CHADEMA walipanga kushindwa Kinondoni pamoja na Siha

sawa.Ila lazma MJUE CCM HAIKUBALIKI
NA NDO MAANA. NEC NA POLISI WANA SAIDIA KUIBA KURA.
kama ccm wanakubalika HAKUNA SABABU za kuiba kura na kufanya udanganyifu.

Haya Mbowe kashakusoma Asante kwa ushauri wako
 
Nilikuwa naona wachagga ni watu wenye akili sana lakini baada ya kuona post yako nimegundua hata wachagga wapuuuzi mpo
 
Hilo la ‘disconnect’ nililizungumzia humu kama wiki mbili hivi zilizopita.

Lakini makamanda kwa jinsi walivyo vichwa maji wala hawakunielewa.

Majuzi tu hapa nimezunguka sehemu kadhaa za Tanzania na nilichokiona kwa macho yangu na kukisikia kwa masikio yangu ni tofauti kabisa na kilichopo mitandaoni.

Rais Magufuli [na by extension CCM] anakubalika sana uraiani kuliko anavyopewa credit na hawa the ‘vocal online minority’.

Nina imani asilimia za ushindi wake zitaongezeka 2020 kuliko ilivyokuwa 2015.

Watch this space....
Siyo tu zitaongzeka bali huenda akapata kura zote. Kama wasimamizi na wasaidizi wao ni makada kindakikindaki wa ccm, wakurugenzi wa halmashauri ni makada ambao ama walikuwa wana uvccm au walishagombea na ubunge, kama RC ni kada halafu ndiye mabosi wa polisiccm, kama mwenyekiti wa tume ni watu aina ya Kailima na kama wale waliopewa ole kwa kutangaza MTU wa upinzani mshindi ndiyo bado wapo, kama wakuu wa mikoa wanaoandika barua kuomba radhi endapo upinzani ueshinda hata kata wataendelea kuwepo basi tegemea huyo mkuu wenu kushinda kwa 100% lakini nisichokuwa na shaka nacho ni kwamba hiyo 100% itakuwa ni kura za watu wasiozidi milioni tano.
Tumeshindwa.Ndio neno fupi tu kwa sasa ambalo wanaChadema lazima tukiri.Tumeshindwa kote-Siha na Kinondoni kwa sababu hatukustahili kushinda.

Mimi si mjumbe wa Baraza Kuu wala kikao chochote cha Chama hivyo sitapata fursa ya kutoa tathmini yangu vikaoni.Nikiwa mwanachama wa kawaida nina haya 10 ya tafakuri:

1.Tumekosa mbinu mpya (21st Century Strategies): Chama hakina mbinu mpya za kisayansi katika siasa licha ya kuwa na wabobezi wa sayansi ya siasa kama Prof. Baregu.Tufahamu tu nadharia za kina Baregu za miaka ya 1980 ya jinsi Mugabe alivyoingia madarakani zimepitwa sana na sayansi za kisasa za kidigiti katika kampeni.

Kwa sasa fasihi za "The Rise of R. Mugabe" walizozizoea akina Baregu zimepitwa na kuja vitu vipya katika fasihi za sayansi za siasa kama "The Power of Speaking With A Purpose; Say It Like Obama" ambapo kuna mbinu humo za kisasa ambazo Baregu na aina ya strategist wa Chama wa sasa hawana. Kosa la kwanza.

2.Agenda setting au confusion agenda?: Kazi kubwa katika kampeni zote mbili ilikiwa ni kuwahakikishia wananchi kuwa wagombea hawa waliotukimbia hawafai.Hapa ukisoma fasihi za kisasa katika kampeni lazima "agenda setting theory" itumike.

Tulikuwa na agenda gani ya kuwarejesha waliokuwa wapiga kura wa hawa wagombea na sasa wamehamia CCM wabaki nasi.Tulitumia muda mwingi kulalamikia taratibu za uchaguzi badala ya kujihakikishia kwanza kura.Tuliegama katika kutengeneza mkanganyiko (confusion agenda) na kubaki hatuna pa kushika.Kosa la ajabu kabisa.

