Chadema isitie aibu mrithi wa Regia!


wewe ni kimeo wa kufikiri
 
Mambo mengine ni ya kisheria ndo maana tunataka katiba mpya. Tume ya uchaguzi wana majina ambayo chama kilishayapeleka na inapotokea mtu anafariki anachukuliwa anayefuatia kwenye orodha. Tushiriki kuunda katiba mpya ili kuyaondoa haya. Hapa hata kama ni CCM ama cdm ni utaratibu huo kumbuka alivofariki Amina CHIFUPA CCM alipatiwa anayefuata japo vijana wengi walitaka angetafutwa wa kufanana naye.

 
Kumbukumbu ipi hv we unajua mizengwe ambayo hutumika na CCM kupata hawa wabunge wa viti maalumu? Chadma ni chama ambacho kwa hilo walijitahidi sema watu tumejaa hila kwani kama mtu ni ndugu na viongozi wa chadema hawaruhusiwi kuwa wabunge? mbona hauhoji mtu kama zainabu Kawawa ambaye najua yeye alifight hakubebwa, haya kina Ana Abdalah na wengine wengi tu. Chadema walitumia mtaalamu mshauri bwana Kitila Mkumbo na waliweka vigezo baadhi ya akina mama walidhani ukiwa kiongozi wa juumuiya basi inakuwa first priority ndo maana mkti wa wanawake chadema alihama kwa kuwa alikosa sifa hizo na akatoka na shutuma nzito.

CHADEMA walichofanya cha kwanza ni kuwa akina mama wote waliogombea ndo walipewa first priority kwa kwanza kuthubutu kuingia kwenye mapambano jukwaa na ndo kilichompatia pia na Marehemu Regia Ubunge. ni ile nguvu na uthubutu wake wa kujitokeza kugombea ndo maana wanawake nadhani wote waliogombea ubunge kwa chadema walipokosa wamepewa viti maalumu. Hata Mdee angekosa angepewa maana walishaonyesha ile sense ya leadership kumbuka Rose Kamili ambaye alihama CCM akiwa diwani na akagombea matokeo yalikuwa na utata nadhani Mh Nagu alitangazwa na tume. Hivyo tuache upashkuna na tena wewe thread nyingi ni za kimalaria sugu nashangaa unapojifanya unawahurumia chadema. Mimi si cdm lkn ni mfuatiliaji

 

Nahisi na kuamini hili jibu linamtosha tu.
 
CHADEMA ni chama makini chenye misingi imara. Itafuata katiba yake na mambo yatakuwa sawa.
 
Chadema haiko kama unavyofikiria.
Mawazo yako ni kama ya yule mother wa Bawacha alijengue-Mama Mosore.
CDM inawatu makini sana, kabla hujalisemea hapa washalijadili.
Mchakato uko wazi, wasi wasi wa nini?
Tulia subiri maamuzi ya fikra pevu
 
Tuantoa tahadhari kabla ya hatari ili kama kuna mchezo wahusika wanataka kuucheza wajue watu tuko macho,hiyo ya kututaka tusubiri mpaka maji yafike shingoni ndio tujue kumbe tunazama haisadii sana.

Tatizo lako hujui Kanuni na taratibu kuhusu Uteuzi wa wabunge wa viti maalumu especially pale mmoja anapoacha au kufariki Dunia, kwa msaada Rejea Uteuzi wa mama wakatare baada ya kifo cha amina chifupa.
 
Tayari anaemfuata Regia ni diwani wa Karatu kwa Mujibu wa Tume,hayo hayapo ndani ya Uwezo wa Chadema tena ni tume baada ya Chama kupeleka majina zamaani kwa Mpangilio

Na watu lazima wakumbuke kwamba sheria ni msumeno.Hakuna swala la upendeleo katika hatua hii maana mpangilio wa majina upo na ulishajulikana. Tusubiri kutangaziwa jina tu .Tuombe tu awe mpiganaji kama Marehemu REGIA(RIP)
 

Ndiyo tatizo la kushiriksha masaburi katika kutoa hoja. Bosi wako washamlambisha sumu huko Mwanza, sijui nani atakuwa anawapa posho za kuleta upupu hapa jamvini.
 

kwa maoni yangu, ningependa atakayeteuliwa atoke kule ambako cdm hawana nguvu za kutosha ili huyo mtu atumike kama njia ya kuwavua wanachama na wapenzi wa mageuzi huko pembezoni mwa nchi au hata katikati kama tabora au dodoma, tanga, lindi, pwani iringa nk
 
Bado tuko kwenye majonzi nadhani kwasasa hili halituhusu!

biashara ni asubuhi, mahesabu baadae. linatuhusu na tusipojenga msingi wa kukijenga chama, watatuharibia hawa viongozi. Human being are selfish in nature
 
Kwahiyo akiteuliwa mtoto wa mkulima ndio haki itakuwa imetendeka ila kinyume na hapo haki itakuwa haijatendeka....... Think loud !!. Naamini kuna vigezo therefore tubase kwenye hivyo vigezo bila kuangalia nani atakuwa ameteuliwa vinginevyo tunawashauri waongeze kipengele cha umasikini katika uteuzi....
 
Gud idea! But mi nadhani ktk kujaza nafas ya dada ye2 RIP mtema, ni vyema kusiwe na upendeleo wowote wa kimahusiano bali inabid achaguliwe m2 mpiganaji na makini lakin asiwe kigeugeu na m2 huyo hatakama atakuwa ni mtoto wa mbowe lakini kinachomata ni uwezo wa m2 ktk maswala ya siasa na si kingine. So hata kama ana undugu na zitto ts oryt.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…