CHADEMA waanzisha mfumo wa kujitathmini.

CHADEMA waanzisha mfumo wa kujitathmini.

Medical Dictionary

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2012
Posts
1,060
Reaction score
309
Kamati kuu ya chadema imeanzisha mfumo wa kutathmini kazi ya kila kiongozi wa kuchaguliwa au kuteuliwa ndani ya chama hicho kama inaendana na maazimio ya chama kuwatumikia wananchi..
Kamati kuu iliazimia kua tathmini hiyo itaanzia katika mchango wa wabunge,madiwani, na wenyeviti wa mitaa...
source:tanzania daima leo
 
Hiyo inaitwa kwa kimombo " balance score card" sijui ndiyo hiyo au, sijui shibuda atapewa rate gani? Sisi wananchi ndiyo tuwa rate au ni viongozi na je wanatumia modality ipi?
 
Good move....but still bado kuna changamoto za kiutendaji ngazi za chini za chama (i.e wilaya mpaka kata). My suggestions wangejaribu kuassign wabunge kikanda ku-monitor kazi za chama kuanzia ngazi za wilaya mpaka kwenye kata, but my take wasi wa-assign kutokana na ukanda walipotokea katika nafasi zao za Ubunge kuondoa mentality za kikanda na kutoa loop-holes kushambuliwa na Magamba.

My experience kama mdau wa chama ni kwamba we need influential political Leaders ambao watakuwa karibu zaidi za viongozi wa wilaya, majimbo na kata hasa kwa mikoa isiyo na Wabunge kutoka CDM. Bado tuna viongozi wengi ngazi za chini za chama ambao lazima wapewe skills za kiutendaji kukabiliana na ushindani na Magamba, kuliko kufika tu wakati wa operesheni za chama.
 
Tutaiga na sie wa mabwepande,haiwezekani muwe wabunifu kutuzidi
 
Hongereni sana CDM,ili ufanikiwe ni lazima kujitathmini na kujua wapi urekebishe na wapi uongeze juhud zaidi!!
Keep it up!
 
Ni jambo jema sana na ndilo hukosekana hata serikalini. Niliwahi kuuliza mfanyakazi mmoja wa serikali kama anajua kitu kinaitwa "Performance Appraisal", alisema hajui. Je mwisho wa mwaka anatathmiwa ili kujua mpango kazi wa idara anayofanya na majukumu yake vinaonesha kufanikiwa? Akasema anafanyiwa "appraisal" ikiwa imefika wakati wa kupandishwa cheo.

Nilijisikia vibaya sana coz japo nimefanya kazi miaka 15 kwa waajiri wawili, nimekuwa na mkataba wa kazi usiozidi miezi 12 na kabla ya kupata mkataba mpya kuna a) je nafasi yake bado inahitajika kwa mwaka mwingine? Kama ndio, b) matarajio ya kazi yake yamefikiwa. Kama ni la, unakwenda nyumbani!!
 
Good move....but still bado kuna changamoto za kiutendaji ngazi za chini za chama (i.e wilaya mpaka kata). My suggestions wangejaribu kuassign wabunge kikanda ku-monitor kazi za chama kuanzia ngazi za wilaya mpaka kwenye kata, but my take wasi wa-assign kutokana na ukanda walipotokea katika nafasi zao za Ubunge kuondoa mentality za kikanda na kutoa loop-holes kushambuliwa na Magamba.

My experience kama mdau wa chama ni kwamba we need influential political Leaders ambao watakuwa karibu zaidi za viongozi wa wilaya, majimbo na kata hasa kwa mikoa isiyo na Wabunge kutoka CDM. Bado tuna viongozi wengi ngazi za chini za chama ambao lazima wapewe skills za kiutendaji kukabiliana na ushindani na Magamba, kuliko kufika tu wakati wa operesheni za chama.

Nimependa mchango wako, kwani ni very constructive idea.
 
Huo ni uwamuzi mzuri, hiyo njia itumike kuwafichua mamluki wanasaidia move ya akina Zoka, Msangi na Rama katika mauaji ya wapinzani.
 
maubunifu yanayotakiwa ni kama haya, sio kugundua mambo yaziada kule mabwepande..
 
Back
Top Bottom