commonmwananchi
JF-Expert Member
- Mar 12, 2011
- 3,377
- 1,954
Wana bodi JF,
Kwa heshima kubwa nawasalimia,
Baada ya hapo twende kwenye Mada,
Edward Lowassa alikuwa mgombea wa urais JMT, kupitia UKAWA, na bila Shaka tuliaminishwa kila kona ya nchi yetu na wapiga debe wake na UKAWA kwa ujumla kwamba bwana huyu alikuwa ndio muarobaini wa matatizo ya nchi hii,
Bahati mbaya kwake na UKAWA kwa ujumla wananchi waliamua vinginevyo na kumuamini zaidi Bulldozer JPM, na akachaguliwa kuingia ikulu ya magogoni, mahali patakatifu alipo mpaka muda huu ninapoandika Mada hii.. Mengineyo ni yamebaki kuwa historia kwa sasa.
Huku UKAWA hususan chadema, kuna pengo la uongozi hususan kwenye nafasi ya katibu mkuu, nafasi iliyoachwa wazi na mpiganaji wa kweli Dk wilbroad slaa, baada ya kujiuzuru nafasi hiyo kwa kile alichokielezea kama kutoridhishwa na mchakato wa kumleta Lowassa ndani ya chadema kama mgombea Urais wa chadema na UKAWA kwa ujumla wao.
HOJA YANGU.
Nafasi ya katibu mkuu wa chama ni muhimu sana kwa uhai na maendeleo ya chama chochote kile cha siasa
Chama cha siasa kinaimarishwa na mikutano ya ndani, pamoja na mikutano ya uhamasishaji na ujenzi wa vyama kuanzia makao makuu hadi matawini na kwenye mashina.
Na yote hii bila Shaka ni moja ya majukumu nyeti ya kiutendaji ya katibu mkuu wa chama.Nafasi ya katibu mkuu ni ya kiutendaji ya kimajukumu ya kila siku.
Sasa baada ya Uchaguzi kuisha, chadema imewawia vigumu kumpata mrithi wa Dk slaa?
Je kama mliuaminisha umma kwamba Lowassa yuko fit na ni kiongozi muadilifu, muaminifu na mchapakazi hodari, na mkadiriki hata kumtosa Dk slaa, kwa nini hamtaki kumpa ukatibu mkuu?
Kama Mbowe ulituaminisha watanzania kwamba Lowassa anafaa kuwa Rais wa JMT, kwa nini hutaki kumpa ukatibu mkuu wa chadema?
Au Mbowe na ukoo kwa ujumla mnaogopa kupoteza udhibiti wa chama, kwa kuwa nguvu ya Lowassa ni kubwa pia kifedha?
Kama sivyo na Mbowe unakumbuka kauli yako nainukuu "ni mjinga pekee au mtu asiyejitambua atakayekataa kumpokea Lowassa na niwahakikishie wanachama wenzangu, kwa mtaji wa Lowassa ni kwamba tutaingia ikulu saa nne asubuhi" mwisho wa kunukuu. Ni kwa nini usichukuwe maamuzi magumu na kujiuzuru Ili vijana waendelee na pale ulipofikia wewe na ubaki kama mzee na mshauri muhimu wa chama pamoja na kuwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni?
Naomba kuwakilisha na tuchangie bila matusi tafadhali...