Waberoya,
CLinton family walimtukana sana Obama. Haikupita miezi kadhaa, walewale waliokuwa wakisema jamaa HAFAI, wakawa jukwaani wakisema jamaa ni MWOKOZI WA USA. Na watu hata hawakusema flip flops. Wakawa naye kwenye majukwaa yote na mwisho wako pamoja serikalini. Hii haikusemwa kuwa imevunja chama.
Iwe isiwe, Zitto kaweka NJIA. next time sijui kama watakuwa na uwezo wa kuzuia watu maana umma utakuwa mapemaaa unadai demokrasia ya kweli iwepo. Siwezi kuwa nachangia 300 kwa mwezi halafu nisikie Chadema ina wenyewe. Kama ina wenyewe basi si wachangie hizo 300 zetu? Kuanzia ilipojileta sokoni kuja kuomba nguvu kwa wananchi, imekosa mwenyewe. Kama wanataka iwe ya wachaga tu au wa kaskazini tu, ipelekeni huko Kibohehe na msiilete Dar kwa Wazaramo.
Nina uhakika na moja. Hiki chama very soon kitakuwa cha Watanzania. Watabana weee, mwisho wake wataachia. Na hapo Chadema itakokota watu kama kokoro. Mzee Mtei utakumbukwa tu kwa kuanzisha Chadema na heshima yako milele itakuwa kubwa. Ila ukianza kuharibu, basi historia itajua wapi ikuweke.
Naipenda film aliyocheza Antonio Banderas iitwayo THE 13th WARRIOR. Humo ndani kuna maneno "mtu akiishi duniani, na watu baadaye waje waichore (ichonge/andika) historia yake, basi huyo mtu ni TAJIRI". Mzee Mtei, USITAKE KUIHARIBU hiyo historia yako.