Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,278
- 25,846
Sasa najua kuwa wagombea wawili waliopelekwa na CHADEMA Bungeni kwa ajili ya uchaguzi wa Wabunge wa EALA wamepata kura nyingi za HAPANA kuliko za NDIYO. Hivyo,wagombea Laurence K. Masha na Ezekiel D. Wenje wamekwama kuchaguliwa.
Jambo la kutia matumaini na kuwaliwaza CHADEMA ni kuwa nafasi zao zote mbili za EALA bado ziko wazi. Kwa maana hiyo,ni CHADEMA tu ndio watakaozijaza nafasi hizo. Tayari Tanzania tumeshapata Wawakilishi wetu saba kati ya tisa tunaopaswa kuwa nao.
Ili kuufanya mchakato kutokuwa na mikwaruzo na utata usio na msingi,CHADEMA ombeni muongozo wa Katibu wa Bunge na muwasilishe tena majina zaidi ya mawili Bungeni ili kujaza nafasi zenu mbili. Itawapasa kuufanya mchakato wa kuwapata wagombea wenu upya.
Nawashauri hivyo kwakuwa EAC ni suala la kitaifa zaidi ya kivyama. Wawakilishi ni wa Tanzania na si CCM,CUF wala CHADEMA. Hakuna haja ya kupambana kisiasa au kimahakama kwa masuala ya kitaifa. Hadi sasa,hakuna aliyekosea wala aliyepatia.
Ufafanuzi: EALA=East African Legislative Assembly
EAC=East African Community