CHADEMA kuweni realistic

CHADEMA kuweni realistic

Mugisher

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
411
Reaction score
360
Sasa nataka niseme hivi, ukisoma thread nyingi huku JF (sio zote) watu wengi wanachukua mawazo yao binafsi nakuyafanya ni ya utafiti. This is typical ya wachangiaji ambao hawako sober, ambo ni wengi huku JF. Na mawazo mengi ni kuwa (1) Fisadi Lowassa anakubalika na tafiti nyingi zimeonyesha hivo (2) CCM wamepotea kwenye ulingo wa siasa au wamekuwa wakimya (3) Fisadi Lowassa ameipasua CCM katikati (4) adui ni CCM si Fisadi Lowassa.

Kwa minajili ya kuwasaidia wale ambao kwamwe hawapendi kusaidiwa (kama utakavyoona wanavyochangia), naomba niwaelekeze kwenye indicators hizi:

(a) Kama kulikuwa na tafiti yoyote iliyomuonyesha kukubalika kwa Fisadi Lowasa, tafiti hiyo ilifanyinka kipindi Fisadi Lowassa yupo CCM. Sasa kubali au kataa, backbone ya umaarufu Fisadi Lowassa ni CCM. Hamna tafiti iliyofanyika akiwa nje ya CCM. Kwa hivyo basi, kutumia tafiti za kale kuzileta katika mazingira ya sasa ni kupotoka.

(b) Kule Kenya, katika tafiti karibia zote, Raila alionekana ni mshindi wa kiti cha urais lakini haikuwa hivyo. Kwa hivyo basi, kuwa sana mwangalifu nazo, hata kama zinaonyesha Jembe-Jembeka Magufuli atashinda kwa asilimia 70.

(c) Tafiti zote zinategemea ni study sample gani iliyochukuliwa. Ukichukua sample ya waendesha bodaboda basi Fisadi Lowassa ni Rais leo hii. Sasa ukiwa ‘mfu' wa akili kama Mazombie wengi unakaribisha magonjwa ya moyo ambayo si ya lazima sana kwa sasa. Nchi bado inakupenda- tambua hilo.

(d) Kipenga cha campaign bado hakijalia. Sasa unataka CCM wajisumbue na nini sasa hivi. Kama kulivyokuwa na shamrashamra za kutolewa mwali Jembe-Jembeka Magufuli na sasa hivi ni haki ya CDM (Mazombie) kuwa na shamrashamra za mgombea wao, ambaye ni Fisadi mwenzao. Sioni kuna ajabu gani hapa. Hii ndio demokrasia.

(e ) Kama nilivyoandika huko nyuma, kupasuka kwa CCM hakupo. Bado hatujaona mpasuko huo wa viongozi au wafuasi kumfuata huyo Fisadi Lowassa huko CDM. Kama Fisadi ni true statesman, a visionary leader tungeona lukiki ya wafuasi wakimfuata. Mimi sijaona..labda mnitumie picha. Kwa MazombieCDM ni lazima umaarufu wake uje na numbers CDM, au utakuwa umaarufu wa vichwa vya habari tu.

(f) Chama lazima kiwe na misingi yake na ikitete kwa all cost. Chama will always be there, but leaders and members will come and go. Leo hii huwezi kuua misingi hiyo kwasababu ndogo tu ya kuingoa CCM kirahisi rahisi tu, na kwenda kinyume na misingi yako, kwa kuvaa gamba la ufisadi lilolivuliwa na CCM. Nakubaliana siasa ni a game of numbers, lakini kwenye siasa pia lazima uwe na realistic strategies (na sio tu a stratergy) au sio utarudi nyuma hatua mbili.

Hivo basi epuka kuiteteresha afya yako kwa kuwa REALISTIC.
 
Pamoja na kuuleta uzi wako kwa kichwa cha kushtua na vijembe na kejeli nyingi naomba nikuambie watanzania walio wengi wanachagua mtu na sio chama. chama cha ccm kinapata ushindi wake mwingi kwa kutegemea tume isiyo huru ya uchaguzi na mbeleko ya jeshi la polisi isiyojua wajibu wake.
 
Pamoja na kuuleta uzi wako kwa kichwa cha kushtua na vijembe na kejeli nyingi naomba nikuambie watanzania walio wengi wanachagua mtu na sio chama. chama cha ccm kinapata ushindi wake mwingi kwa kutegemea tume isiyo huru ya uchaguzi na mbeleko ya jeshi la polisi isiyojua wajibu wake.


Tanzania ya sasa watu walio na ufahamu kama wewe ni wachache saaanaaa! Lakini poa utajielewa tuu. Mchana mwema.
 
Hiyo dicription yako wasomi tutakucheka...napata shak na uelewa wako mleta uzi

Wapigaji kura wote ni wasomi? Hebu niambie ni wasomi wangapi wanapiga kura? Usiwe unaandika tu just for the sake of it. Nyie ndio mnatia aibu JF. Inaonekana ni genge la CHADEMA. Ngoja nirudi tena, tatizo kubwa la wachangiaji wengi kama wewe ni kukandia tu..lakini nyie wenyewe hamuandiki kitu. Kama wewe sasa umekandia tu lakini kucounter mawazo yangu kwa opinion yako au fact huwezi. Wewe ni representation ya wengi waliokuwepo JF. Usiwe kama jamaa mmoja alinikandia kwa kukosea spelling (kama wewe hapo juu)... just that. Lakini kwenye mantiki ya issue hacomment.
 
Mugisher

inaelekea wewe ni mhaya au mchaga lazima uweke kiingereza kuongeza msisitizo.
 
Last edited by a moderator:
Khaa!! Huu ni moja ya uzi ambao walevi wa JF hawapendi kusoma na kuelewa. Serikali inabidi iongeze mochwari pamoja hospitali za kutibu magonjwa ya akili. Tukutane October :glasses-nerdy:
 
Sawa lakini embu mambo yako binasfi unayawekaje humu mbona Kuna jukwaani la unakubali kwa nini use post huko unrealistic wako hapa ni upi mmmmmmmmh
 
Napenda kuisoma JF ili nijifundishe kiswahili sasa nikiona kiingereza inanipotezea hamu.

Kaka binadamu ni watu wakusameheana. Nisamehe hivi hivo. Hata wewe usidhani kila unachokiandika unawakosha wote. Kuna wale wachahce pia hawapendi kusoma kiswahili sasa tuwatenge?
 
kweli kabisa umeongea mambo ya msingi... hatuwez kuyumbshwa na siasa uchwara za kuchafuana alafu leo wanawakumbatia,never
 
Back
Top Bottom