Chadema waishiwa sera

nadhani unashindwa kutofautisha siasa za majukwaani na siasa za kimipango. vilevile tujue kuwa mtoto wa kiongozi naye ni binadamu kama wengine na nimtanzania na mwenye haki kama wengine. jambo kubwa la kujadili ni je? nafasi hizo wanazipata kwa ushindani uliohuru kama wengine? kama kuna walakini katika upatikanaji wa nafasi hizo hiyo ndo hoja ya msingi. najua kuna taratibu za kuwapata viongozi ndani ya vyama vyao. nadhani anayesambaza huo ujumbe anatakiwa kutueleza walivyo "by-pass" taratibu ili watoto wao wapate nafasi hizo na hata wengine wametishwa kujiondoa ili watoto wao wapate.

jambo la msingi sio ..."mbona na wale wanafanya hivyo"? hilo haliwezi kuhalalisha uovu wowote.

swala la kukutumia sms ni swala la kawaida na tabia ya vyama vya siasa kushawishi wasiokuwa wao wajiunge.

swala la sms wala halijaasisiwa na ccm. hata ccm imeiga. nakumbuka hata daruso-udsm tulitumia sms kabla ya ccm.

swala la vua gamba vaa gwanda ni jambo jema tu kwa chama kujitafutia wana chama. kumbuka chama ni taasisi yenye miongozo yake na ndiyo yenye miongozo ya mienendo ya wanachama wake. kwa hiyo hata huyo mwenye gamba akiingia akakuta mfumo mzuri wa maadili na miiko atakuwa mzuri tu. hakuna aliye zaliwa ni gwanda au gamba ila mifumo yetu ndiyo imekuwa ikituumba au kutuumbua. kingunge wa miaka ya sitini na sabini enzi za mfumo wa maadili na miiko wa mwalimu ni tofauti na kingunge wa leo wa mfumo ulio oza ili hali chama ni kilekile. tafakari.
 
Chadema kimekuwa kinavuta watu kwa nguvu kuingia kwenye Chama, bila kujua madhara yake makubwa ya baadae, Mfano Kiongo anasimama anasema VUA GAMBA VAA GWANDA. Fikilia huyu unayemvuta aliko sasa unamponda je akija huku utamwosha na Omo ili atakate ama atakuja kuendeleza ufisadi?

Ndugu yangu kuna wengine wanajiunga na maisha ya ushenzini kwa kuwa hawana njia mbadala, ila pindi wanapopata upenyo tu wanabadilika kiasi kwamba hata wewe unawasahau. Ni kuhakikishie ukweli ni kuwa, Japokuwa CCM inalalamikiwa kuwa ni chama cha mafisadi lakini si wote mafisadi bali wanalazimika kucheza muziki wa anayemlipa mpiga zumali.
 
Naona umekuwa mratibu mipango wa cdm,huwezi kurupuka na kuwapangia wafanye nin kwani wao wanajua mipango yao itakavoenda
 

We wasema, Misri walikusanyia zaidi ya miezi 3 revolution square kumtoa GADAFI, Arusha imedumaa siku nyingi. Kama siyo presha za CHADEMA mji ungejengwa rami. Bila CHADEMA ungeujua ufisadi wa nchi?
 

Na bado, Misri walikusanyika zaidi ya miezi 3 mfululizo kumtoa rais wao. Mji umedumaa, njoo uone presha za CHADEMA zilivyo sababisha mji mzima kujengwa Rami. Nyie endeleeni kutulia mafisadi wawale hadi macho. Bora kudumaa kuliko kuibiwa
 

Akili yako mbaya kama hiyo avatar yako

Ficha upumbavu wako usifiche hekima yako (Source: Invisible)

Labda unazungumzia arusha ya kule kijijini kwenu
 

Wewe usiyejielewa ndo unaona sisi wakazi wa ar tunasumbuliwa, wewe ni msemaji wetu sisi watu wa arusha? Mm leo najivunia kuwepo CDM hapa town kwan leo huwez kumnyanyasa mtu na ashindwe kudai haki yake arusha hatujalala tumeamka wewe nahs unatokea magambani
 
We wasema, Misri walikusanyia zaidi ya miezi 3 revolution square kumtoa GADAFI, Arusha imedumaa siku nyingi. Kama siyo presha za CHADEMA mji ungejengwa rami. Bila CHADEMA ungeujua ufisadi wa nchi?

Achana nae huyo mwenye meno kama ngiri wala hajui anaongea nini
 

Ameishiwa sera huyo......tena akome kutusingizia watu wa arusha
 
Mimi naamini mtanzania wa kawaida na mwenye akili timamu hawezi kuisema vibaya CHADEMA na kuisifu CCM. Hivi bila CHADEMA uozo wa CCM tungeujua lini?, CUF kimekuwa chama kikubwa cha upinzani lakini wameshindwa kuwajuza watanzania juu ya ufisadi na uzembe wa serikali pamoja na kuongozwa na professor wa uchumi
 
"Kama mmekosa ya kufanya si mwende kwa Ridhiwani akawape Ukuu wa Wialya kama Mrisho Gambo"- hapa hatuami kwenye track yetu,kaeni na roho kwatu zenu huko huko mabwepande........
 
Alafu Cdm na GJL wanakulaza macho sana ,angalia usije ukazimia,mwenzako kinana anatokea arusha na tayari kajikataa , watoto wa mjini wanaita kasepa.
 