3.Wagombea au wasindikizaji: Moja ya mbinu ya ushindi iliyotushinda ni hii.Tulipaswa kuteua wagombea wasio na shaka katika majimbo haya.

Hapa Siha naomba ninyamaze tu kwa sasa maana ni aibu.Lakini Kinondoni tuliamua kuchagua picha ituwakilishe katika uchaguzi. Kosa la karne.

4. Tulitaka kushiriki au tuna agenda ya maendeleo?Hoja za kuwafanya wananchi wakusikilize katika chaguzi hizi ni maendeleo.

Hakika ukiacha kulalama lalama juu ya hiki na kile sikuwahi kusikia mgombea wetu yeyote akija na mkakati hasa wa kuwaletea maendeleo yapi wananchi wa majimbo husika tofauti na kazi inayofanywa sasa na CCM na watendaji wa Serikali. Kosa sana hili.

5. Wapiga debe wachovu: Katika stratejia hii tulishindwa kabisa. Wakati wenzetu walileta watu kwa mkakati wa kushadidisha agenda yao ya maendeleo; mawaziri, wabunge wao na wazee sisi eti unamtegemea Lowassa au Sumaye akutafutie kura. Lowassa yule yule asiyeweza kuzidisha hata dakika 7 anapoongea na aliyeitika juzi kumwaga masifa kwa Serikali ya CCM ndio aweze kukutafutia kura?

Hata kimkakati hatukuwa tunaeleweka tunataka nini. Mbowe anayekubalika zaidi Kaskazini na angekuja Siha angeongeza nguvu akahitimisha kampeni Dar es Salaam ili akimaliza tu blah blah jukwaani akawahi kuku na bia.

6. Agenda ya chama ni dhoofu: Hivi leo agenda yetu ni ipi hasa katika kuwahamasisha wananchi watuunge mkono?

Nauliza tena na tena ni ipi?Tulipigania ufisadi uondolewe leo tumekumbatia watuhumiwa tuliowataja kuwa mafisadi; tulitaka uzembe uondolewe Serikalini leo tunageuka na kutetea wazembe wanaochukuliwa hatua Serikalini. Nauliza tena na tena tulitaka kushinda chaguzi hizi kwa agenda ipi pana ya maendeleo?

7.Agenda vs raslimali: moja ya vitu vinatuuma katika hiki chama ni kuendelea kudhoofu uwezo wa kufikiri licha ya Baraza Kuu kuwa na Maprofesa.

Nimezungumzia agenda hapo juu lakini hata kama tungekuwa nayo kuna maamuzi ya chama yanatuumiza na wananchi wa sasa si wajinga.

Mfano tuliwatoa wabunge wetu wote siku ya kupitisha Bajeti mwaka jana na huenda tutafanya hivyo mwaka huu.Huu ni uamuzi wa kichovu.Unakataa bajeti Bungeni halafu unarudi kwenye jimbo kuomba kura eti utaleta maendeleo!Kwa bajeti ipi sasa?

8.Kigeugeu cha kisiasa: Wanachama wengi wanaumizwa na hili.Uchaguzi wa marudio uliopita tulisusia tena kwa hoja nzito eti hakuna uwanja sawa wa demokrasia.

Uchaguzi huu tukarudi kushiriki.Uwanja sawa wa demokrasia ulijengwa lini na wapi tofauti na tulivyolalamika mwanzo?

Ukiwa na wahuni katika uongozi ndio maana wenye akili wanajiondokea halafu tunaishia kupiga propaganda za kununuliwa.

9.Siasa za kutegemea huruma: Baada ya kushindwa katika yote niliyoyataja awali bado tunaegama katika siasa za kutegemea huruma ya wananchi eti watakuwa tu wamechoshwa na CCM.

Niwaambie viongozi, na hasa kwa sababu ya 10, nitakayoijadili hapa punde dhana hii imepitwa na wakati.

Kwa sasa kutegemea huruma, uongo na kutengeneza matukio ili CCM na Serikali yake vichukiwe sio vitu tena vya maana kwa sasa "kila mtu anapambana na hali yake."

