CHADEMA lipeni hawa watu mishahara

CHADEMA lipeni hawa watu mishahara

Joined
Jun 30, 2013
Posts
21
Reaction score
14
Mimi ni mwana Chadema ambaye msimamo wangu juu ya chama changu hautiliwi shaka.Lakini kwa hili naomba nikiombe chama changu na viongozi wangu wa juu kuwa,wakati umefika wa kuwalipa mishahara viongozi wa Wilaya na Mikoa hasa Wenyeviti na Makatibu.

Si kweli kwamba ni viongozi wa Makao Makuu ya Chama tu ndiyo wanaofanya kazi kubwa inayostahili malipo.Kazi inayofanywa na viongozi wa ngazi za chini pia ni kubwa ambayo kuna kila sababu ya kuwalipa mishahara watu hawa. Viongozi wa mikoa na Wilaya kwa muda wamefanya kazi za chama na kuacha hata majukumu yao ya kifamilia kwa kujitolea tu.

Wakati umefika sasa chama kiwalipe mishahara ili wafanye kazi za chama kwa ari zaidi. Zile nyimbo za kuwa chama hakina fedha zimepitwa na wakati. Haiwezekani wakurugenzi wa chama makao makuu wakalipwa zaidi ya 1m halafu zikosekane hata sh laki 3 za kuwalipa viongozi wa mikoa na wilaya.

Nawasilisha.
 
Ndio maana akina Mbowe hawaliamini Baraza Kuu la Taifa la Chadema kuhusiana na sakata la Zitto kwasababu wanajua fika kule hawakubaliki na wale Viongozi wa Mikoani na Wilayani ambao kimsingi ndio huunda Baraza kwa asilimia kubwa.Mbowe na wenzie hawataki kushea keki ya Chama na Viongozi wa Mikoani.
 
Naunga mkono hoja

wazo hili lina afya sana kwa chama, tatizo ni kwamba mwenyekt anatafuna ruzuku za chama (ambazo kimsingi ndo zingewalipa hawa watumishi wa chama) na yeyote anayehoji anaitwa msaliti mfano wa kwanza ni chacha wangwe (rip) na sasa akina zito.............
anayepinga asome nyaraka zote mbili, ya marehemu wangwe kisha ya akina zito.
tatizo ni mahaba ya ajabu dhidi ya mbowe kutoka kwa wafuasi wake na kwa staili hii mabadiliko tuyatakayo itakuwa ni ndoto za mchana tu!!!
 
Katiba mpya iondoe huu UPUUZI wa vyama vya siasa kupewa RUZUKU na serikali.

Tafsiri tuliyopewa jana na Judge Utamwa ni kwamba VYAMA VYA SIASA NI VYAMA VYA HIARI. Hivyo mtu kama amejiunga na vyama vya siasa maana yake umekubali KUJITOLEA. Kupewa ruzuku vyama vya siasa ili kuwalipa wanachama/viongozi wake waliomua KUJITOLEA kutumikia vyama hivyo ni kupoteza pesa yetu kodi.

Leo mathalani Simba, Yanga, Azam etc ikadai nayo wenyeviti wao na makocha walipwe na serikali posho/mishahara kwa maana ya serikali kutoa ruzuku kwa timu hizo itawezakana?

Stop this madness the govt URP.
 
CCM wanalipwa shilingi ngapi kwa mwezi ukichukulia ni chama tajiri,kinatumia rasilimali za watnzania zilizoibiwa mapema MWAKa 1992, zinazoibiwa sasa toka seriklin au mndhani hatujui kuwa wenyeviti wa halmashauri ni wajumbe wa kamati za siasa za wilaya?
wazo hili lina afya sana kwa chama, tatizo ni kwamba mwenyekt anatafuna ruzuku za chama (ambazo kimsingi ndo zingewalipa hawa watumishi wa chama) na yeyote anayehoji anaitwa msaliti mfano wa kwanza ni chacha wangwe (rip) na sasa akina zito.............
anayepinga asome nyaraka zote mbili, ya marehemu wangwe kisha ya akina zito.
tatizo ni mahaba ya ajabu dhidi ya mbowe kutoka kwa wafuasi wake na kwa staili hii mabadiliko tuyatakayo itakuwa ni ndoto za mchana tu!!!
 
Naunga mkono hoja 100%.Hii sasa inapaswa kuwa aibu kwa Chadema.Ni ajabu chama kinachopigania maslahi mazuri ya watumishi wa umma na umma mzima wa watanzania kinashindwa kwa makusudi kabisa kuwalipa viongozi wake wa mikoa na wilaya.
Katika thread hii tuache u pro Zitto na Mbowe tujadili hoja ili kilio hiki kisikike.
 
CCM wanalipwa shilingi ngapi kwa mwezi ukichukulia ni chama tajiri,kinatumia rasilimali za watnzania zilizoibiwa mapema MWAKa 1992, zinazoibiwa sasa toka seriklin au mndhani hatujui kuwa wenyeviti wa halmashauri ni wajumbe wa kamati za siasa za wilaya?

mkuu, mada iliyombele yetu ni namna gani chama kiwalipe watendaji wetu mikoani - mambo ya maccm yanakujaje hapa tena?!
by the way, chadema haipaswi kuendesha shughuli zake kwa kuiangalia ccm yenyewe imefanya nn.
 
mkuu, mada iliyombele yetu ni namna gani chama kiwalipe watendaji wetu mikoani - mambo ya maccm yanakujaje hapa tena?!
By the way, chadema haipaswi kuendesha shughuli zake kwa kuiangalia ccm yenyewe imefanya nn.

umemjibu vizuri sana,
 
Kumbe hawalipi????? Sasa hii ela yote ya ruzuku inaishia wapi??
 
mkuu, mada iliyombele yetu ni namna gani chama kiwalipe watendaji wetu mikoani - mambo ya maccm yanakujaje hapa tena?!
by the way, chadema haipaswi kuendesha shughuli zake kwa kuiangalia ccm yenyewe imefanya nn.
Safi mkuu,jibu zuri sana. tatizo la kutojitambua ndio kama hilo,hoja nyingine unaingiza hoja nyingine
 
Amenijibu vizuri wapi? Hapa mwanga tuna vitongoji viwili tu vya CDM lakn makao makuu ya cdm wanatuma fedha za kulipia pango la ofisi, shajara na posho za viongozi wa wilaya ingawa si kubwa lkn makao makuu wanajitahidi tofauti na mnavodhani kuwa fedha hazishuki wilayani!
umemjibu vizuri sana,
 
Amenijibu vizuri wapi? Hapa mwanga tuna vitongoji viwili tu vya CDM lakn makao makuu ya cdm wanatuma fedha za kulipia pango la ofisi, shajara na posho za viongozi wa wilaya!
Nimekusaidia kubold na kuongeza size ili ulisome hilo jina, wilaya hiyo ipo kaskazini na ndipo pesa yoooooote ya chama inapelekwa.
 
Back
Top Bottom