Nawapongeza wote mliochangia hata mliodiliki kutoa matusi, lakini haijalishi ilimradi ujumbe umeupata. Naendelea kushangaa mtu mwenye akili zake anawazia mambo ya 2015, huku hana mpango wa kujipanga kubwa anaendelea kubomoa. Je hiyo ndoto ya 2015 ndo mtaanza kujenga daraja zima au ukuta?. Kinachosabisha ushindi ni kidogo sana kwa macho, na wala si wingi wa watu kwenye mikutano na wala si kingine ni kura. Je Chadema mnafikiri wote wanaohudhulia ni wenu ama wengi wanakuja kushuhudia umaarufu wa kiongozi aliyopo jukwaani?. Hata Masanja na Joti wakitangaza leo watakuwepo sehemu fulani watu watajaa, sababu kubwa kuwashuhudia. Waweza kusoma sana hadi uzeeni lakini kikubwa usielimike. Tuamke tuache majisifu yasiyo na maana. Kesho nitaandika habari ya kusifu Chadema ili uone nitakavyo pongezwa kumbe unafiki mtupu, ndicho kinachofanyika kwenye kura.


Tache ubishi tujenge taifa letu
 
Join Date : 27th September 2012
Posts : 10
Rep Power : 305
Likes Received1
Likes Given0Umeanza vibaya, daah!!!
 

'...the guilty are afraid'! Au kiswahili maana yake 'hatia yatia woga' au dhamira mbaya husuta!

Najua nisingitafisri ungetoka kapa kwa jinsi ulivyojikoroga hapo juu.

Jambo moja lafurahisha umemtamka vizuri Dr. Na la pili umetambua kuwa wenye uchaguzi ni ccm basi kwa sasa wengine zamu yao itafika tu usiwe na shaka. Nafuu mara mia ungechangia maoni yako kuhusu hili linaloendelea ss hv yaani chaguzi. Hebu toa maoni wapiga kura tunalo lipi la kujitia matumaini.

Utakuwa umelifanyia uzuri jukwaa na wote wana GT! hii nayo maana yake Great Thinkers wa humu- kiswahili chake ... Muulize huyo mdogo mtoto wa jirani atakusaidia
 
vipi mkeo hapati wateja?wewe vipi ulitaka wateja?nenda zanzibar kuna biashara nzuri sana wewe na mkeo mtapata wateja wengi sana...masaburi yanawashawasha?nenda zenji kawashwewashwe..wakunekune

hukupaswa kumshambulia kwa maneno makali hivi mkuu, gt hujibu hoja kwa hoja au hata kiroja pia hujibiwa kwa hoja! Hebu angalia maneno yako haya umemshambulia hata mkewe, huyo anamakosa gani?
Gwakisa Mwandule said:
nenda zanzibar kuna biashara mzuri sana wewe na mkeo
 
Usiwe na mawazo mgando ndani ya CCM kuna maadui wengi kuliko waliopo nje, usifikiri walioshindwa katika hizo chaguzi wamependa na usione ajabu hao ndo waliotunga na kuandika hizo sms. Kama watakuwa wameandika wafuasi wa CDM itakuwa ni fursa pia ya kuufahamisha umma juu ya undugunization ndani ya CCM kwani ilishawahi kutamkwa kuwa CCM ina wenyewe na wenyewe ndo hao waliobakia yaani watoto wa masikini CCM sio chama chao.
 

Yaani umejiunga juzi tu lakini unatoa mapovu ya kufa mtu duuh!!hii ni nowma kweli hizi shule za kata zinatoa vioja kama si vituko vya karne huyu nae katoka wapi Lol!!Kaka kajipange then uje tena,Kwanza rufaa ya Mh Godbless Lema bado ilisomwa kwa mara ya kwanza sasa sifahamu ulisikia wapi kuwa ameshindwa rufaa yake au umeona kwa TBC??Sasa kwa ufupi ni bora ya kutokuwa na hoja kuliko kuwa na hoja za rushwa,kueneza udini,kutumia jeshi la polisi kuuwa raia,kukandamiza demokrasi,kutoroha wanyama i mean kuwauza wakiwa hai,kuteka watu wanaowapigania maisha yenu yawe bora na wewe ukiwa mmoja wapo uliyemaliza shule ya kata hivi majuzi,kuwa na hoja za kilimo kwanza pasipo kuwashirikisha wakulima kila leo utasikia katika Hotel hiyo kuna kikao cha wakulima lakini ukitizama hakuna hata mkulima mmoja ni wezi watupu na wanalipana hela ya walipa kodi,Kuhusu Arusha Mh Godbles Lema ndio alikuwa mbunge wa Arusha mjini kama hufahamu ndio maana nakisema ulitokea wapi hata hufahamu na hili sasa ulitaka Mh Lema akapambane huko Tanga au Bububu wakati yeye ndio mlengwa wa Arusha kaka pole sana.Jaribu kutulia leta hoja ijadiliwe na sio ushuzi kama huu kubuka humu wanaitwa Home of the Thinkers so jaribu kutulia ili usijaze utumbo kwa Profile yako.KUMBUKA WE DONT CARE ABOUT THE NUMBER WE CARE ABOUT THE QUALITY OF THE NUMBER nikiwa na maana ya kusema usijaze mijipost ambayo ni ya kindondo wake up man.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…