Wananchi wa sasa wanatazama uhalisia wa mambo katika maisha yao na sio mbwembwe na siasa za kizamani za kukunjishana ngumi na kupiga hewa.

10.Mtu huyu John Pombe Magufuli (JPM): Kama wanasiasa za maendeleo lazima tukiri kuwa utendaji wa JPM na stratejia za washauri wake hasa vijana Serikalini na katika chama CCM vimetunyima ajenda.

Hili kama utalikataa ulikubali ndio uhalisia. Utawaambia nini watu wa Kinondoni waliokuwa wa kwanza kuonja raha ya mabasi ya mwendokasi waliokuwa wakiyaona ktk movie za Cyborg au No Retreat No Surrender?, utawaambia nini watu wa Kino ambao Serikali juzi imetangaza inawaletea flyover mpya Mwenge na Moroko? una nini kipya cha kuwaambia watu wa Kino ambao fedha za sherehe za Uhuru zimetumika kupanua barabara yao kipande cha Moroko hadi Mwenge n.k?

Una nini cha kuwaambia wananchi wa chini wa Kinondoni wanaosave pesa zao kidogo kwa sasa kwa sababu Serikali inawalipia elimu bure?

Lazima tukiri JPM na Serikali yake ya sasa wametuvuruga na pamoja na mapovu yetu mitandaoni ni siku tu tutakapouona ukweli huu ndipo tutajua alaaa kumbe wale wananchi tuliokuwa tunadhani ni base yetu wameshahamia kuleee na "wanapambana na hali zao."

Katika mazingira kama haya huwezi kuja na siasa za kutiana matumaini bila mikakati za kuitana tu "kamanda" mara sijui kunja Ngumi

Malya Swai
SIHA Kilimamjaro

Mbona Sasa mliamua kupiga risasi na mliogopa kutoa viapo vya mawakala

Mbona Bunge nzima mlihamishia kinondoni?

Mbona mnanunua madiwani?

Mbona mnaogopa mikutano ya siasa?

Mbona kila siku mnaombwa kuombewa?

Mbona mnatumia polisi?

Ahaa mnaogopa sana nyie
 
Strictly speaking Tanzania si nchi ya vyama vingi (hii ni tangu 1992), mfumo hauruhusu. Na sisi raia wa kawaida tujue siasa ni ajira tu kama zilivyo njia nyingine za kuendesha maisha, hivyo ni vema tusiweke matumaini makubwa sana kwao eti wapo kwa ajili ya kutusaidia. Hata wangeshinda wapinzani bado kwa mwananchi wa kawaida hali ingeendelea kuwa ileile.
Watu tunaowahitaji sana ni wajuzi ambao watatuelimisha kuhusu mifumo mizuri zaidi ya kupeleka nchi mbele, wale wanaoelewa vizuri nchi nyingine zinavyofanya mambo yao ambayo tunaweza kuiga. Hapa unapata watu wa elimu za aina zote, si wanasiasa peke yao.
Na huku ndiyo kuitoa nchi kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine, haitategemea awamu gani au chama gani kipo madarakani.
 
Chadema ni chama kinatafuta kura za huruma lakini ni chama very very disorganised na haifai kupewa dola.
Hawana hata organisation chart ndio maana viongozi wao hawajui majukumu yao
 
Tumeshindwa.Ndio neno fupi tu kwa sasa ambalo wanaChadema lazima tukiri.Tumeshindwa kote-Siha na Kinondoni kwa sababu hatukustahili kushinda.

Mimi si mjumbe wa Baraza Kuu wala kikao chochote cha Chama hivyo sitapata fursa ya kutoa tathmini yangu vikaoni.Nikiwa mwanachama wa kawaida nina haya 10 ya tafakuri:

1.Tumekosa mbinu mpya (21st Century Strategies): Chama hakina mbinu mpya za kisayansi katika siasa licha ya kuwa na wabobezi wa sayansi ya siasa kama Prof. Baregu.Tufahamu tu nadharia za kina Baregu za miaka ya 1980 ya jinsi Mugabe alivyoingia madarakani zimepitwa sana na sayansi za kisasa za kidigiti katika kampeni.

