Cdm kwanini inataka ipeleke mawakala vituoni kwanza? Kwanini wanataka mawakala wawepo vituoni? Kwanini mnamuhofu mccm DED kuliko mCdm mwenye kununulika hata akiwa na levo ya ubunge na udiwani? Na kama Mbunge ananunulika, wakala ni nani kituoni?
 
Nikuambie kitu, siku uchaguzi utakapofanyika kama mnavyotaka, pande zote zitii sheria na kanuni, hapo mtajifunza jambo, kwamba watanzania sio vilaza.
nimeshasema CHADEMA hatukatai kushindwa.
BALI TUNASHINDWA VIPIII?.
hyo ndo hoja ya msingi..
kushindwa UCHAGUZI ni jambo LA kawaida Ila isiwe KWA wizi au mbinu CHAFU ZA KUIBA KURA HATUTAKUBALI.
ndo maana nimeuliza NI uchaguzi gani CCM walishinda kihalali ?
 
MKUU SAWA YOOTE HAYO YALIFANYWA NA CCM, SASA TUFANYE NINI? TUKAE TUU NAKULALAMIKA BILA MAAMUZI YEYOTE?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…