vitangaye
Member
- Jul 28, 2015
- 45
- 27
Historia ni mwalimu mzuri kweli. Kiongozi yoyote aliyesoma historia ni rahisi sana kuongoza.
CHADEMA ni chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania. Ndicho chama kinachofuatia kwa kuwa na wafuasi wengi na ushawishi baada ya Chama tawala (CCM). Watanzania wengi wameweka tumaini lao katika chama hiki. Pamoja na kuwa na wafuasi wengi na kifananisha chama hiki na UTOPIAN SOCIALISTS. Kwa waliosoma historia hasa Elimu ya juu si wageni katika msamiati huu.
Utopian socialist ni wakina nani ?
Mwishoni mwa karne ya 17 hadi 18 kulitokea mfumo tano wa maisha katika historia ya binadamu. Huu ni mfumo wa kijamaa usio kuwa wa kinyonyaji. Baada ya mfumo wa kibepari kukomaa, unyonyaji uliongezeka kwa kasi ya ajabu. Tabaka la chini (maskini au wafanyakazi ambao walikuwa hawana uwezo wa kumiliki ardhi, mtaji na njia nyingine za uzalishaji waliishi kwa shida na ku nyanyaswa sana )wanafanya sana kazi asubuhi mpaka jioni lakini ujiira ni kiduchu. Mabepari na serikari yao waliishi kwa raha sana, yaani kama malaika (according to Mkulu). Ndipo wakaibuka watetezi wa wanyonge hawa ambao ni Robert Owen,Henry De Saint -Simon, Charles Forier n. k. Hawa ndio waanzilishi wa Utopian socialism.
Kwa nini waliitwa Utopian socialist?
Waliitwa hivyo kwa sababu ya njia walizotumia kudai haki zao. Yaani wao waliamini kwamba ipo siku mabepari watasalimisha Mali zao kwa serikari na tabaka la chini. Wao waliishia kulalamika tu huku wakiisubiria kwa hamu siku mabepari na serikari yao watakaposalimisha mali hizo kwa tabaka la chini sio kwamba wao wapambane hadi wanchukue mali kwa mabepari kama Ardhi, viwanda ,mtaji n. K.
Mwishoni mwa karne ya 19 hadi 20 wakaibuka watetezi wengine wa maskini na wafanyakazi, hawa waliitwa Scientific Socialist. Hawa waliongozwa na Karl Marx, Fredrick Angels, Vladimir Lenin, Joseph Stalin n.k. Hawa walikuwa tofauti kidogo na utopian socialists. Wao waliamini kwamba class struggle and violence. Was the better means of achieving socialist goals. Hii ilipelekea October revolution 1917 na kisha kuasisiwa Kwa serikari ya kijamaa mara ya kwanza bara la Ulaya Nchini Urusi.
Kwa nini nasema CHADEMA ni Utopian socialist ?
Kwasababu mbinu wanazozitumia CHADEMA kudai haki hazitofautiani Sana na za kina Robert Owen, Henry De Saint -Simon n. k. Mfano mbinu wanayoitumia ya Kususa uchaguzi, Matamko yasiyotekelezeka,kila siku kutoa matamko kwenye vyombo vya habari. Kibaya zaidi wanaamini kwa kufanya hivyo wataigopesha serikali hii tukufu. Chadema wanaamini kwamba ipo siku Mtawala atakuwa mpinzani. Mathalani uchaguzi mkuu wa mwaka 2015,Chadema chini ya Lowasa walijinasibu kwamba wameshinda uchaguzi, wakaishia tu kulia kulia kwamba watangazwe kuwa wao ndio washindi bila mapambano yoyote yale.
Nawaambia Chadema na Wapinzani wengine, Hakuna mahali popote pale ambapo serikari kandamizi iliondoka voluntarily. It was through class struggle (between the oppressor $ oppressed) and violence. Wasitegemee kukamata dola kwa imani tu.
Chadema hawana nia thabiti ya kukamata dola zaidi ya usanii na kutanguliza maslahi binafsi.
Kidumu chama cha mapinduzi.
Mwanachama mtiifu wa
CCM tawi la mtandaoni.
Kwa sasa napatikana Zanzibar.