thanx Killa for this useful post...I should hard code this thanks.
Eeeh, kama kawaida yenu wafata bendera wa Chadema, hampo objective kupinga hoja aliyotoa Tendwa, kazi kusema katumwa tu...well said!
It is clear kuwa mnatumiwa na wanasiasa bila kujua, wao wanahudhuria vikao, wanakubaliana, then hawaji kuwaambia ukweli . Hiki chama si makini, ni uchu wa madaraka tu. Hata kama sisiem wanakosea, ila CDM is not the right SUB either.
Inawezekana mkawa hamsomi hoja na kuzielewa, ngoja nimege kipande kidogo tu ili msome wavivu nyinyi:
nadhani chadema hawako wazi katika hili, kwani uhalali wa mary chatanda lilishatolewa ufafanuzi na katibu wa bunge. Sheria iko wazi na ilifafanuliwa na katibu wa bunge baada ya madiwani wa pande zote mbili kuonyesha utata walipokuwa katika kikao cha kwanza cha uchaguzi wa meya, ambapo vyama vyote viwili vilikuwa vikilalamikia ushiriki wa mjumbe mmoja mmoja kutoka kila chama.
Anasema ufafanuzi walioupata juu ya uhalali wa wabunge hao wa viti maalum waliokuwa wakilalamikiwa na vyama vyote viwili ni kwamba, sheria inawatambua wabunge kama madiwani wa sehemu wanazotoka na inaendelea kufafanua chama kinachowakilishwa na mbunge wa viti maalum, kitakuwa na haki ya kumpangia kazi sehemu yoyote isipokuwa hataruhusiwa kufanya kazi katika eneo lingine.
Anasema baada ya ufafanuzi huo utata wa suala la uwakilishi wa mbunge huyo wa viti maalum ukawa umemalizika na kwamba haelewi sababu za chadema kususa kuendelea na uchaguzi wa meya na kushangazwa na chama hicho kukwepa kueleza wafuasi wake suala hilo huku ikiendelea kushikilia msimamo wa kutomtambua mbunge huyo wa viti maalum wa ccm.
Uhalali wa uchaguzi wa meya
msajili anasema, baada ya kususia uchaguzi uliofanywa bila chadema kushiriki vyama hivyo viwili vinavyohusika katika suala hilo vilipaswa kuzungumza ili kupatikana kwa suluhu na kwamba yeye alikubali kuwa msuluhishi, lakini anasema hajui sababu ya chadema kuamua kuitisha maandamano kabla ya kumalizika kwa mazungumzo ambayo anasema anaamini yangeweza kuleta suluhu na kujenga amani miongoni mwao.
Anasema jambo moja ambalo haliko wazi na ambalo angependa chadema wakaliweka bayana ni kueleza wazi agenda yao, na nini wanachokitaka au wanachokusudia badala ya kufanya mambo ambayo kwa namna moja ama nyingine yanaweza kuhatarisha amani na kupunguza imani ya wananchi dhidi ya chama hicho.
haijulikani hasa wanataka nini, maana kama ni kweli ilikuwa uhalali wa mary chatanda walishasomewa sheria na wakaelewa. Awali walizungumzia suala la kutaka katiba, kila mtu aliunga mimi nimeunga mkono nimetoa maoni yangu, waziri mkuu naye kasema, na mwisho rais ameridhia, sasa waeleze wanataka nini ili madai yao yawe wazi na yaeleweke,
Semeni mnataka nini tuwaelewe....!