Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Kwa mujibu wa taarifa ambazo nimepenyezewa na wanyetishaji wangu wa kuaminika zinaeleza kuwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kinajipanga kutoa sapoti ya nguvu katika ahadi ya Mh Edward Lowassa, Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, ya Kuwasaidia chakula wananchi ambao wanakabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula kutokana na ukame uliolikumba taifa huku Serikali ikigoma kutoa msaada wowote.
CHADEMA wamepanga kuutangazia umma wakati wowote utaratibu mzima wa zoezi hilo la kumuunga mkono Mh Lowassa, mwanasiasa ambaye ametokea kuwa kipenzi cha watu kwa nyakati zote, mwenye upendo, mpole na asiye na majivuno.
Mpango huo unakuja kukiwa na ukimya mkubwa miongoni mwa taasisi za kijamii na kupuuzwa kwa tatizo la njaa kwa baadhi ya maeneo kwa sababu za kisiasa huku wananchi baadhi wakiishi kwa mlo mmoja, baadhi ya maeneo wanashindia maembe na mifugo ikifa kwa kukosa malisho kulikosababishwa na kukosekana kwa mvua za vuli katika maeneo mengi ya nchi, na wananchi Hawa kuwa wamejiandaa na akiba ya kutosha ya chakula.
Mchakato huo wa kumuunga mkono Lowassa utaruhusu watakaoguswa kutoa mchango wa chakula hususani nafaka zinazoweza kuhifadhika kwa muda, mafuta ya kupikia, fedha taslim n.k kwa utambulisho wa wazi au wa siri na baadae mamlaka za eneo husika zitashirikishwa kuhakikisha wenye uhitaji wanapata msaada mapema kabla hawajadhurika zaidi wakati Serikali ikisubiriwa kuendelea kujitafakari.
Kwa jinsi mtonyo unavyoeleza, zoezi litahusisha marafiki wote wa Lowassa na CHADEMA wa ndani na nje ya nchi!
Hofu yangu ni endapo Serikali itaridhia mpango huu mwema kufanikiwa kusaidia watanzania wenzetu au itaendelea na msimamo wa kukana kutokuwa na ukosefu wa chakula kwa baadhi ya wanajamii na mifugo kipindi hiki waumini wa dini mbalimbali wakiendelea kufanya maombi kuombea mvua inyeshe kunusuru hali.