Chadema inataka kuisafisha CCM dhidi ya tuhuma za ufisadi?

meningitis

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
8,394
4,748
Ukiongelea kelele nyingi za Ufisadi mkubwa na wenye madhara na ulioongelewa sana nchi hii ni ufisadi wa Richmond.

Hiki kilikuwa ni kilele cha ufisadi nchini na rekodi yake haijawahi kufikiwa.

Rekodi yake ni kubwa kwani kwa mara ya kwanza waziri mkuu aliangushwa au kujiangusha kutokana na tuhuma za ufisadi...ambazo kwa kiasi kikubwa zilipigiwa kelele na kusemwa sana na chadema.

Hakuna asiyekumbuka list of shame ikiyotajwa pale mwembe yanga na wanachama wa chadema.

Leo hii chadema inajaribu kutupa karata yake upya kwa kutaka kumsafisha mmoja wa mafisadi kinara watuhumiwa wakuu wa sakata hilo.

Kwangu mimi hili ni kosa la kiufundi linalorudiwa na Chadema ...yaani Chadema wanataka kumsafisha lowassa miaka michache baada ya kuukosa urais kwa tuhuma za ufisadi.

Wengi wa wananchi ambao tayari waliiamini chadema katika mapambano dhidi ya ufisadi walikataa kumchagua fisadi...how come chadema wafikirie kufanya jaribio lingine la kumsafisha fisadi??

Nilitegemea chadema wajiweke pembeni zaidi dhidi ya huyu fisadi na kurudi tena kwa wananchi kwa kuwaomba radhi kwa hadaa walizojaribu kuzufanya.

Somo na maoni yangu ni kwamba ili sisi wananchi tukubali kuwa jamaa sio fisadi basi itatubidi kuamini kuwa CCM sio chama cha mafisadi.

Kwa hisani ya Chadema Asilia.
 
ufisadi wa richmond ulisemwa sana sio kwa sababu ya ukubwa wake bali ni kutokana na ongezeko wa uelewa wa watu na ongezeko la wabunge wa upinzani bungeni,lakini sote ni mashahaidi kuna maafisadi makubwa yamefanywa nchi hii kabla ya richmond na yote yalifunikwa na Ma CCM
 
hivi mradi wa umeme wa pesa nyingi kiasi hicho-unataka kuniambia Mkataba wake hukupelekwa kwenye baraza la mawaziri,unataka kuniambia kikwete hakuupitisha? ni nani mwenye final say ndani ya serikali??
kwa nini umuhukumu Lowassa na kumuacha Kikwete??
 
kwa hiyo ongezeko la uelewa na idadi ya wabunge wa upinzani haikuona huo ufisadi meingine wenye ukubwa mithili ya ruchmond?
 
hivi mradi wa umeme wa pesa nyingi kiasi hicho-unataka kuniambia Mkataba wake hukupelekwa kwenye baraza la mawaziri,unataka kuniambia kikwete hakuupitisha? ni nani mwenye final say ndani ya serikali??
kwa nini umuhukumu Lowassa na kumuacha Kikwete??
Uwe umepelekwa au haukupelekwa

Iwe JK amehusika au hakuhusika...

Kitendo cha kuanza kubishia ripoti ya ufisadi huo ni kitendo cha kuhalalisha usafi wa ccm.
 
Back
Top Bottom