BABU KIDUDE
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 1,587
- 918
Ni upuuzi kujibu hoja ya kipuuzi
Siasa ni dynamic na wakati fulani ufumbuzi wa tatizo moja huzalisha tatizo jingine, usijifungie ndani ya box,
Ahaaa... baba yupi? Najaribu kujiuliza kama unaweza kutengeneza hoja na kuitetea. Je unaweza ukajieleza na kutoa fikra zako bila kutumia maneno yenye ukakasi? Mara nyingi nimeshuhudia watu ambao ni wepesi wa kuongea pale ambapo lugha ya matusi inatumika na wewe unaonekana ni mmoja wao. Mara nyingi watu hawa hutulia tuli pale ambapo mazingira ya mjadala ni tulivu na watu kutoa hoja zao na kupingana kwa hoja.Upuuzi mwingine kama wa baba fulani
Unapiga zumari mwenyewe unacheza mwenyewe na unataka tukusifie? chagua moja hama upige hama ucheze, wekeni uwanja huru madawa hakuna hospital jamani acheni utani ohh, Rushwa bado ipo haswa high ways humu, watu bado wanasingiziwa kesi huku mtaaani matapeli kila kona ya Nchi, na nk any si kila mwenye kichwa anafikiri vingine vya Kuvalia kofia tuu
Siwezi kutoa upuuzi kama huu, kwa hiyo hakuna cha kutetea. Jifunze kitu kidogo ungekuwa na busara usingeendeleza upuuzi huu. Ungetoa hoja inayoboresha upuuzi wako; kwa sasa hoja zako zimebadirika, au ndiyo akili za kushiliwa na remote? CHADEMA/UKAWA hawajahaha na hawatahaha. Wanohaha ni wale wanaotumia dola bila kujua katiba ya nchi na sheria zake. Kachukue posho yako LumumbaAhaaa... baba yupi? Najaribu kujiuliza kama unaweza kutengeneza hoja na kuitetea. Je unaweza ukajieleza na kutoa fikra zako bila kutumia maneno yenye ukakasi? Mara nyingi nimeshuhudia watu ambao ni wepesi wa kuongea pale ambapo lugha ya matusi inatumika na wewe unaonekana ni mmoja wao. Mara nyingi watu hawa hutulia tuli pale ambapo mazingira ya mjadala ni tulivu na watu kutoa hoja zao na kupingana kwa hoja.
Sasa watu wanaongea kama yameisha vile hawaweki hata akiba ya maneno asee duhNaamini JPM ameanza kwa kuchukua hatua za wazi zinazoonekana. Matatizo haya yamekuwepo kwa miaka mingi na itachukuwa muda mrefu kuyamaliza au kuyapunguza.
Nenda shuleCHADEMA na vyama washirika wanaounda UKAWA wamejikuta kwenye wakati mgumu wa kukosa ajenda baada ya Rais John Pombe Magufuli kuanza kutekeleza ahadi ambazo alizitoa kwenye kampeni za uchaguzi wa mwaka 2015. CHADEMA na vyama washirika wamekuwa wakipeta sana kwa kuibua madudu ya CCM kama rushwa na ufisadi, uzembe serikalini, uongozi mbovu, ahadi zisizotekelezeka na mambo mengi ya ovyo yalikuwa yakitendeka serikalini. Rais Magufuli kwa kiasi flani ameweza kuwashughulikia baadhi ya wala rushwa na mafisadi na kuwatumbua watumishi hewa na kusimamia serikali yake namna ambayo Watanzania hatujawahi kushuhudia kwenye awamu ya 2,3 na 4.
Ni kweli kwamba mambo ambayo yalikipa CHADEMA sifa ni kukemea rushwa na ufisadi serikalini, uongozi mbovu, ahadi hewa za CCM na kushindwa kwa serikali ya CCM kuzitumia vyema rasmali za nchi kwa manufaa ya Watanzania. Mambo haya kwa sasa ndiyo anayoyashughulikia rais Magufuli. Usugu wa matatizo haya umepungua na kuyafanya yasiwe "hot news" kisiasa na CHADEMA kushindwa kuyatumia matatizo haya kama ajenda kwenye mijadala yao. Hivyo CHADEMA/UKAWA wamejikuta hawana ajenda ya kuwafanya wasikike magazetini, redioni, TV na vijiweni.