Kwa sasa fasihi za "The Rise of R. Mugabe" walizozizoea akina Baregu zimepitwa na kuja vitu vipya katika fasihi za sayansi za siasa kama "The Power of Speaking With A Purpose; Say It Like Obama" ambapo kuna mbinu humo za kisasa ambazo Baregu na aina ya strategist wa Chama wa sasa hawana. Kosa la kwanza.

2.Agenda setting au confusion agenda?: Kazi kubwa katika kampeni zote mbili ilikiwa ni kuwahakikishia wananchi kuwa wagombea hawa waliotukimbia hawafai.Hapa ukisoma fasihi za kisasa katika kampeni lazima "agenda setting theory" itumike.

Tulikuwa na agenda gani ya kuwarejesha waliokuwa wapiga kura wa hawa wagombea na sasa wamehamia CCM wabaki nasi.Tulitumia muda mwingi kulalamikia taratibu za uchaguzi badala ya kujihakikishia kwanza kura.Tuliegama katika kutengeneza mkanganyiko (confusion agenda) na kubaki hatuna pa kushika.Kosa la ajabu kabisa.

3.Wagombea au wasindikizaji: Moja ya mbinu ya ushindi iliyotushinda ni hii.Tulipaswa kuteua wagombea wasio na shaka katika majimbo haya.

Hapa Siha naomba ninyamaze tu kwa sasa maana ni aibu.Lakini Kinondoni tuliamua kuchagua picha ituwakilishe katika uchaguzi. Kosa la karne.

4. Tulitaka kushiriki au tuna agenda ya maendeleo?Hoja za kuwafanya wananchi wakusikilize katika chaguzi hizi ni maendeleo.

Hakika ukiacha kulalama lalama juu ya hiki na kile sikuwahi kusikia mgombea wetu yeyote akija na mkakati hasa wa kuwaletea maendeleo yapi wananchi wa majimbo husika tofauti na kazi inayofanywa sasa na CCM na watendaji wa Serikali. Kosa sana hili.

5. Wapiga debe wachovu: Katika stratejia hii tulishindwa kabisa. Wakati wenzetu walileta watu kwa mkakati wa kushadidisha agenda yao ya maendeleo; mawaziri, wabunge wao na wazee sisi eti unamtegemea Lowassa au Sumaye akutafutie kura. Lowassa yule yule asiyeweza kuzidisha hata dakika 7 anapoongea na aliyeitika juzi kumwaga masifa kwa Serikali ya CCM ndio aweze kukutafutia kura?

Hata kimkakati hatukuwa tunaeleweka tunataka nini. Mbowe anayekubalika zaidi Kaskazini na angekuja Siha angeongeza nguvu akahitimisha kampeni Dar es Salaam ili akimaliza tu blah blah jukwaani akawahi kuku na bia.

6. Agenda ya chama ni dhoofu: Hivi leo agenda yetu ni ipi hasa katika kuwahamasisha wananchi watuunge mkono?

Nauliza tena na tena ni ipi?Tulipigania ufisadi uondolewe leo tumekumbatia watuhumiwa tuliowataja kuwa mafisadi; tulitaka uzembe uondolewe Serikalini leo tunageuka na kutetea wazembe wanaochukuliwa hatua Serikalini. Nauliza tena na tena tulitaka kushinda chaguzi hizi kwa agenda ipi pana ya maendeleo?

7.Agenda vs raslimali: moja ya vitu vinatuuma katika hiki chama ni kuendelea kudhoofu uwezo wa kufikiri licha ya Baraza Kuu kuwa na Maprofesa.

Nimezungumzia agenda hapo juu lakini hata kama tungekuwa nayo kuna maamuzi ya chama yanatuumiza na wananchi wa sasa si wajinga.

Mfano tuliwatoa wabunge wetu wote siku ya kupitisha Bajeti mwaka jana na huenda tutafanya hivyo mwaka huu.Huu ni uamuzi wa kichovu.Unakataa bajeti Bungeni halafu unarudi kwenye jimbo kuomba kura eti utaleta maendeleo!Kwa bajeti ipi sasa?

