ally ngomanzito
Member
- Oct 7, 2015
- 86
- 108
Viongozi wa greater Dar Es Salaam wakati wa kikao na waandishi wa habari mapema hii leo wakitoa maazimio yao dhidi ya ubaguzi unaofanywa na kituo cha television ya TBC dhidi ya upinzani.
Wamesema wanatoa onyo kali na la mwisho kwa TBC maana ni chombo cha umma kinachoendeshwa kwa kodi za watanzania hivyo kiache kuendeshwa kwa minijali ya CCM tu.
Pia katika kikao hicho viongozi wa Dar es salaam kuu wameongelea zoezi linaloendelea chini ya serikali ya rais Magufuli la utumbuaji majipu na kubainisha ni kiini macho kwa watanzania.akifafanua zaidi katibu Ndugu Kileo amesema anachofanya magufuli kwanza ni ukiukwaji wa sheria za nchi za ajira kazini ya mwaka 2004 lakini pia ni kinyume cha uongozi wa kidemokrasia ambapo kila mtu anahaki ya kusikilizwa na simaamuzi ya upande mmoja tu.
Zaidi Mh Kileo amesema kinachofanyika ni kiini macho kwa sababu CCM inataka kujisafisha na uchafu huo wa jiji uliotendwa na Meya aliyepita ambaye ni mwanachama wa CCM Mh Masaburi kiuhalisi mkurugenzi hapitishi mkataba bila kuwepo saini ya Meya na kamati ya mahesabu kuidhinisha hivyo basi wao wanamtaka Mh Magufuli kudeal na watendaji wazembe kwani hata wao wasingelea wazembe ila kwa kufuata utaratibu wa kisheria na si mabavu.
Mh Kileo amesema anachofanya rais Magufuli sasa ni kupanga safu yake ya uongozi ambapo katika kuwatoa wale wateule wa Kikwete ameamua kutumia hii njia ya majipu na sivinginevyo.
Hakihitimisha kikao hicho Mh Kileo amesema wao kama kamati kuu ya dar es salaam kuu pia wanasikitishwa na ubaguzi unaofanywa na serikali dhidi ya mameya wanaotokana na ukawa.kwa kile kilichotokea juzi kwenye uzinduzi wa daraja la kigamboni na hata ile kauli aliyotoa mh raisi wakati wa uzinduzi wa mradi wa kinyerezi 2.