CHADEMA, Polisi wanuka damu za binadamu.

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,808
6,502
MATUKIO ya umwagaji damu ambayo yamekuwa yakitokea kwenye mikutano ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), yamesababisha mwenendo wa siasa katika siku za hivi karibuni kuchukua mwelekeo wa harufu ya damu.

Vyanzo vya habari vilivyowasiliana na gazeti hili, vinasema kuwa hatua ya Chadema, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Jeshi la Polisi kuhusishwa katika mlolongo wa matukio hayo ya umwagaji damu, ni ushahidi tosha kwamba wote wanaguswa moja kwa moja na harufu hiyo ya damu.

Gazeti hili limedokezwa kuwa matukio mengi ya umwagaji damu yanayotokea kwenye mikutano ya Chadema, kuanzia Arusha, Iringa, Morogoro na kwingineko, Polisi wameonekana kuwa katikati ya matukio hayo.

Imeelezwa kuwa Polisi wanatajwa kuhusika katika matukio hayo kwa namna mbili, ikiwemo baadhi ya askari wake wasio waaminifu kudaiwa kuhusika katika matukio hayo ya umwagaji damu, lakini pia kwa kitendo chao cha kushindwa kuwanasa wahusika kabla na baada ya matukio hayo.

Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa waliozungumza na gazeti hili, walisema kuwa namna ya kwanza inatokana na mwenendo wa siasa za ushindani baina ya vyama vikuu viwili vinavyoshindana kuusaka ukuu wa dola, ambavyo ni CCM na Chadema, kwamba umechochea uhusika wa polisi katika matukio hayo.

Gazeti hili limeelezwa kuwa ndani ya jeshi hilo hivi sasa kuna ufa na inadaiwa kwamba baadhi ya askari wake wasio waaminifu wameamua kufanya kazi kwa karibu na vyama hivyo vinavyoshindana, badala ya ile ya kusimamia maslahi ya taifa kutokana na sababu zao, ikiwemo baadhi yao kutopendezwa na mwenendo wa baadhi ya mambo katika sehemu zao za kazi.

Tukio la bomu la Jumamosi iliyopita lililotokea kwenye mkutano wa Chadema jijini Arusha, ambalo Chadema wanalituhumu Jeshi la Polisi kuhusika na kwamba wana ushahidi na hilo, limezidi kulipaka damu jeshi hilo.

Hii inatokana na kile kinachodaiwa kuwa baadhi ya askari wake wasio waaminifu wamejipenyeza na kugeuka kuwa mawakala wa CCM, huku wengine wakidaiwa kuwa upande wa vyama vya upinzani, hususani Chadema na kushiriki harakati hizo chafu za umwagaji damu.

Kauli hii inathibitishwa na maelezo yaliyowahi kutolewa na viongozi wa juu wa Chadema, ambao kwa nyakati tofauti waliwahi kukaririwa wakisema kuwa baadhi ya maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama wanaripoti kwao na wamekuwa wakiwapatia baadhi ya taarifa.

Juzi kauli kama hiyo ilitolewa Bungeni na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Mwigulu Nchemba, ambaye alilieleza Bunge kuwa Chadema imekuwa ikiwatumia watumishi wasio waaminifu ndani ya serikali kuleta vurugu na hujuma ya Taifa.

Hoja kama hiyo inajengwa na wachambuzi, pamoja na wafuatiliaji wa masuala mbalimbali kwa msingi kwamba baada tu ya tukio hilo la bomu la sasa, viongozi waandamizi wa Chadema na wale wa CCM wameonekana kushambuliana, kila upande ukinyooshea kidole upande mwingine, huku polisi wakitajwa katikati yao.

Wakati CCM wakikishutumu Chadema kuhusika katika matukio ya umwagaji damu kwa lengo la kukigombanisha chama hicho na wananchi, Chadema wao wamekuwa wakilituhumu Jeshi la Polisi kuwa linatumiwa na CCM kutekeleza vitendo viovu kwa lengo la kukiangamiza.

Mauaji ya kisiasa ambayo yamekuwa yakitokea kwenye mikusanyiko, mikutano, maandamano au mazingira ya kisiasa yaliyohusisha Chadema, ni mengi kiasi cha kukijengea mazingira yenye sura ya mzozo wa kisiasa.

Taarifa zilizokusanywa na gazeti hili, likiwemo tukio la bomu lililolipuliwa kwenye mkutano wa chama hicho siku ya Jumamosi, zinaonyesha kwamba hadi sasa jumla ya watu waliouawa kwenye mikusanyiko au mikutano yake wamefikia 12.