8.Kigeugeu cha kisiasa: Wanachama wengi wanaumizwa na hili.Uchaguzi wa marudio uliopita tulisusia tena kwa hoja nzito eti hakuna uwanja sawa wa demokrasia.

Uchaguzi huu tukarudi kushiriki.Uwanja sawa wa demokrasia ulijengwa lini na wapi tofauti na tulivyolalamika mwanzo?

Ukiwa na wahuni katika uongozi ndio maana wenye akili wanajiondokea halafu tunaishia kupiga propaganda za kununuliwa.

9.Siasa za kutegemea huruma: Baada ya kushindwa katika yote niliyoyataja awali bado tunaegama katika siasa za kutegemea huruma ya wananchi eti watakuwa tu wamechoshwa na CCM.

Niwaambie viongozi, na hasa kwa sababu ya 10, nitakayoijadili hapa punde dhana hii imepitwa na wakati.

Kwa sasa kutegemea huruma, uongo na kutengeneza matukio ili CCM na Serikali yake vichukiwe sio vitu tena vya maana kwa sasa "kila mtu anapambana na hali yake."

Wananchi wa sasa wanatazama uhalisia wa mambo katika maisha yao na sio mbwembwe na siasa za kizamani za kukunjishana ngumi na kupiga hewa.

10.Mtu huyu John Pombe Magufuli (JPM): Kama wanasiasa za maendeleo lazima tukiri kuwa utendaji wa JPM na stratejia za washauri wake hasa vijana Serikalini na katika chama CCM vimetunyima ajenda.

Hili kama utalikataa ulikubali ndio uhalisia. Utawaambia nini watu wa Kinondoni waliokuwa wa kwanza kuonja raha ya mabasi ya mwendokasi waliokuwa wakiyaona ktk movie za Cyborg au No Retreat No Surrender?, utawaambia nini watu wa Kino ambao Serikali juzi imetangaza inawaletea flyover mpya Mwenge na Moroko? una nini kipya cha kuwaambia watu wa Kino ambao fedha za sherehe za Uhuru zimetumika kupanua barabara yao kipande cha Moroko hadi Mwenge n.k?

Una nini cha kuwaambia wananchi wa chini wa Kinondoni wanaosave pesa zao kidogo kwa sasa kwa sababu Serikali inawalipia elimu bure?

Lazima tukiri JPM na Serikali yake ya sasa wametuvuruga na pamoja na mapovu yetu mitandaoni ni siku tu tutakapouona ukweli huu ndipo tutajua alaaa kumbe wale wananchi tuliokuwa tunadhani ni base yetu wameshahamia kuleee na "wanapambana na hali zao."

Katika mazingira kama haya huwezi kuja na siasa za kutiana matumaini bila mikakati za kuitana tu "kamanda" mara sijui kunja Ngumi

Malya Swai
SIHA Kilimamjaro
Si kuhangaika kusoma uliyoyaandika bali nimeona nikuulize swali.
Wasimamizi wa uchaguzi waliwanyima vibali/viapo kwa makusudi ili asubuhi ya tarehe hiyo walau kwa nusu saa vituoni kusiwepo na wakala yeyote wa upinzani.
Na ndivyo ilivyokuwa.
Madhara ya kutokuwepo mawakala na CCM wakawa ni wao peke yao vituoni,ni kuletwa kwa kura za bandia na kuingizwa katika masanduku.
Hapo wapinzani walitakiwa wafanye nini kushinda hiyo mbinu?

Watajipanga.
 
Mbona Sasa mliamua kupiga risasi na mliogopa kutoa viapo vya mawakala

Mbona Bunge nzima mlihamishia kinondoni?

Mbona mnanunua madiwani?

Mbona mnaogopa mikutano ya siasa?

Mbona kila siku mnaombwa kuombewa?

Mbona mnatumia polisi?

Ahaa mnaogopa sana nyie
We endelea tu na "MBONA" zako hizohizo, ila alichokisema mtoa mada kina mantiki sana. Na msipobadirika, hizo Mbona zitaendelea kwa kipindi fulani tu cha wakati, kisha zitatoweka kwakuwa na Cdm haitakuwepo. Chama kipya chenye kujitambua kitashika usikani wa upinzani nchini na kinaweza ndicho kitakachokuwa mbadala wa Ccm kwenye dola... Mbona, Mbona na Mbona.
 
