Ndugu wadau, mimi nilikuwa mfuatiliaji sana wa Siasa za CHADEMA lakini ninachokiona sasa ni kama hawa ndugu zangu wameshindwa Siasa kabisa.
Mtawala amewazuia kufanya mikutano ya hadhara kinyume kabisa na Katiba ya Nchi, na wao wamekubali na hawajachukua hatua zozote zenye mashiko zaidi ya kusubiri kile kinachoitwa maridhiano.
Nilichojifunza ni kwamba, mtawala ameshajua udhaifu wa CHADEMA ulipo. Kwa hiyo anawaendesha atakavyo.
Tusishangae siku moja mtawala akiwazuia CHADEMA kuvaa sare za chama chao hadharani. Kwa hali kama hii, bila shaka watatii na kisha wataanza malalamiko na kelele nyingi kwamba wameonewa. Kitakachofuata, mtawala atawataka kuingia kwenye maridhiano eti ya kujadili kuvaa sare za chama chao. Bila aibu, watakubali kuingia kwenye maridhiano hayo.
Nawauliza ndugu zangu wa CHADEMA, ivi mtawala angewazuia kula Chakula mngekubali kirahisi namna hii?
Au mtawala angewaambia mtembee bila nguo kabisa mngekubali kirahisi namna hii?
Haya yote yanadhihirisha kwamba bado hampo serious na hamjakomaa kisawa sawa kushika dola.
Kama mnashindwa kupambana na adui wenu wa ndani, je, mkishika dola mtaweza kupambana na adui wa nje?
Si mtatishwa kidogo tu, kisha mnachuchumaa.
Kama mngekuwa serious kabisa, hamkutakiwa hata kidogo kukubali kutofanya mikutano ya hadhara.
Au hata sasa mlitakiwa kuwa mmeshaanza kufanya hiyo mikutano ya hadhara ili muone mtawala atachukua hatua gani dhidi yenu.
Kama hatua kali zingechukuliwa dhidi yenu kutokana na kufanya mikutano ya hadhara, mngeanza ku deal na hatua hizo ikiwa ni pamoja na kufanya maandamano ya Amani kupinga hatua hizo za mtawala.
Karibuni wadau.
Ndio maana muda mwingine huwa naomba raia waumizwe haswa ili akili zikae Sawa.Huwa wanakwaza Sana. Wanajifanya kuipenda CCM mambo yakiwa magumu wanailaumu CHADEMA.
Kichaa wewe unaeokosa logical reasoning!CDM inaweza kuwa na Wanachama wasiopungua 5,000,000 au zaidi Nchi nzima, je, ni lini waliandamana Wanachama hao wote 5000000 wakapigwa risasi au wakawafunga wote gerezani?
Jitu linaongezewa bei ya Petrol au Bando la simu linasema chadema inabidi imteteeUmejibia vema mkuu,uzuzu wenye uoga wa mtoa hoja hii ndio tatizo kubwa, yeye analala na kujificha chini ya uvungu wa kitanda huku akitegemea CDM ndio impiganie haki zake, kutwa kulalama humu wakati wana uoga wa kipuuzi, push back kwa haki yako sio kutegemea upiganiwe
Ndo maana nimesema, CDM bado hamjaiva. Kama mnatishwa kidogo tu mnaufyata, je, mkishika dola mtaweza kuhimili vitisho vya Mabeberu?Umejibia vema mkuu,uzuzu wenye uoga wa mtoa hoja hii ndio tatizo kubwa, yeye analala na kujificha chini ya uvungu wa kitanda huku akitegemea CDM ndio impiganie haki zake, kutwa kulalama humu wakati wana uoga wa kipuuzi, push back kwa haki yako sio kutegemea upiganiwe
Upumbavu mwingine huu,mabeberu ndio akina nani wakati ndio wanaotoa 40%ya budget yako ya kuendesha nchi?,CDM isingeipeleka nchi vitani kisa urafiki wa Nyerere na Obotte, ule ulikua uamuzi butu, na elewa hata hizi juhudi za kuikomboa SA ,watanzania hatuna chetu kule, Kenya wanafanya biashara kubwa na SA kuliko Tanzania na wamepewa haki ya e Visa ya SA, sisi bado ni 90days kwa mwaka, pigana vita yako usitegemee watu wakupiganie wakati wewe umefwata mkia wako na unatumia nguvu nyingi kulalama humu kwenye soft landingNdo maana nimesema, CDM bado hamjaiva. Kama mnatishwa kidogo tu mnaufyata, je, mkishika dola mtaweza kuhimili vitisho vya Mabeberu?