Vifo hivi ni vile vilivyotokea Arusha, Januari 5, 2011, Igunga (Novemba 2011), Arumeru Mashariki (Aprili 2012), Iramba (Julai 14, 2012), Morogoro (Agosti 27, 2012) na Iringa Septemba 02, 2012.

Katika maandamo yaliyoitishwa na Chadema Januari 5, 2011 Jijini Arusha, ambayo hayakuruhusiwa na polisi, watu watatu walipoteza maisha, baada ya chombo hicho cha dola kudaiwa kutumia nguvu na risasi za moto kutawanya waandamanaji.

Mbali na hilo, uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga pamoja na matukio mengine yaliyojitokeza na yaliyohusisha vurugu baina ya Chadema na CCM, ni lile la mfuasi wa chama hicho cha upinzani, Mbwana Masoud, ambaye alitekwa, kuteswa na kunyongwa katika mazingira ya kutatanisha.

Aidha mara baada ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki, kiongozi wa Kata wa Chadema, Msafiri Mbwambo, alichinjwa na chanzo chake kudaiwa kusababishwa na masuala ya kisiasa.

Mauaji mengine ni yale yaliyotokea katika Kijiji cha Ndago, Wilaya ya Iramba, mkoani Singida, ambako kijana mmoja anayedaiwa kuwa kiongozi wa Kata wa UVCCM alikutwa amepoteza maisha katika kijiji hicho, jirani na eneo ulipofanyika mkutano wa hadhara wa Chadema.

Mengine ni yale yaliyotokea mkoani Morogoro, katika maandamano ya chama hicho ambacho kimekuwa na mvutano na Polisi, wote wakinyoosheana vidole kuhusu mauaji ya kijana Ally Zona.

Tukio jingine ni lile la mkoani Iringa, wakati wa kufungua matawi ya Chadema kwenye kata ya Nyololo, Polisi wanadaiwa kumlipua kwa bomu Mwandishi wa Habari, Daudi Mwangosi.

Matukio hayo yote ya uhalifu dhidi ya binadamu yanayofanywa kwenye mikutano ya Chadema, huku Jeshi la Polisi likidaiwa kuhusika katika baadhi ya matukio, wachambuzi wa mambo wanayatafsiri kuwa ni ushahidi tosha kwamba kuna fikra za kuangamizana.

Kwa upande mwingine, kitendo cha Chadema, ambacho kwa muda mrefu kimekuwa kikinyooshewa kidole na Polisi kwa kuendesha siasa za kibabe zinazogharimu maisha ya Watanzania, nacho kinatajwa kuwa chanzo cha umwagaji damu unaotokea katika baadhi ya mikusanyiko yake.

Duru za habari zimeeleza kuwa hatua ya Chadema kudaiwa kuhusika katika mipango ya utekaji na utesaji wa watu mbalimbali pia imekipaka damu chama hicho.

Hoja hii inajengwa na wafuatiliaji wa mambo katika msingi kwamba, tayari Mkurugenzi wa chama hicho wa Idara ya Ulinzi na Usalama, Wilfred Lwakatare pamoja na kada wa chama hicho, Ludovick Rwezaura, wamefikishwa mahakamani kwa kosa hilo la kupanga njama za kuteka watu.

Ni kwa namna hiyo hiyo, na mwendelezo huo wa matukio ya umwagaji damu, baadhi ya wachambuzi wanaona Chadema ndicho kinachokabiliwa na wakati mgumu zaidi, tofauti na CCM, chama dola ambacho nacho kimekuwa kikinyooshewa vidole.

Madai haya yanapewa nguvu na kile kilichoanza kuonekana sasa baada ya tukio la bomu la siku ya Jumamosi, ambapo kauli za kushutumiana za wanasiasa zimeonekana kuchukua nafasi kubwa kiasi cha kutishia kufunika hoja ya Chadema kutaka uchunguzi wa kina ufanyike kubaini wahusika wa tukio hilo.

Tayari kwa nyakati tofauti, Chadema kupitia kwa viongozi wake wa juu, kimekaririwa kikisema kuwa wana ushahidi unaowahusisha polisi katika mlipuko wa sasa, lakini hawatauwasilisha kwao kwa sababu hawana imani nao.

