CHADEMA: Kuelekea Uchaguzi 2014 na 2015

CHADEMA: Kuelekea Uchaguzi 2014 na 2015

iringa

Member
Joined
Feb 5, 2012
Posts
66
Reaction score
33
Kumekuwepo na mijadala mingi kuhusiana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) juu ya mustakabali wake kisiasa hasa baada ya kuwavua uanachama wanachama wake waandamizi na matokeo ya uchaguzi wa madiwani uliofanyika hivi karibuni na CDM kuambulia kata 3 kati ya 27.


Mojawapo ya sababu kuu zilizotajwa na chama ni pamoja na kutoboreshwa kwa daftari la wapiga kura kwa mda mrefu sasa, hivyo kuwanyima vijana wengi nafasi ya kupiga kura hasa ikizingatiwa ndio wanao onekana kukikubali chama hiki kikuu cha upinzani kwenye medani za kisiasa nchini.

Pili ni uingiliaji wa dola kwenye shughuli nzima ya uchaguzi kwa kuwepo na matukio kadhaa wa kadha yanayousisha kukamatwa kwa viongozi wa CDM na mawakala wa chama sehemu mbalimbali ulikofanyika uchaguzi huo.

Sababu zinaweza zikawa ni nyingi sana zaidi ya hizo na zinazoitaji tathimini ya kisayansi kuelekea chaguzi zijazo za serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu mwakani ili kuleta matokeo chanya kwa upinzani Tanzania.

Jambo moja kubwa ni kuwa japo chama kimekuwa kikipata misukosuko mingi nyakati za uchaguzi lakini ukubalikaji wake maeneo ya mijini umekuwa mkubwa sana tofauti na maeneo ya vijijini hata kama hila na fitina kinzani zimekuwa zikifanyika kutoka chama tawala. Ndio maana haikushangaza kata ya Sombetini na Njombe mjini kunyakuliwa toka CCM.

Mijini kumekuwa na elimu kubwa ya uraia tofauti na vijijini kupitia vyanzo mbalimbali hasa pale ambapo kimekubalika, wapo waliomeza yamini kwa chama na ndio maana imekuwa rahisi kupata matokeo mijini japo vikwazo ni vingi. Vijijini ni tofauti kabisa na mijini, CHADEMA ni msingi inafanya kazi kusawazisha tofauti hii lakini yaitajika nguvu ya ziada kuwatengeneza wafia chama watakokuwa tayari kukipigania chama kama ilivyo mijini.

Nguvu ya CCM bado ni kubwa na inapungua kwa taratibu sana.

Kwa kuwatumia viongozi wa kanda na wenyeji wa maeneo husika pekee kuimaliza mizizi ya chama tawala huko itachukua mda mrefu na uwenda ikachelewesha ukombozi kwenye chaguzi zijazo.

Kuna haja sasa ya viongozi wenye sura ya kitaifa kuanza kufanya ziara ndani ya vijiji vilivyoko mabonde kuinama ambavyo havijawai kufikiwa na kiongozi yeyote yule mkubwa ndani ya chama. Hili litaleta hamasa ya hali ya juu kwa watanzania wenzetu hawa na kuifanya oparation M4C CHADEMA ni msingi kufanikiwa kwa kiwango kusudiwa.

Uwingi wa kazi, majukumu ya kiuongozi, ukubwa wa nchi na rasilimali fedha ni kikwazo juu ya utekelezaji wa rai hii, pamoja na hayo ni lazima chama kikubali kukabiliana na changamoto hizi, vinginevyo mwanya unaoipa CCM ushindi utaendelea kuwepo kwa kipindi cha miaka mingi ijayo na kuzuia jitihada za kuiletea nchi yetu maendeleo kupitia ushindani wa medani za kisiasa.
 
Kurekebisha daftari la wapiga kura ni jambo la muhimu. Lakini kubwa zaidi ni hili: Tume ya uchaguzi bado ni ya CCM! Bila kuwa na tume huru ya uchaguzi nchini, upinzani kushinda kwa kishindo ni ndoto!! CCM itaendelea kushinda kwa hila za tume katika kila uchaguzi.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Kamanda umeeleweka vizuri sana, ushauri wako utanyiwa kazi, sababu viongozi wetu ni wasikivu na waelewa, chini ya usimamizi wa kamanda Mbowe na Dr wa ukweli Slaa, ondoa shaka. Kamanda, kwa sasa jambo la msingi, tunapaswa kudai haki yetu ya kikatiba ya kupiga kura, kwa kuhakikisha daftari la kudumu la wapiga kura linaboreshwa, na tunapeana hamasa ya kwenda kujiandikisha, hili ni jambo linaloturudisha nyuma muda mrefu tangu ufanyike uchaguzi 2010, hata hivyo tunashukuru vingozi wetu, kwa kuwaelimisha wananchi, kwani hata haya mafanikio machache uyaonayo, tunapigiwa kura na wengi waliokuwa ccm au walioko ccm, hata tukikazana sana kutoa elimu vijijini, bila daftari hakuna kitu, tutazi kupeana lawama tu, vyote viende kwa pamoja, hapo tufanikiwa.
 
Du!, umeafanya research then ndo ukawasilisha!, safi sana and it is too logical,, hizi ndo mada nzur m2 kwanza unajichambua na kujipanga kupitia misin ya ukwel na uharal wa kile unachokuja kupresent!,,"no research no right 2 speak". ni kwel unakisema na kwa sasa inahitajika nguvu ya ziada xana kuelekeza vijjn ambapo wa2 bado wana upofu wa akili m2 anasema ccm ilinizaa na ndo inanilisha,,,so wa2 kama hawa bado kaz 2nayo ya kuelekea mageuz ya kimfumo wa utawala...pia daftar likishaboreshwa bac mambo yatakuwa mazur mno!
 
Back
Top Bottom