CHADEMA msimpokee Makonda

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
26,512
Reaction score
40,197
Kufuatia taarifa za kufukuzwa kwake UVCCM ambapo ni wazi kwa hatua hiyo anaweza akachukua uamuzi wa kujitoa kutoka chama chake cha CCM na kutaka kujiunga na CHADEMA.

Mpaka sasa CCM na intelejensia yake wameshindwa kudhibiti kasi ya CHADEMA kukubalika kwa wapiga kura wengi, hivyo CCM kwa kusaidiwa na wataalam wa kijasusi wameandaa mbinu kadhaa za kuidhoofisha CHADEMA kwa kutengeneza mitafaruku ndani ya CCM ili makada wa juu watimkie CHADEMA kwa kazi maalum.

CCM inakufa, hivyo CHADEMA jipangeni vyema kushika dola.
 
Mkuu nakuunga mkono,haiingii akilini kina shonza wamefukuzwa siku nyingi na mda mrefu walikuwa mamluki halafu jana juzi wahamie CCM jana UVCCM inamfukuza Makonda halafu kesho anajiunga.
 
Mkuu nakuunga mkono,haiingii akilini kina shonza wamefukuzwa siku nyingi na mda mrefu walikuwa mamluki halafu jana juzi wahamie CCM jana UVCCM inamfukuza Makonda halafu kesho anajiunga.
...kabisa mkuu.

CCM wanaweza kufanya lolote ilimuradi wapate wanachokitaka. Hii ya Makonda ni trick.
 
Ni angalizo zuri, nimefanya kazi na Makonda katika kampeni za uraisi za mwaka 2005, ninafahamu mapenzi yake kwa CCM ni makubwa kiasi gani. Katu hawezi kuwa mwanachama mwaminifu wa chama kingine nje ya CCM. Atatusumbua kama Shibuda.
 
Ni angalizo zuri, nimefanya kazi na Makonda katika kampeni za uraisi za mwaka 2005, ninafahamu mapenzi yake kwa CCM ni makubwa kiasi gani. Katu hawezi kuwa mwanachama mwaminifu wa chama kingine nje ya CCM. Atatusumbua kama Shibuda.
Ingawa ana haki ya kikatiba kujiunga na chama chochote cha siasa, lakini CHADEMA wana haki kumkubali ama kumkataa.

Sasa kinachotakiwa ni kujenga kada mpya ya viongozi ambao hawana nasaba na CCM ili kuepusha madudu ya chama tawala kuendelea kutesa umma.
 
UKO SAWA,HAWA JAMAA NI HATARI NA SI WAKUAMINI KWA JAMBO LOLOTE NA HASA IKIZINGATIWA wanatapatapa mbaya.NI KAWAIDA NA LAZIMA KWA CHAMA CHOCHOTE MAKINI KUWA MAKINI ZAIDI KINAPOPAMBANA NA CHAMA TAWALA KILICHOFIKIA HATUA ZA MWISHO ZA UHAI WAKE HIVYO KUISHIWA HOJA NA NAMNA BORA YA KUONGOZA TAIFA HIVYO KULIINGIZA TAIFA KATIKA SIASA ZA GHILBA,VITISHO NA PROPAGANDA ZISIZO NA MASHIKO KWA WANANCHI.
 
CCM ya leo imejaa sumu inayoangamiza taifa.
Rasilimali za nchi zinatumika kwa shughuli za chama ndo maana wamejisahau hadi kufikia kujiona ha HAKI YA KUZALIWA ya kuitawala nchi hii.

CHADEMA chukueni hii tahadhari maana mengi yanakuja
 
Binafsi sisemi asipokelewe kabisa; inaweza ikatokea wakapokelewa kama wanachama kama ulivyosema kwa kuwa wanayo haki kikatiba, lakini chadema wasifanye haraka kuwaingiza watu kama hawa kwenye vyombo vya maamuzi ya chama. Ikiwa ni pamoja na kuwatumia kwa uangalifu majimboni mwaka 2015. Maana nina uhakika CCM wataweka mamluki wengi wa kuja kuchukua form za kugombea majimboni na baadaye kutangaza kujitoa ili kuwasafishia njia CCM.
 
Wataumia kigezo gani kumkataa?
Unajua kwanini USA inaiunga mkono Israel kwa nguvu zake zote?
What goes around comes around, kigezo watakachokitumia kumkataa Makonda ndicho kitakachokuja kutumika kumkataa mtu mnayemtaka na hapo ndipo kitachimbika.
Wakati mwingine ni bora kuweka hisia pembeni na kufuata sheria na kanuni...
 