Hata hivyo wakati malumbano haya yakiendelea, uchunguzi wa kitaaluma wa tukio hilo pamoja na mengine yenye sura ya kisiasa umebaki kuwa tata.

Kwa hisani ya Mtanzania Jumapili.
 
Siasa za Tanzania kwa sasa ni hasara tupu. Inaonekana kama demokrasia imekuja wakati wananchi na hasa viongozi wa kisiasa bado ni POLITICAL IMMATURITY.

Kila siku tunasikia wanasiasa wanapiga kelele na kauli mbiyu ya UZALENDO lakini wala huhitaji kuambiwa tazama kwenye body language yao kujua kama matendo yao yanasukumwa na UBINAFSI.

Wanasiasa wetu kwa sasa hawawezi hata kushilikiana kwa moyo wote katika majanga kama ya misiba badala yake kwa sasa vifo na misiba yenye mwelekeo wa kisiasa imekuwa ni TURUFU MBADALA. Matendo kama haya ni kiashilio cha kutosha kuwa UBINAFSI wa wanasiasa Tanzania umechukua mkondo kwenye kiwango cha chini kabisa cha kibinadamu katika siasa za Tanzania.

Nchi inakoelekea sasa itakuwa ni NO GO ZONE AREA kwa viongozi, wanachama au wapenzi wa chama kingine kama kuna kifo au maafa ya kiongozi, mwanachama au mpenzi wa chama fulani kingine amefariki.

Ni bora kuhubiliwa matendo mema na shetani ambaye anajitambulisha kama ni shetani kuliko kuhubiliwa UZALENDO, UKOMBOZI, MAENDELEO na wanasiasa waliovaa sura za kibinadamu wakati fikra na matendo yao niya kishetani.

Tanzania ilikuwa ni nchi ambayo wananchi wake walikuwa wanatambika kupata mvua ili wapate mavuno mazuri lakini kwa sasa wanasiasa wetu wanatambika vifo vya kisiasa vitokee bila kujalisha chanzo ni nini ili mwisho wa mwaka kwenye bakuri la kura wapate mavuno mazuri ya kisiasa. This is more than POLITICAL BANKRUPTCY.

Wanasiasa wetu ndiyo chanzo cha matatizo ya kitaifa wakati wananchi ndiyo wanawategemea wawe SOLUTION ya matatizo ya kifaifa. It's preposterous.

Kama haya ndiyo maendeleo ndani ya demokrasia basi ni bora turudi huko ambako hakuna maendeleo.

We used to have peace, harmony and tranquility with less democratic freedom. Now is the other way around.
 
kuamua kuitetea ccm ni sawa na kujitwisha furushi la kinyesi lisipo kushinda kwa uzito litakushinda harufu!!!
 
Inawezekana kuna ukweli katika unayosema kuhusu wanasiasa wetu.

Lakini najiuliza, mbona hao wanasiasa wanaoonekana 'wakorofi' wanaandamwa na vyombo vya dola kwa muda kisha wanaachwa baada ya umaarufu wao kupungua?

Kumbuka jinsi ambavyo Augustino Lyatonga Mrema aliandamwa sana na vyombo vya dola, na kushutumiwa uhaini, uroho wa madaraka, ukosefu wa uzalendo n.k. Ni lini vyombo hivyo vya dola viliridhika tena na uzalendo wake, na kumfutia shutuma hizo? Sababu ya badiliko hilo la ghafla ni nini?

Kumbuka jinsi Maalim Seif Shariff Hamad alivyotuhumiwa kuwa chama chake ni cha kigaidi. Kumbuka mambo yanayofanana na ya sasa ambapo raia waishio Pemba na Unguja walikuwa na mapambano na polisi na mara kadhaa kuuawa mikononi mwa polisi, na daima matamko ya watawala ilikuwa kulaumu Chama cha Wananchi (CUF) na viongozi wake. Je, kuna hata kiongozi mmoja wa CUF alihukumiwa kwa makosa hayo? Je ni lini watawala wetu walitutamkia kuwa CUF na viongozi wake hawakuwa na malengo ya ugaidi? Ni lini wamebadilika kama kweli walikuwa magaidi? Je, ni nini msimamo wa watawala kuhusu hao ambao waliwatuhumu kuwa magaidi?

Sasa tumeona Chadema inaandamwa na watawala na vyombo vya dola? Unaona uhusiano wowote na shutuma zilizoelekezwa kwa hao walioandamwa mwanzoni? Uhusiano upi?