Ingekuwa CDM imeshika dola wakati wa vita vya Tanzania na Uganda bila shaka tungekuwa tulishapigwa vizuri kabisa.
Maana, Idd Amin angewatisha kidogo tu na ninyi mngemwachia Nchi.
Hapo kuna tatizo. Hadi leo hii unaamini kuna Nchi wanatupatia sisi misaada; Are you serious?Upumbavu mwingine huu,mabeberu ndio akina nani wakati ndio wanaotoa 40%ya budget yako ya kuendesha nchi?,CDM isingeipeleka nchi vitani kisa urafiki wa Nyerere na Obotte, ule ulikua uamuzi butu, na elewa hata hizi juhudi za kuikomboa SA ,watanzania hatuna chetu kule, Kenya wanafanya biashara kubwa na SA kuliko Tanzania na wamepewa haki ya e Visa ya SA, sisi bado ni 90days kwa mwaka, pigana vita yako usitegemee watu wakupiganie wakati wewe umefwata mkia wako na unatumia nguvu nyingi kulalama humu kwenye soft landing
Ndo maana nimesema, CDM bado hamjaiva. Kama mnatishwa kidogo tu mnaufyata, je, mkishika dola mtaweza kuhimili vitisho vya Mabeberu?
Ingekuwa CDM imeshika dola wakati wa vita vya Tanzania na Uganda bila shaka tungekuwa tulishapigwa vizuri kabisa.
Maana, Idd Amin angewatisha kidogo tu na ninyi mngemwachia Nchi.
Sawa kabisa. Mbowe alibambikwa kesi ya Ugaidi na akakaa Rumande kwa muda mrefu tu.Kwa taarifa yako, watu wamefungwa, wamepata vilema vya maisha na ww haukuonekana. Umebaki unaagiza tu wakati huna mchango wowote. Akina Mbowe si ndio walipewa mpaka kesi ya ugaidi kwa kufanya makongamano ya katiba mpya huku serikali ikiwa imekataza mikutano? Huko mahakamani hakimu si ndio alikuwa anatupilia mbali mapingamizi ya CDM, huku akikubaliana na ushahidi wa jamhuri hata kwa ushahidi uliokuwa unaonyesha ni wa kutunga kabisa? Inshort uko kinadharia zaidi lakini huna lolote ujualo.
Sawa kabisa. Mbowe alibambikwa kesi ya Ugaidi na akakaa Rumande kwa muda mrefu tu.
Swali langu linabaki palepale kwamba, CDM mmeshindwa Siasa?
Ni hivi, Wanachama wa CDM Nchi nzima wanaweza kuwa hata zaidi ya 5,000,000.
Je, Mbowe alipokuwa yupo ndani kwa kesi ya kutengenezwa, ni Wanachama wangapi wa CDM waliandamana Nchi nzima kupinga kitendo hicho?
Hapo napo mlitaka waanze kwanza kuandamana Wanachi?
Hoja yangu kwa CDM ni ile ile kwamba kwa sasa CDM ni kama mmeufyata hivi kwani hamuoneshi kama kweli mna nia thabiti ya kushika dola.Kwahiyo kutokuandamana ndio kutokufanya siasa? Hoja yako ni nini hapa, ni maandamano au kufanya siasa? Hebu tuwekane sawa kwanza ili tujue unataka nini.
Hoja yangu kwa CDM ni ile ile kwamba kwa sasa CDM ni kama mmeufyata hivi kwani hamuoneshi kama kweli mna nia thabiti ya kushika dola.