Ally Kanah upo sahihi kabisa. I hope kuna watu kwenye vikao vya ndani vya CDM wanaowapa viongozi wa juu ukweli kama huu.

Tatizo ni kwamba kumekuwa na disconnect kati ya kinachozungumzwa mitandaoni na kilichomo mitaani. Kilichomo mitaani ndicho kinachowapa CCM kura nyingi kama tulivyoziona kwenye hizi chaguzi.

Wasomi wa mitandaoni wanajifariji bila kuangalia uhalisia ulivyo mitaani. Watu wanabaki kusingizia:
Kununuliwa
Kuhongwa
Kuiba kura
Polisi kuwahujumu CDM

Basi ilmradi utasikia kila visingizio na hawazungumzii mbinu za kujikwamua kama ulivyoainisha hapa.

Kudos kamanda.
Halafu hizi hoja kama kununuliwa, kuibiwa kura, kuhongwa, Polisi nk ni zenye kufariji na kujipa moyo kiuzembe kabisa. Wanaacha kufikiria mbinu sahihi wanajificha kwenye machaka hayo. Nimeuliza humu, Kwanini watu hawakwenda kupiga kura?

Kuna mawili hapa, eidha hawana imani tena na upinzani au wana imani na utendaji wa serikali hata Bunge na vyama kwao si msingi tena.

Wanasiasa wa Kitanzania, haswa wa upinzani, tusijidanganye, watz waliosoma kufikia levo za kujua maswala ya siasa haswa mfumo wa vyama vingi ni wachache sana, ndio maana akina Dr. Slaa walitumia hoja ya ufisadi, inaeleweka kwa wengi, lakini ukisema sijui serikali inabana demokrasia na ukaifanya kuwa ni hoja, kwa Tz bado sana hiyo. Watu wanataka kero zao za huduma za kijamii zitatuliwe, hawana haja na civil rights, hili liko wazi tu. Wachache sana wenye kuzijua na kuzihitaji haki za kiraia.
 
Uchaguzi ukiwa huru na haki ccm ijiandae kutoka ikulu
Wakati wewe unaendelea kuota uchaguzi huru na wa haki, (sijui hata uko nchi gani kama hata US kumefanyika sintofahamu) wapo ambao wanawaza usifanyike kabisa ama kipindi cha urais kiongezwe.

Watumishi wakiongezwa mishahara, ajira na stahiki zingine, zikiwa safi. Mzunguko wa fedha ukirejea nk hayo ya uchaguzi hayatakuwa na mashiko tena, narudia tena watz wana shida na social rights si civil rights?
 
Chadema hawana ubavu huo wa kuja na mkakati wowote na hakuna mkakati wowote utakao fanikiwa kwani mkurugenzi ni wetu watendaji ni wetu police ni wetu na kila kitu kina toka kwenye mamlaka yetu.
Habari ndo hiyo sasa ninyi endeleeni kupiga kelele na maumivu yenu sisi hatujali. Jipen presha bure lakini ccm ni mbele kwa mbele.
Na wewe huna tofauti na Cdm kifkra, Aliyekuambia mkurugenzi ni wako nani? Aliyekuambia Polisi ni wako ni nani? Hivi ninyi Mnaishi nchi nyingine hamchangamani na watanzania? Fanyeni kazi, watanzania wanataka kuona matokeo si kelele za mbwembwe. Kizazi cha wafia vyama kishapotea nchini, mmebaki wachache sana.

Siasa zote, ziwe za upinzani ama chama tawala, kwa sasa ni lazima zibadili mifumo yake. We endelea tu kuwaamini wakurugenzi na mapolisi utadhani hao sio watu.
 
