Kamanda umeeleweka vizuri sana, ushauri wako utanyiwa kazi, sababu viongozi wetu ni wasikivu na waelewa, chini ya usimamizi wa kamanda Mbowe na Dr wa ukweli Slaa, ondoa shaka. Kamanda, kwa sasa jambo la msingi, tunapaswa kudai haki yetu ya kikatiba ya kupiga kura, kwa kuhakikisha daftari la kudumu la wapiga kura linaboreshwa, na tunapeana hamasa ya kwenda kujiandikisha, hili ni jambo linaloturudisha nyuma muda mrefu tangu ufanyike uchaguzi 2010, hata hivyo tunashukuru vingozi wetu, kwa kuwaelimisha wananchi, kwani hata haya mafanikio machache uyaonayo, tunapigiwa kura na wengi waliokuwa ccm au walioko ccm, hata tukikazana sana kutoa elimu vijijini, bila daftari hakuna kitu, tutazi kupeana lawama tu, vyote viende kwa pamoja, hapo tufanikiwa.