CHADEMA, mmeshindwa Siasa?

Daisam

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2016
Posts
2,622
Reaction score
3,147
Ndugu wadau, mimi nilikuwa mfuatiliaji sana wa Siasa za CHADEMA lakini ninachokiona sasa ni kama hawa ndugu zangu wameshindwa Siasa kabisa.

Mtawala amewazuia kufanya mikutano ya hadhara kinyume kabisa na Katiba ya Nchi, na wao wamekubali na hawajachukua hatua zozote zenye mashiko zaidi ya kusubiri kile kinachoitwa maridhiano.

Nilichojifunza ni kwamba, mtawala ameshajua udhaifu wa CHADEMA ulipo. Kwa hiyo anawaendesha atakavyo.

Tusishangae siku moja mtawala akiwazuia CHADEMA kuvaa sare za chama chao hadharani. Kwa hali kama hii, bila shaka watatii na kisha wataanza malalamiko na kelele nyingi kwamba wameonewa. Kitakachofuata, mtawala atawataka kuingia kwenye maridhiano eti ya kujadili kuvaa sare za chama chao. Bila aibu, watakubali kuingia kwenye maridhiano hayo.

Nawauliza ndugu zangu wa CHADEMA, ivi mtawala angewazuia kula Chakula mngekubali kirahisi namna hii?

Au mtawala angewaambia mtembee bila nguo kabisa mngekubali kirahisi namna hii?

Haya yote yanadhihirisha kwamba bado hampo serious na hamjakomaa kisawa sawa kushika dola.
Kama mnashindwa kupambana na adui wenu wa ndani, je, mkishika dola mtaweza kupambana na adui wa nje?

Si mtatishwa kidogo tu, kisha mnachuchumaa.

Kama mngekuwa serious kabisa, hamkutakiwa hata kidogo kukubali kutofanya mikutano ya hadhara.
Au hata sasa mlitakiwa kuwa mmeshaanza kufanya hiyo mikutano ya hadhara ili muone mtawala atachukua hatua gani dhidi yenu.

Kama hatua kali zingechukuliwa dhidi yenu kutokana na kufanya mikutano ya hadhara, mngeanza ku deal na hatua hizo ikiwa ni pamoja na kufanya maandamano ya Amani kupinga hatua hizo za mtawala.

Karibuni wadau.
 
CCM ni sharti ifumuliwe kutokea ndani kama Jiwe alivyokuwa anaifanya. Upinzani wa Chadema na ACT ni sawa na uchumia tumbo hauna maslahi kwa raia wakawaida ila wenye vyama, na ndio maana "rais" pendwa Dr. Slaa alishikishwa mapene akasahau harakati, kuna dodoso Aikaeli kalamba asali saa hizi anadai bitozo anaupiga mwingi.
 
chadema imeshagundua inapigania mapumbavu ndio maana imeyaacha yajifie natural death
 
chadema imeshagundua inapigania mapumbavu ndio maana imeyaacha yajifie natural death
Jitu limelala kitandani linaongezewa gharama za bando. Linaingia Mtandaoni na kulalamika kuwa chadema haijapigania bando isipande.


Watanganyika ni wapumbavu Sana Bora waandamane Kwasababu ya diamond au zuchu na sio maisha yao

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Umenena !!
 
Wakati huo wanaanza kufanya hayo ww umejifungia chumbani!! Baada ya hapo utarud hapa na kusema CDM wanataka kutuletea machafuko na vita!! Kwasasa watanzania sio wa kuwapigania wazee ni mpaka pale watakapo jitambua!!
 
Hapo ndipo mnapofeli CDM.
Ninyi ndo mlioiva kiitikadi. Badala ya ninyi kuongoza maandamano, kinyume chake mnasema eti kila Raia apambane yeye mwenyewe. Huku ni kukwepa majukumu yenu ya Msingi katika siasa kwa kisingizio hicho.

Wanachi watawaunga mkono ikiwa tu kwanza ninyi wenyewe mmeonesha nia hiyo kwa vitendo.

Mtu atakupokea jembe kulima shamba ukiwa shambani, na siyo nyumbani.
 
Wakati huo wanaanza kufanya hayo ww umejifungia chumbani!! Baada ya hapo utarud hapa na kusema CDM wanataka kutuletea machafuko na vita!! Kwasasa watanzania sio wa kuwapigania wazee ni mpaka pale watakapo jitambua!!
Ndo maana nimeuliza, CDM mmeshindwa Siasa?
Wajibu wa chama cha siasa ni kuwaoganize Wananchi, lakini huwezi ku organize ukiwa nyuma, bali ukiwa mstari wa mbele.
Kama mnasema Watanzania siyo wa kuwapigania, basi huko ndo kushindwa siasa. Sasa mnatafuta maridhiano ya nini?
 

Kwa taarifa yako, watu wamefungwa, wamepata vilema vya maisha na ww haukuonekana. Umebaki unaagiza tu wakati huna mchango wowote. Akina Mbowe si ndio walipewa mpaka kesi ya ugaidi kwa kufanya makongamano ya katiba mpya huku serikali ikiwa imekataza mikutano? Huko mahakamani hakimu si ndio alikuwa anatupilia mbali mapingamizi ya CDM, huku akikubaliana na ushahidi wa jamhuri hata kwa ushahidi uliokuwa unaonyesha ni wa kutunga kabisa? Inshort uko kinadharia zaidi lakini huna lolote ujualo.
 


Nadhani pona pona ya CCM kwa Sasa ni CHADEMA kutokuwa na kauli. Ndio maana wamewaficha kwenye maridhiano ya kinafiki. Kusema ukweli haya maridhiano yatazama na CHADEMA Kama hawatawastukia CCM mapema.
 

Usimlinganishe ACT na CHADEMA. CHADEMA ipe heshima yake. Mpaka ACT ipitie CHADEMA waliyoyapitia siyo leo.
 

Tofautisha ujinga na hekima. Viongozi wa CHADEMA wamefunguliwa kesi ngapi?. CHADEMA waliitishha ukuta nyie wenyewe mkawacheka, mkawa mnadai mnasubiri kuona wanavyopewa kipondo.

Mbowe alipokuwa na kesi ya ugaidi ulifika hata mahakamani?. Punguza unafiki , vyama vipo vingi , nenda TLP au NCCR , CHADEMA haitaki wanafiki Kama wewe.
 
Kulikuwa na tamko kuwa mwisho wa mwezi huu kutakuwa na kikao cha kamati kuu ya chadema. Sijui kitakuwepo!
 

Huwa wanakwaza Sana. Wanajifanya kuipenda CCM mambo yakiwa magumu wanailaumu CHADEMA.
 

Kipindi Chadema wanafanya harakati mnadai Chama Cha vurugu, wakitulia ni Chama Cha maslahi. Maslahi gani iliyonayo CHADEMA haina mbunge Wala diwani, au haipokei Ruzuku.

Bakini na CCM yenu , CHADEMA itajengwa na wanachadema wenyewe.
 

Mbona hao wananchi hawakuunga mkono harakati za UKUTA wakabaki wanasubiria kuona polisi na JWTZ watakavyoua Viongozi wa CHADEMA. Mbowe juzi kaongea ukweli wananchi hawajitokezi hata Kama ni maandamano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…