Kama ni kweli Chadema wamekuwa wakitumia Polisi kutekeleza matukio hayo, kwa nini Rais, ambaye ana mamlaka ya kuunda Tume Huru ya Kimahakama kuchunguza matukio yote hayo yenye mashaka, anasita kuunda Tume Huru ya Kimahakama kuchunguza matukio hayo. Je, kama Intelijensia yetu ina uhakika kuwa uhalifu huu unaratibiwa na Chadema, kwa nini tusiruhusu tume hiyo ituthibitishie ukweli huo ili tukikatae kwa nguvu zote huku tukiwa na hakika kuwa tumekikataa kwa hatia na matendo yao?

Najiuliza pia, iwapo watawala wetu, na vyombo vyetu vya dola vina ushahidi na uhakika wa uhusika wa Chadema katika matendo hayo ya kihalifu, je hayo matendo hayakiuki masharti ya uhalali wa chama cha siasa kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa ya 1992? Kama inakiuka, kwa nini suala hili lisiwe la kisheria (kuchukua hatua za kukifuta chama kwa mujibu wa sheria), badala yake linakuwa la kisiasa (wanasiasa wa chama tawala kuhubiri UGAIDI wa chadema kwenye majukwaa ya siasa kutaka wananchi wakatae Chadema na kuwachagua wao)? Hivi hatuoni hatari ya kuendelea na siasa za kuhukimiana majukwaani wakati mahakama za kutoa hukumu zipo?

Ng'wamapalala, nina uhakika wewe ni mtu makini, nakuomba utafakari haya ukiwa na akili iliyo wazi kutafuta ukweli.
 
Stupid like Werema!
 
Watakutukana sana pamoja na kwamba hilo bandiko lako lina ukweli mkubwa.kazi ya wakurupukaji na watembea na sumu mifukoni hadi baa ni matusi,kila kitu matusi!!!!!
 
Yani kila mtu haeleweki wanahabari hawaeleweki, watawala hawaeleweki,wapinzani hawaeleweki,wasomio ndiyo kabisaa wanaganga njaa tuu

"To know the enemy is half the victory"
 
[QUOTE)We used to have peace, harmony and tranquility with less democratic freedom. Now is the other way around.[/QUOTE]

We used to be stupid!Now with all the technology and source of information we can see clearly what is going on ,in and outside our country.Unless our leaders change how they lead,these must be the last times to enjoy the taste of little peace we have!
 
Inawezekana kuna ukweli katika unayosema kuhusu wanasiasa wetu.

Lakini najiuliza, mbona hao wanasiasa wanaoonekana 'wakorofi' wanaandamwa na vyombo vya dola kwa muda kisha wanaachwa baada ya umaarufu wao kupungua?

Kumbuka jinsi ambavyo Augustino Lyatonga Mrema aliandamwa sana na vyombo vya dola, na kushutumiwa uhaini, uroho wa madaraka, ukosefu wa uzalendo n.k. Ni lini vyombo hivyo vya dola viliridhika tena na uzalendo wake, na kumfutia shutuma hizo? Sababu ya badiliko hilo la ghafla ni nini?

Kumbuka jinsi Maalim Seif Shariff Hamad alivyotuhumiwa kuwa chama chake ni cha kigaidi. Kumbuka mambo yanayofanana na ya sasa ambapo raia waishio Pemba na Unguja walikuwa na mapambano na polisi na mara kadhaa kuuawa mikononi mwa polisi, na daima matamko ya watawala ilikuwa kulaumu Chama cha Wananchi (CUF) na viongozi wake. Je, kuna hata kiongozi mmoja wa CUF alihukumiwa kwa makosa hayo? Je ni lini watawala wetu walitutamkia kuwa CUF na viongozi wake hawakuwa na malengo ya ugaidi? Ni lini wamebadilika kama kweli walikuwa magaidi? Je, ni nini msimamo wa watawala kuhusu hao ambao waliwatuhumu kuwa magaidi?

Sasa tumeona Chadema inaandamwa na watawala na vyombo vya dola? Unaona uhusiano wowote na shutuma zilizoelekezwa kwa hao walioandamwa mwanzoni? Uhusiano upi?

