Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,673
- 149,860
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeondoa mahakamani kesi dhidi ya polisi kupinga amri ya kupiga marufuku maandamano na mikutano ya hadhara, baada ya kubainika upungufu wa kisheria katika hati ya mashtaka.
Akizungumza na Mwananchi ofisini kwake, Jaji Mohammed Gwae aliyepangwa kusikiliza shauri hilo alitaja upungufu wa kisheria uliobainika kwenye hati ya mashtaka ni kumjumuisha Kamishna wa Opereresheni na Mafunzo wa Polisi, Nsato Mssanzya ambaye kisheria alistahili kufunguliwa shtaka katika masjala kuu.
“Baada ya kushauriana na mawakili wa Chadema kuhusu suala hilo, waliamua kwa hiari yao kuondoa kesi yao kwa ajili ya kuifanyia marekebisho hati yao ya mashtaka,” alisema Jaji Gwae
Wakili wa Chadema, John Mallya aliyekuwa ameongozana na mwenzake Paul Kipeja alisema shauri hilo halikuanza kusikilizwa kutokana na kutokamilika kwa taratibu za kiofisi za kimahakama.