Vipi kuhusu udikteta? CHADEMA/UKAWA walikuwa wakimnadi Mhe Lowassa kama kiongozi ambaye ataipeleka Tanzania mchakamchaka na kuondoa uzembe serikalini na kuwatumikia watanzania, kukuza uchumi na kuondoa umaskini Tanzania. Kwa tafsiri yangu mchakamchaka ni kutovumilia mambo ya ovyo kama uzembe, wafanyakazi hewa, shule bila madawati, kipindupindu, maandamano yasiyokuwa na tija, rushwa na ufisadi, kutotekeleza ahadi za serikali, ukwepaji kodi, uporaji ardhi, serikali kubaki Dar japo makao makuu yake ni Dodoma na mambo mengine mengi. Sasa inakuwaje CHADEMA wanalalamika pale ambapo Rais Magufuli anaipeleka Tanzania mchakamchaka?
RAI YANGU KWA CHADEMA: Inapaswa CHADEMA na vyama washirika wa UKAWA wajitathmini na kujipanga upya. Kama chama cha upinzani misingi yake ni ipi? Ni matatizo yapi yanaikabili Tanzania na wana njia zipi mbadala za kuyatatua matatizo haya? Ili chama kiendelee kubaki hai na kisikike (kisiwe 'dormant') je ni hoja zipi zenye mashiko zitumiwe kuikosoa serikali?
Mwacha huu hakuna watakalaosema CHADEMA la kuwaumiza wana CCM na wanaomuunga mkono Magufuli zaidi ya MATUSI. Magufuli kawamaliza.
mkuu kijembe kiko wapi?Ni vyema kujibu hoja kwa hoja siyo kujibu hoja kwa vijembe.
Too much of anything is harmful. ....kila jambo lina kiasi. ...kodi mpaka kutoa pesa benki? which type of taxesKwa hiyo kwa uelewa wako unaona natetea riziki yangu? Tatizo kubwa la baadhi ya wanachama wa CHADEMA ni kupinga hata kile kisichopingika. Hivi inakuingia akilini pale ambapo mtu anakerwa na hatua anazozichukua JPM kuhakikisha kwamba kodi stahiki inalipwa serikalini? Wewe binafsi unauonaje utendaji wa JPM?
Too much of anything is harmful. ....kila jambo lina kiasi. ...kodi mpaka kutoa pesa benki? which type of taxes
is that? ??? Wanaoafiki waseme ndioooooooo. ....Ccm nzima ndiyoooooo
Mtoa mada nimeona nisikuache hivihivi coz naona una uhelewa hafifu sana ni hivi hayo yote anayofanya JPM ni matunda ya kuwepo upinzani kwahivo basi ili nchi iendelee tunahitaji wapinzani wenye nguvu pengine kuliko CHADEMA
Nina uelewa labda mara mia zaidi yako. Hujaielewa mada na nilichokiandika. Napenda kazi wanayoifanya CHADEMA na upinzani kwa ujumla. Tatizo la CHADEMA wamejichanganya na sasa hivi wanachokifanya ni kujaribu kufurukuta ili wasisahaulike kwenye siasa na chama kikawa kama NCCR ilivyo. Ila kadi wanayoitumia CHADEMA ya kupambana na JPM wakimuita dikteta itamaliza chama kwa sababu baada ya miaka mitano kuisha utendaji kazi wa JPM utawafanya Watanzania kudharau porojo za udikteta na hapo CHADEMA itawabidi kubadilishia gia angani na kuleta jipya. Kuna mambo ya msingi ambayo CHADEMA wangeweza kukomaa nayo. Mambo ya kimfumo na katiba inayompa JPM nguvu nyingi na siyo kukomaa na JPM binafsi.
Kwanini usiwashauri CHAUMA, ACT-wazalendo, UDP and the like, Kila mara CHADEMA/UKAWA. Why? acha wivu!