Siku kadhaa zimepita tangu nilipokutana na Prof. Abdallah Safari maeneo ya Posta Dar es salaam ambaye pamoja na kusema anahama Chadema wakati wowote alimtupia lawama Mhe. Mbowe na kikundi chake cha kina Sugu, Msigwa, Mdee, Lema na wengineo kuwa wanakiharibu chama. (Nisiingie kwa undani kuhusu hilo maana sio lengo la thread hii) lakini Prof akatoa 'compliment' kwa ndugu Kigaila kwa kusema kwa kimombo...'he is excellent'!
Wakati mwingine nilikuwa Dodoma kikazi ikawa kama coincidence nilikutana na Cecil Mwambe ambaye na yeye pamoja na mameno yake kufanana na ya Prof lakini alisema Kigaila ndio mtu pekee ambaye angeweza kukiunganisha Chama na kwamba ni mtu asiyefisadika!
Baadhi ya wajumbe wa Kamati kuu kwa nyakati tofauti walionekana 'kumpenda' Kigaila.
Kigaila ana nini? Kwa nini wote wanaoondoka Chadema na wenye mpango wa kuondoka Chadema wanasema wasingeondoka kama Kigaila angekuwa Mwwnyekiti Chadema?
Sent using
Jamii Forums mobile app