Kama ni kweli Chadema wamekuwa wakitumia Polisi kutekeleza matukio hayo, kwa nini Rais, ambaye ana mamlaka ya kuunda Tume Huru ya Kimahakama kuchunguza matukio yote hayo yenye mashaka, anasita kuunda Tume Huru ya Kimahakama kuchunguza matukio hayo. Je, kama Intelijensia yetu ina uhakika kuwa uhalifu huu unaratibiwa na Chadema, kwa nini tusiruhusu tume hiyo ituthibitishie ukweli huo ili tukikatae kwa nguvu zote huku tukiwa na hakika kuwa tumekikataa kwa hatia na matendo yao?

Najiuliza pia, iwapo watawala wetu, na vyombo vyetu vya dola vina ushahidi na uhakika wa uhusika wa Chadema katika matendo hayo ya kihalifu, je hayo matendo hayakiuki masharti ya uhalali wa chama cha siasa kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa ya 1992? Kama inakiuka, kwa nini suala hili lisiwe la kisheria (kuchukua hatua za kukifuta chama kwa mujibu wa sheria), badala yake linakuwa la kisiasa (wanasiasa wa chama tawala kuhubiri UGAIDI wa chadema kwenye majukwaa ya siasa kutaka wananchi wakatae Chadema na kuwachagua wao)? Hivi hatuoni hatari ya kuendelea na siasa za kuhukimiana majukwaani wakati mahakama za kutoa hukumu zipo?

Ng'wamapalala, nina uhakika wewe ni mtu makini, nakuomba utafakari haya ukiwa na akili iliyo wazi kutafuta ukweli.
Mwanaukweli ninashukuru kwa angalizo lako.

Kwanza niseme Multiparty democracy in 1992 ilikuja Tanzania wakati viongozi wa CCM na serikali yake walikuwa hawataki na hawakuwa wamejiandaa kwa mabadiliko hayo. Kama kusingekuwa na POLITICAL AND ECONOMIC EXTERNAL PRESSURE ninaamini nchi isingeingia kwenye huu mfumo wa kisiasa.

Kwa viongozi wengi wa kisiasa kipindi hicho ilikuwa ni vita kimaslahi ya kichama na katika hilo ndiyo tunapata leo matunda ya vita hivyo vya kimaslahi ambavyo kwa sasa vimechanganywa na vita vya maslahi binafsi kwa maana kuwa UTAIFA au UZALENDO haupo tena.

Mbinu na misingi ya kisiasa ambayo CCM ilikuwa imejijengea na kuimarika nchini ndiyo hiyo hiyo iliendelea kuitumia katika kukabiliana kisiasa na wanasiasa au chama kingine kilichoonekana kama ni tishio la kisiasa. Vyama vya siasa za kikomusti zilitumia mbinu za propaganda na pale iliposhindikana, zilikuwa zinatumia mpaka mbinu za kimafia kueneza siasa zake kwa kuwashughulikia "wakorofi"wa kisiasa.

Sikukatalii na ninakubaliana na wewe kuwa CCM imetumia sana mbinu "chafu" kisiasa, hizi ni pamoja na political character assassination kwa wanasiasa na vyama ulivyovitaja hapo juu.

Tatizo lililopo kwa sasa nchini ni kwa vyama vingine vya kisiasa ku-copy & Paste mbinu za kikomusti za CCM ambazo kwangu zimepitwa na wakati katika ulimwengu huu wa siasa wa karne ya 21 na kuanza kuzitumia kiasi kwamba kwa sasa inakuwa ni vigumu kujua kama nani ni SHETANI na nani ni MARAIKA katika ulimwengu huu wa siasa safi.

Kutenda kama CCM ni disadvantage kwa opposition parties kwa sababu hawana uzoefu na political strength kwenye siasa za aina ya kikomunisti.
 
Last edited by a moderator:
siku zote watu wagumuupita,kumbuka firauni,yupo wapi leo?polisi na serikali yao dhalimu zitapita yupo wapi MOI ALIYE JIITA PROFFESAR WA SIASA ZA KENYA,leo wakenya wana katiba mpya
 
Kujaribu kujenga hoja zinazoonyesha kwamba nchi inaendeshwa na "wanasiasa" kama vile hakuna wenye dhamana ya dola ni mkakati laghai sana kwa mustakabali wa taifa. Mleta mada kuwa mkweli; nchi hii kuna chama cha siasa kilichokabidhiwa mamlaka ya dola. Kuna Rais, Mawaziri na watendaji wakuu walio katika nafasi na wenye nyenzo za kuendesha majukumu yao kama inavyostahili. Leo hii kukitwisha chama cha upinzani kama CHADEMA mzigo wa kuvurugika kwa amani na kukishirikisha na taasisi nyeti za dola kama Polisi ni kama kusema wenye mamlaka hawapo au hawana madaraka ya kufanya lolote; ni upuuzi au ulaghai wa hali ya juu.