Waje tu! lakini wasiwe na nguvu ili wasisumbue. Wengine ni mapandikizi kama Shibuda, lkn kwa vile tushamjua tunamuangalia tu apige sarakasi zake ambazo hazidhuru chama.
 
nafikiri aachwe aje kama anataka ila asiwekwe kwenye chombo cha maamuzi
 

Hata cdm siku hizi inatuma mashushushu kwenda ccm. Hawataamini siku hesabu zinawekwa mezani
 
hakuna kuogopa ogopa!muacheni aje kwani inteligensia ya chadema ni ya hali ya juu zaudi.angalia kina shonza walivyoumbuka!
 
Wew ni mshamba na una akili ya kutaka kula kama shonza,sasa dada ako shonza ana akiba coz ni mwanamke je wew!Fikiria ukombozi wa taifa hili,kama ni umaskini ulishapigika sana na vijisenti vya kodi yako unapewa hata hus2ki?Shauri yako shonza akizidiwa atavua chupi wew je!Acheoi upotevu wa mawazo miaka 50 hakuna maendeleo,afu bado mnarudi ccm,bora wangeenda kuuza miili yao kuliko kwenda kutafuta maisha ccm
 
Ni kweli kwamba CCM, inayokaribia Kufa, inajarbu kutumia njia mbalimbali kukwepa Kaburi! Ikiwemo ya kuwanunua Makada, wa Chadema, wenye njaa "Kali"na wanaofikiri kwa kutumia Matumbo, lakini pia kuwatimua Baadhi ya Viongozi wa wa Vijana, na kuwapa maelekezo ya Kujiunga na Chadema, ili Kukivuruga!

Kujiunga Chadema kwa Mwanachama aliye fukuzwa Ndani ya ccm ni Haki Kikatiba! Sasa ambacho kinahitajika ni kuwa Makini na watu hawa Mamluki, na hakuna haja ya Kuwapa uongozi wowote ndani ya Chama, hadi watakapo fikisha angalao miaka mitano.
Tujifunze kulingana na Makosa, hawa watu waliowahi kuwa Viongozi ndani ya chama cha Magamba Huwa hawabadiliki,Mfano. Muangalie Shibuda, Matata Meya wa Ilemela, na wengine wengi.

MUNGU IBARIKI TANZANIA!!!!
MUNGU IBARIKI CHADEMA!!!!
 
Mkuu nakuunga mkono,haiingii akilini kina shonza wamefukuzwa siku nyingi na mda mrefu walikuwa mamluki halafu jana juzi wahamie CCM jana UVCCM inamfukuza Makonda halafu kesho anajiunga.



NI sawa kuwa na wasiwasi wakuu, kuna wakati nilimhofia sana Ole milya kutokana na ukaribu wake kwa EL. lakini nikakukmbuka jinsi kina W. Kabouru walivyotulizwa nikagundua kua CDM ni chama makini sana.
Nilimhofia sana marando enzi zile nikahsi ni shshu flani sijaona madhara yake hadi sasa.
Mimi napendekeza apokelewe incase akiomba kwakuwa hatashiriki vkao vyvyte muhm zaidi ya kampeni za m4c ambazo atasaidia kuanika uozo wake mwenyewe........................
 
Ni angalizo zuri na la muhimu sana maana kuli-implement sioni kama kuna hasara.ni vema tuka waangalifu sana hasa dakika hizi za kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.kuna watu wengi tu watalipwa kwa fedha za walipa kodi waingie chadema na baadhi waliomo kuanzisha migogoro ndani ya chama cha chedema.angalia walichokifanya kina-shonza,leo wanasimama bila uoga katika majukwaa na kuvaaa kijana ishara ya magamba.watahutubia nini jukwaani kama sio kuzungumzia cdm na kupandikiza chuki na kutaka kukidhoofisha?wapendwa wote na hasa wapigania uhuru wa kweli tuichukueni tahadhali hii na tuifanyie kazi.
 
jamaa huyo ni shushushu alikuwa Muccobs miaka mingi sana, hafai kabisa huyo.
 
Huyo makondomu sawa alichopata xcm ina wenyewe alikuwa hajui eee kuwa malipo hapa hapa duniani
 

Akijileta wampokee tu kwani ni haki yake kikatiba na baada ya hapo probation period/bench kama mie miaka mitano kupima somo la uvumilivu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…