CHADEMA msisafirie nyota ya Gwajima!

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
21,443
40,537
Ni kosa kubwa sana kisiasa kumtegemea Askofu Josephat Gwajima kwenye kupambana na CCM na wafuasi wao. Kama si Gwajima Dr. Slaa angewasumbua sana CHADEMA 2015, kama si mzee wa "Single touch double manifestation" mpaka leo ishu ya Daudi Bashite ingekuwa imeshakufa na Mbowe angekamatwa na CHADEMA wangebakia kulialia kwamba wanaonewa.

Kuna jambo linazidi kupata nguvu kwamba tangu kuondoka kwa Dr. Slaa chamani kumekosekana mtu wa kupanga mikakati ya kisiasa. Huu ujinga wa kusubiri CCM ikosee ndiyo muibuke unawagharimu. Ni lini mtarudi kwenye njia kuu ya kuonesha njia mbadala ya kuongoza nchi yetu? Mmepigwa ganzi kwa Propaganda za CCM kwamba kwa kumpokea Lowassa eti ajenda dhidi ya Ufisadi imekufa!?

Hivi kwenu nyie mtu kutumia rasirimali za nchi kuendeleza eneo la kwao kwa kuwa tu ana madaraka si ufisadi? Hii nchi sasa inaendeshwa bila ya kusimamia vipaumbele vya kibajeti nyie mpo kimya sana. Nilipomuona "Rafiki" yangu Boniphace Jacob kwenye Ibada ya Gwajima nikajua sasa kama chama mmepotea njia.

Mange Kimambi anafanya kazi "yenu" na hata Wema Sepetu alipohamia CHADEMA Mange alitoa angalizo kwamba wanaokuja si lazima wabakie, wakija watunzeni. Lakini hata mnaonekana mnawajali basi? Hivi hata kama kuna ujanja ujanja kwenye kutekwa kwa Roma Mkatoliki nyie ni lini mliwahi kukaa na watu wa aina yake na kuwapongeza kwa kufanya kazi "yenu" bila hata ya kutumwa. Ney wa Mitego kwa nini alikwenda kule baada ya "kuachiwa" badala ya kuja kwenu?

Leo watu wote walikuwa wanaelekeza macho na masikio yao kwa Gwajima wajue atasema nini kuhusu Diamond. Lakini Diamond alikuwa anafanya kazi ya kuishambulia CHADEMA kwa kupitia mlango wa nyuma kwa kusambaza ujumbe wa hofu. Kwa nini watu wasiwe na hamu ya kusikia CHADEMA watasema nini kuhusu Diamond badala yake wasubiri Gwajima atasema nini?
 
Gwajima ana wish kila ugomvi umuhusishe ili apate ndoano ya kuvutia attentions kwenye kanisa lake.
Anajua akishakuwa popular & influential hata asipogombea uongozi vyama vya siasa vitamtumia na yeye kujiongezea ulaji.
 
Hoja yako imebase kwa rafiki yako Bonaphace Jacob kwamba kwanini yuko kwa Askofu?
Kuonekana kwake hakuna uhusiano wa chama kuwa kinamtegemea aseme ndio wapate hoja pale ni kanisani una haki hata wewe kuhudhuria mkuu.
 
Back
Top Bottom