ANAKUBALIKA KWA KUIBA KURA.
ANAKUBALIKA KWA KUWATESA WAPINZANI.
usione RAIA wamekaa kimya ukafikiri wanapenda yanayotokea.
NIAMBIE NI UCHAGUZI GANI CCM WALISHINDA KWA HAKI?
hata huyo magufuli mwaka 2015 kuna mabox ya kura yalikamatwa yakiwa na kura za tiki kwa magufuli.
UMESAHAU?
NIAMBIE NI UCHAGUZI GANI CCM WALISHINDA KWA HAKI?
Endeleeni kuamini hayohayo, ili mbaki hivyohivyo.
 
sikia nikwambie.
CHADEMA SIO KAMA TUNAKATAA KUSHINDWA KWENYE UCHAGUZI.
BALI TUNATAKA TUSHINDWE KWA HAKI.
SASA MNASEMA MNAKUBALIKA KWANINI MNAIBA KURA?
Unaambiwa hiyo kauli ya kuiba kura, kununuliwa kwa watu ni kauli zenu za kujipa matumaini tu na kujifariji, hilo jambo halipo. Endelea hivyohivyo ubaki hivyohivyo.
 
hahaa.
ONA AIBU BASI.
UNAKUMBUKA MWAKA 2015 MASANDUKU YALIYOKAMATWA YAKIWA NA KURA ZA NDIO ZA MAGUFULI.
LABDA UMESAHAU.
JUZI KWENYE UCHAGUZI WA KINONDONI UNAKUMBUKA MWANDISHI ALIRIPOTI NINI KUHUSU WIZI WA KURA?
wewe kweli ni msahaulifu.
NARUDIA TENA HAKUNA UCHAGUZI HATA MMOJA AMBAO CCM WALISHINDA KIHALALI BILA KUFANYA UDANGANYIFU.
 
muache kelele zenu humu.
kutuambia mnakubalika HAPO HAPO MNAIBA KURA.
acheni mpambano upigwe kihalali na HAKI alafu muone.
Nikuambie kitu, siku uchaguzi utakapofanyika kama mnavyotaka, pande zote zitii sheria na kanuni, hapo mtajifunza jambo, kwamba watanzania sio vilaza.
 
Si kuhangaika kusoma uliyoyaandika bali nimeona nikuulize swali.
Wasimamizi wa uchaguzi waliwanyima vibali/viapo kwa makusudi ili asubuhi ya tarehe hiyo walau kwa nusu saa vituoni kusiwepo na wakala yeyote wa upinzani.
Na ndivyo ilivyokuwa.
Madhara ya kutokuwepo mawakala na CCM wakawa ni wao peke yao vituoni,ni kuletwa kwa kura za bandia na kuingizwa katika masanduku.
Hapo wapinzani walitakiwa wafanye nini kushinda hiyo mbinu?

Watajipanga.
Kwanza hukusoma post yake halafu unataka yeye ndiye akusome,,,, hivi Cdm kwanini inataka ipeleke mawakala vituoni kwanza? Kwanini wanataka mawakala wawepo vituoni? Kwanini mnamuhofu mccm DED kuliko mCdm mwenye kununulika hata akiwa na levo ya ubunge na udiwani? Na kama Mbunge ananunulika, wakala ni nani kituoni?
 
Nikuambie kitu, siku uchaguzi utakapofanyika kama mnavyotaka, pande zote zitii sheria na kanuni, hapo mtajifunza jambo, kwamba watanzania sio vilaza.
nimeshasema CHADEMA hatukatai kushindwa.
BALI TUNASHINDWA VIPIII?.
hyo ndo hoja ya msingi..
kushindwa UCHAGUZI ni jambo LA kawaida Ila isiwe KWA wizi au mbinu CHAFU ZA KUIBA KURA HATUTAKUBALI.
ndo maana nimeuliza NI uchaguzi gani CCM walishinda kihalali ?
 
Mbona Sasa mliamua kupiga risasi na mliogopa kutoa viapo vya mawakala

Mbona Bunge nzima mlihamishia kinondoni?

Mbona mnanunua madiwani?

Mbona mnaogopa mikutano ya siasa?

Mbona kila siku mnaombwa kuombewa?

Mbona mnatumia polisi?

Ahaa mnaogopa sana nyie
MKUU SAWA YOOTE HAYO YALIFANYWA NA CCM, SASA TUFANYE NINI? TUKAE TUU NAKULALAMIKA BILA MAAMUZI YEYOTE?
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom