MgungaMiba
JF-Expert Member
- Aug 28, 2011
- 999
- 816
Ikumbukwe kuwa mwaka jana mnamo mwezi wa May/June CHADEMA mara baada kuzindua M4C pale Jangwani, DSM, operesheni hiyo ilielekea mkoani Mtwara na Lindi, kwa Mkoa wa Mtwara Operesheni hii ilikwenda kwenye majimbo yote sita na Kata nyingi kwa kila jimbo zilifikiwa, ingawa kwa bahati mbaya Operesheni hii ilikatishwa katika Mkoa wa Lindi kabla haujafikiwa wote kutokana na msiba wa Mzee Bob Makani. Viongozi Wakuu takriban wote walikwenda huko.
Agenda kubwa walioikuta ikiwa na mgogoro mkubwa huko ilikuwa ni suala la bei ndogo ya Korosho na kukosekana kwa malipo ya pili ya zao hilo. Jambo ambalo lilipelekea kutokea vurugu kubwa kwa baadhi ya maeneo kama vile Tandahimba.CHADEMA iliwaambia wananchi hao kuwa kwakuwa Wabunge wao hawawatei Bungeni, basi suala hilo watalibeba wao kwenda kuwawakilisha kwenye kikao kifuatacho cha Bunge.
Lakini CHADEMA ilienda Mtwara ikiwa na Agenda yake, Gesi, wananchi wengi wa huko hawakuwa na habari nayo wala kujua thamani yake halisi zaidi ya kuisikia kwenye vyombo vya habari. CHADEMA kwa makusudi iliamua kuwazindua wananchi hao kwa kuwaambia kuwa wakati wanaumizana kupigania bei ya Korosho, mali yenye thamani ya mabillioni (Gesi ya Asili) inahamishwa kutoka kwao, nao wataachwa hivihivi wakihangaika na bei duni ya Korosho, wakati viwanda vya kuprocess Gesi hiyo vinaweza kujengwa Mtwara na wao wakanufaika.
Aidha mikataba ya ovyo na taratibu zisizo naanufaa zitasababisha Gesi hiyo kunufaisha zaidi wawekezaji hao, Mafisadi wachache Serikalini, na Wananchi wataishia kubebeshwa mzigo mzito wa madeni ya gharama ya kuisafirisha Gesi hiyo na kuendelea kubaki kwenye lindi la umaskini, kama ilivyo kwenye maeneo yenye dhahabu nyingi. Ufafanuzi ulitolewa kwa ufasaha mkubwa na nini kilipaswa kufanyika ili Gesi hiyo iweze kuwaondoa kwenye umaskini na kulinufaisha Taifa kwa ujumla.
Miezi takriban sita sasa tangu Opereshen hiyo ifanyike, Serikali ilipuuza yote yaliyosemwa, kwa maana ina akili sana, ikaendelea na ilivyotaka, ikaenda kukopa Matrillioni kutoka China kwa mikataba ambayo ni rather dubious, ili iweze kuhamisha Ges hiyo kwenda Dar, kisha bila shaka deni hilo lije lilipwe kwa kodi za Wananchi haohao wanaoonekana hawana akili, wahaini nk.
Lakini ni dhahiri Wananchi wa Mtwara, lile somo liliwaingia akilini vizuri sana, wameamka, wamekataa na Ujumbe umefika, serikali inataka haitaki itabidi ifuate ushauri wa Mzee Mkapa, wasiwaite wananchi hao ni wahaini, bali wakae nao, wazungumze nao ili muafaka upatikane, ubabe wa serikali hautasaidia kwani Wananchi wakiamua kwa pamoja wanakuwa na nguvu kuliko Serikali.
Kwa wale wanaodai CHADEMA itoe tamko, sielewi wanataka tamko gani, kwani CHADEMA ilishatoa tamko lake kuhusu Gesi kwa kishindo kikubwa wakati wa Operesheni mpaka Mkoa mzima wa Mtwara ukatikisika na sasa Wananchi wameitika, kazi iko kwa Serikali, kusuka au kunyoa!