CHADEMA kama chama cha siasa kinaweza kufutwa mara moja ikithibitika hakienendi ipasavyo. Polisi na vyombo vingine vya dola vinaweza kurekebishwa vikitenda ndivyo-sivyo. Huu uchambuzi wa "kijumlajumla" unaokwepa kuweka kidole kwenye ukweli wa mambo ni ubabaishaji mwingine tusioutaka. Tunataka serikali ifanye kazi yake na wana siasa na vyama vyao wafanye kazi yao. Ushahidi wa polisi kutesa na kuua kwa malengo ya kisiasa umeonekana. Serikali haijachukua hatua zinazoondoa utata katika matukio mengi tu mabovu yanayohusisha polisi badala yake tunasikia watuhumiwa wakipandishwa vyeo huku matukio husika yakiwa hayafikia hitimisho. Kusema CHADEMA (chama cha upinzani) inatumia polisi wasio waaminifu kufanya mauaji ni hoja ya kijanja kuficha aibu. Polisi kumkamata Lwakatare kwa ushaidi wa You Tube na kusita kuwagusa wengine kama akina Ilunga na Lipumba ni ubabaishaji mtupu. Huwezi kuendesha shughuli za dola "kiswahili" namna hiyo.

Kwa kifupi, hakuna haja wala sababu ya kurudi nyuma (sijui kwenye mfumo wa chama kimoja?). Upinzani wa kweli is here to stay; in whatever party form or under whichever leadership. Serikali inatakiwa ijue kuwa mfumo wa vyama vingi ndio UMEKOMAA sasa. Ijiweke sawa kuukubali na kuutumikia ipasavyo. Kujaribu kulinda vikundi vya mafisadi na walaghai ndani ya chama tawala ni kujidanganya na kuliletea taifa mtafaruku ambao hautakuwa na mwisho. Watu kama akina Pinda are just remnants of a dying system. Aidha, hata chama kingine kikiingia madarakani hali itakuwa hivyohivyo; kitalazimika ama kutumikia wananchi bila ubabaishaji au kijiandae kukumbana na dhahama inayokitokea CCM hivi sasa. Tena wakati huo mambo yataziki kuwa magumu zaidi. It will always be fire under their feet!
 
Inawezekana kuna ukweli katika unayosema kuhusu wanasiasa wetu.

Lakini najiuliza, mbona hao wanasiasa wanaoonekana 'wakorofi' wanaandamwa na vyombo vya dola kwa muda kisha wanaachwa baada ya umaarufu wao kupungua?

Kumbuka jinsi ambavyo Augustino Lyatonga Mrema aliandamwa sana na vyombo vya dola, na kushutumiwa uhaini, uroho wa madaraka, ukosefu wa uzalendo n.k. Ni lini vyombo hivyo vya dola viliridhika tena na uzalendo wake, na kumfutia shutuma hizo? Sababu ya badiliko hilo la ghafla ni nini?

Kumbuka jinsi Maalim Seif Shariff Hamad alivyotuhumiwa kuwa chama chake ni cha kigaidi. Kumbuka mambo yanayofanana na ya sasa ambapo raia waishio Pemba na Unguja walikuwa na mapambano na polisi na mara kadhaa kuuawa mikononi mwa polisi, na daima matamko ya watawala ilikuwa kulaumu Chama cha Wananchi (CUF) na viongozi wake. Je, kuna hata kiongozi mmoja wa CUF alihukumiwa kwa makosa hayo? Je ni lini watawala wetu walitutamkia kuwa CUF na viongozi wake hawakuwa na malengo ya ugaidi? Ni lini wamebadilika kama kweli walikuwa magaidi? Je, ni nini msimamo wa watawala kuhusu hao ambao waliwatuhumu kuwa magaidi?

Sasa tumeona Chadema inaandamwa na watawala na vyombo vya dola? Unaona uhusiano wowote na shutuma zilizoelekezwa kwa hao walioandamwa mwanzoni? Uhusiano upi?

