CHADEMA UK yapongeza uongozi mpya

CHADEMA UK yapongeza uongozi mpya

Joined
Dec 11, 2010
Posts
3,321
Reaction score
6,331
CHADEMA UK TUNATOA PONGEZI KWA MAFANIKIO YA MKUTANO MKUU

Siku kadhaa zilizopita CHADEMA kikiwa ni chama kinachobeba ndoto za ukombozi za waTanzania walio wengi, kilipiga hatua kubwa na kukamilisha jambo la kihistoria. Baada ya kujenga chama kwenye ngazi na mashina, misingi, wilaya na kanda, CHADEMA ilifanya mkutano mkuu wa kuchagua viongozi wakuu wa chama kuanzia kiti cha Mwenyeki na Katibu pamoja na mabaraza ya chama.

Katika uchaguzi huo ambao uliendeshwa kitaalamu na kwa umakini mkubwa viongozi wakuu walipatikana kwa njia ya demokrasia. Hili lilikuwa ni jambo la kishujaa lililowahakikishia wale wenye duku duku kuhusu uimara wa vyama vya upinzani kama CHADEMA ukichukulia maanani namna ambavyo serikali inatumia njia za kiharamu kuviua vyama hivi either kwa kupandikiza puppets au kwa kutumia vyombo vya dola kama Policcm kuvikandamiza. Ukomavu huu wa kisiasa ni ishara kubwa kwamba sasa CHADEMA iko tayari kuishika dola na kuwabadili waTanzania na kuwapa tena heshima yao waliyokuwa wameipoteza kutokana na mlolongo wa viongozi na serikali nyepesi zilizokosa uchungu na uzalendo kupelekea kuuza nchi na kuwaacha waTanzania wakiteseka.

Sisi CHADEMA UK tunapenda kuchukua nafasi hii kuipongeza safu nzima ya ungozi kwa kupata dhamana ya kukiongoza chama. Kipekee na makusudi ya dhati kabisa, tunapenda kumpongeza kamanda Mbowe na Dr Slaa kwa kukubali tena kuipeperusha bendera ya chama wakati huu muhimu tunapoelekea uchaguzi mkuu 2015. Tunapenda kusema kwamba, imani yetu kwa viongozi hawa ni kubwa kwani ni mengi ambayo chama kimepitia chini ya safu hii imara isiyotetereka.

Tunapenda pia kuwapongeza viongozi wote wa mabaraza ya chama (BAVICHA, BAWACHA na Baraza la Wazee la CHADEMA). Mabaraza haya ambayo ni muhimili imara wa chama, ni imani yetu kwamba yamepata viongozi shupavu watakaoleta mabadiliko dhabiti na halisi ili kupambana kumtoa ccm madarakani.

Salamu zetu pia ni kwa viongozi wa ngazi mbali mbali wa chama waliochaguliwa katika hatua mbalimbali zilizokuwa na lengo la kukiimarisha chama kwenye ngazi ya msingi. Tuna Imani kwa kila mmoja yuko tayari kwa mapambano haya.

Mwisho kwa kuyatumia maneno ya Henri Ford aliyesema, "Coming together is a beginning; keeping together is a progress; and working together is a success" tunapenda kuwahakikishia kwamba CHADEMA UK itaendelea kusapoti na kufanya kazi kwa ukaribu na viongozi wote wa ngazi zote za chama kwenye harakati tulizoko sasa hivi. Sisi tunaamini kwamba kwa pamoja tutaweza. Tunaamini katika kufanya kazi kama timu moja tukiwa na lengo na madhumuni mamoja. Kwa kushirkiana kama timu (TEAM: Together Everyone Achieve More) hakuna mbalo CHADEMA itashindwa kutimiza.

Mungu ibariki CHADEMA na nchi yetu ya Tanzania.

Ofisi ya katibu - CHADEMA UK
 
....

......"Coming together is a beginning; keeping together is a progress; and working together is a success"
......

102_6487.jpg
 
Hongera team from UK mmetambua jinsi tunavyopambana tupo pamoja 4rever god bless us amen.
 
Safari bado Mungu hawatie nguvu wote wanaitakia CHADEMA ushindi lakini pia kuna haja kutupia jicho la tatu katika muungano wetu.
 
pongezaneni tu hata kutoka kule Kanada, Ujerumani lakini mkae mkijua , Taifa litalindwa na hilo zozote za kuhatarisha amani mtakazozileta kupitia kwa hao wanaowapongeza
 
pongezaneni tu hata kutoka kule Kanada, Ujerumani lakini mkae mkijua , Taifa litalindwa na hilo zozote za kuhatarisha amani mtakazozileta kupitia kwa hao wanaowapongeza

Kwa hiyo taifa linalindwa na polisiccm kwa kile kinacho endelea Dodoma?!
 
pongezaneni tu hata kutoka kule Kanada, Ujerumani lakini mkae mkijua , Taifa litalindwa na hilo zozote za kuhatarisha amani mtakazozileta kupitia kwa hao wanaowapongeza


Hizo Songs zilishachuja tafuteni mpya,mlizitumie enzi za kibaraka wenu Mrema na baadae kwa Cuf,sasahivi watanzania tumeamka hatudanganyiki,
 
pongezaneni tu hata kutoka kule Kanada, Ujerumani lakini mkae mkijua , Taifa litalindwa na hilo zozote za kuhatarisha amani mtakazozileta kupitia kwa hao wanaowapongeza

Ovyooooooo
 
Back
Top Bottom