Hemed Mzee Hemed
Senior Member
- Jun 26, 2013
- 186
- 41
Jamani angalien tupo wengi tunaonyemele jimbo la rungwe magharibi akiwemo na mh diwani wa kiwira, sio mwambene peke yake.
Natangaza rasmi kuchukua fomu na kugombea ubunge Rungwe Magharibi 2015. Nimechoshwz na usultani ambao umeshindwa kuleta tija. Oscar Mwambene tangulia kaka na mimi nakuja nyuma yako..
Yupo kjana mwengine anajulikana kwa jina Engineer Mwamboneke. naye katangaza nia kugombea kupitia Ukawa (chadema)- Jimbo Rungwe Magharibi.
Jamaa ni Engineer pia ni mtaalamu wa usimamizi wa Miradi. Anatokea Kijiji cha KIKOTA- Naye tumuunge mkono.
Haujamtendea haki Mwaipasi, mtaje kiukamilifu.
Hiyo ligi nimeipenda. Sasa hivi hakuna kupokea Magamba. Mwailenge naye yupo ? Kijana anatisha !!
CCM walizani wao ndo wanaweza kuwa na idadi ya wagombea wengi?
Ila mwakyusa alishasema hagombei mwaka huu ! Atakayegombea Ni dr ulisubisya mpoki kama mambo yakienda sawa !
Frank Magoba na Richard Kasesela je?
Ila mwakyusa alishasema hagombei mwaka huu ! Atakayegombea Ni dr ulisubisya mpoki kama mambo yakienda sawa !
Magoba ni mkazi wa Mbagala Kiburugwa , Rungwe anatafuta nini tena ? aache tamaa bhana .
Mpoki atamuweza Kasesela?
Kumbukumbu ninazoziona hapa katika kura za maoni CCM ilikuwa na Magoba, Kasesela, na Mwakyusa na CHADEMA ilikuwa na mmoja tu YUSUPH Suleiman
Mpoki atamuweza Kasesela?
kasesela ni mwepesi kuliko pamba! hana tofauti na Mwakalebela bila kuteuliwa hawezi chochote , fanya utafiti .
Basi Crazy GK atafaa
Jimbo la Rungwe magharibi ambalo kwa sasa Mbunge wake ni Profesa David Mwakyusa, litakuwa na moto mkali wa kisiasa mwaka huu. Mpaka sasa wanachama 18 wa CHADEMA wameonyesha nia ya kuwania ubunge katika jimbo la Rungwe Magharibi, mkoani Mbeya. Wengi zaidi wanatarajiwa kujitokeza.
Waliojitokeza mpaka sasa ni:
1. Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Mbeya Mjini, John Mwambigija, almaarufu - Mzee wa upako;
2. Diwani wa kata ya Mwakibete, jijini Mbeya - Lucas Mwampiki;
3. Yusufu Asukile - Ambaye pia alikuwa mgombea 2010;
4. Sophia Mwakagenda - Mwanachama Mwandamizi;
5. Tabia Mwakikuti;
6. Bertha Mwakasege;
7. Laurent Mwakalibule;
8. Barnaba Pamboma;
9. Wilfred Mwaipyana;
10. Tibandelage Kalinga;
11. Richard Mugogo;
12. Danford Kifukwe;
13. Ahobokile Mwaitenda;
14. Ayubu Mwakisale;
15. Festo Mwaipaja;
16. Richard Mbalase;
17. Deo Mwailenge, na
18. Mwaipasi
Hao ni wana-CHADEMA wanaotishia ubunge wa Mwakyusa na wana-CCM wengine.
Nani ataibuka kidedea na kupeperusha bendera ya CHAMA hicho? Tusubiri.
SOURCE: RAIA MWEMA - Felix Mwakyembe, 0713-290487 - Toleo la 394, Feb 25, 2015
Ukiwa na namba yake ya simu Mpongeze.