Kama ni kweli Chadema wamekuwa wakitumia Polisi kutekeleza matukio hayo, kwa nini Rais, ambaye ana mamlaka ya kuunda Tume Huru ya Kimahakama kuchunguza matukio yote hayo yenye mashaka, anasita kuunda Tume Huru ya Kimahakama kuchunguza matukio hayo. Je, kama Intelijensia yetu ina uhakika kuwa uhalifu huu unaratibiwa na Chadema, kwa nini tusiruhusu tume hiyo ituthibitishie ukweli huo ili tukikatae kwa nguvu zote huku tukiwa na hakika kuwa tumekikataa kwa hatia na matendo yao?

Najiuliza pia, iwapo watawala wetu, na vyombo vyetu vya dola vina ushahidi na uhakika wa uhusika wa Chadema katika matendo hayo ya kihalifu, je hayo matendo hayakiuki masharti ya uhalali wa chama cha siasa kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa ya 1992? Kama inakiuka, kwa nini suala hili lisiwe la kisheria (kuchukua hatua za kukifuta chama kwa mujibu wa sheria), badala yake linakuwa la kisiasa (wanasiasa wa chama tawala kuhubiri UGAIDI wa chadema kwenye majukwaa ya siasa kutaka wananchi wakatae Chadema na kuwachagua wao)? Hivi hatuoni hatari ya kuendelea na siasa za kuhukimiana majukwaani wakati mahakama za kutoa hukumu zipo?

Ng'wamapalala, nina uhakika wewe ni mtu makini, nakuomba utafakari haya ukiwa na akili iliyo wazi kutafuta ukweli.
Mwanaukweli, umeongea mambo ya msingi.
Yote yanayotokea hapa nchini yamejaa siasa chafu na dharau kwa wananchi.

Najiuliza, ni kweli vyombo vyetu vyote vya usalama haviwezi kuzuia matukio haya yasitokee?
Jibu ni moja tu na la uhakika, ni muendelezo wa yale mengi tuliyoyasikia na kuyaona, kukaa kimya kama walivyokaa kimya pale KIA,wanyama wakapanda ndege.

Naamini kuwa, yeyote aliye makini hawezi kusimama na kusingizia kuwa matukio haya yanafanywa na watu wa nje ya Serikali. Kwa kufanya hivyo atakuwa anaivua nguo Serikali yake mwenyewe na vyombo vyote vya usalama, anabomoa utu na taaluma za watu.

Kama mtu aliye nje ya vyombo vya usalama anaweza kufanya haya basi vyombo vyote vya usalama vifutwe, tuunde upya kwa sifa na vigezo vingine, maana hatupo salama na hakuna maana ya kuwa navyo.
Tuwe na vyombo vya usalama vitakavyo zuia matukio mabaya na sio vinavyosolve matokeo ya matukio, wakati damu ya watu wasio na hatia imeshamwagika.
 
Nakuunga mkono%100 mkuu. MAPAMBANO NI MBELE HAKUNA KURUDI NYUMA..
Kila kitu kina gharama zake, hata nyerere angekuwepo leo angekusimulia masahibu aloyapata. Ni upumbavu mkubwa, kukata tamaa kwa sababu ya ccm kutumia vyombo vya dola.
 
Mwanaukweli ninashukuru kwa angalizo lako.

Kwanza niseme Multiparty democracy in 1992 ilikuja Tanzania wakati viongozi wa CCM na serikali yake walikuwa hawataki na hawakuwa wamejiandaa kwa mabadiliko hayo. Kama kusingekuwa na POLITICAL AND ECONOMIC EXTERNAL PRESSURE ninaamini nchi isingeingia kwenye huu mfumo wa kisiasa.

Kwa viongozi wengi wa kisiasa kipindi hicho ilikuwa ni vita kimaslahi ya kichama na katika hilo ndiyo tunapata leo matunda ya vita hivyo vya kimaslahi ambavyo kwa sasa vimechanganywa na vita vya maslahi binafsi kwa maana kuwa UTAIFA au UZALENDO haupo tena.

Mbinu na misingi ya kisiasa ambayo CCM ilikuwa imejijengea na kuimarika nchini ndiyo hiyo hiyo iliendelea kuitumia katika kukabiliana kisiasa na wanasiasa au chama kingine kilichoonekana kama ni tishio la kisiasa. Vyama vya siasa za kikomusti zilitumia mbinu za propaganda na pale iliposhindikana, zilikuwa zinatumia mpaka mbinu za kimafia kueneza siasa zake kwa kuwashughulikia "wakorofi"wa kisiasa.

Sikukatalii na ninakubaliana na wewe kuwa CCM imetumia sana mbinu "chafu" kisiasa, hizi ni pamoja na political character assassination kwa wanasiasa na vyama ulivyovitaja hapo juu.

Tatizo lililopo kwa sasa nchini ni kwa vyama vingine vya kisiasa ku-copy & Paste mbinu za kikomusti za CCM ambazo kwangu zimepitwa na wakati katika ulimwengu huu wa siasa wa karne ya 21 na kuanza kuzitumia kiasi kwamba kwa sasa inakuwa ni vigumu kujua kama nani ni SHETANI na nani ni MARAIKA katika ulimwengu huu wa siasa safi.

Kutenda kama CCM ni disadvantage kwa opposition parties kwa sababu hawana uzoefu na political strength kwenye siasa za aina ya kikomunisti.
Mkuu, hapo naomba unifafanulie kwenye hiyo nyekundu: Mbinu gani wapinzani walizo copy na ku paste?
 
Kila kitu kina gharama zake, hata nyerere angekuwepo leo angekusimulia masahibu aloyapata. Ni upumbavu mkubwa, kukata tamaa kwa sababu ya ccm kutumia vyombo vya dola.

Amezunguka wee lakini hafunguki,"tatizo ni CCM".
 
Kichwa cha habari hakiendani na content, edit heading, badala ya chadema eka ccm
 
Mkuu, hapo naomba unifafanulie kwenye hiyo nyekundu: Mbinu gani wapinzani walizo copy na ku paste?
Mkuu, maana yangu ilikuwa ni kwa CHADEMA kufanya siasa za character assissination na political rethoric zenye zero-sum game wakati haijawa entrenched kwenye public servants na pia hawana extra power zinazopatikana kwenye state organ kama Police, TISS, RC's and DC's.

CHADEMA wanapopanda majukwaani na kuanza kusema siku wakiingia IKULU watahakikisha mafisadi wote, viongozi wa serikali walioko madarakani, viongozi wa CCM na hata wafanya biashara wanaotegemea CCM kuwa huo ndiyo utakuwa mwisho wao, huko ni kufanya siasa za zero-sum game ambazo anayepata anachukua vyote na anayekosa anakosa vyote.

Hii ni statement ndogo lakini imebeba UZITO mkubwa katika mstakabali wa Taifa. Kuwaambia hawa watu na makundi kama kesho wataamukia magerezani, kufilisiwa na kufukuzwa kazi ina maana huko ni kugusa maslahi binafsi kwa maana kuwa siasa zinahama kutoka siasa za kitaifa au kichama na kuwa personal fighting. Ogopa sana pale binadamu mwenye nguvu ya kimfumo anapoanza kupigania uhai wake. Hata matukio ya ajabu yanayotokea nchini inawezekana yako chini ya uangalizi wa vikundi hivi (Individual power) kama issue ya Mwakyembe, Kibanda n.k.

CCM wamefanikiwa kuweza kuzicheza hizi kete za siasa za ulimwengu wa tatu kwa sababu nguvu za kimfumo wanazo na ndizo ambazo zimekisimika chama. Tumeona baadhi ya wafanyabiasha pale wanapotaka kujiengua kutoka CCM huwa wanashughulikiwa na wengine wana decide kurudi tena kwa kuogopa kushughulikiwa. Mfumo uliojengwa baada ya kuachana na Azimio la Arusha uliacha mianya ambayo wajanja ndani ya mfumo na baadhi waliokuwa nje waliitumia kujitajirisha dubiously. CCM inawafahamu lakini kwa vile wako ndani ya mfumo ndiyo maana huwezi kuona kama wana matatizo.

Kwangu mimi naona CHADEMA wangekuja na statement za political reconciliation ambazo haziyamegi makundi haya ya kijamii ambayo ndiyo yana nguvu kisiasa na kutoyafanya kuwa disenfranchised kwenye political process yao. CHADEMA wanapokuja na kauli mbiu na kusema peoples power wanasahau kuwa katika siasa za Tanzania kwa sasa kuna individual power ambayo ina nguvu zaidi ya peoples power. Politically, they can't afford to bypass individual power.

Haya makundi yanaweza yakawa yameichoka CCM lakini yanakosa pa kwenda kwa sababu hata CHADEMA wanadai hawapokei makundi kama haya kutoka CCM kwa sababu CHADEMA siyo pango lao kwa maana kuwa hayapati hata support kutoka CHADEMA to withstand CCM political and economic pressure wakiwa nje ya mfumo.

Ninatumaini nimeweka na kuboresha vizuri maelezo yangu.
 
Back
Top Bottom