Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,188
- 7,490
Wakuu, hii ni kama kanuni, ikitokea kila mtu unayemuona au unayeishi naye au anayekuongoza unamuona mbaya, ujue watu hao si wabaya bali mbaya ni wewe.
Yaani unaanza kuishi na Juma siku mbili unalia umepigwa, anakuja John unakaa naye siku moja unalalamika anakula chakula chote anakunyima, anakuja Joseph usiku mmoja tu ukiamka unalia, ukiulizwa shida nini unasema usiku anakuvuta shuka. Anakuja Erik siku moja tu unalalamika anakusema vibaya: unapoona hivyo, ujue wenye matatizo si wale unaokaa nao bali ni wewe na tafuta njia ya kubadilika.
Alikuwepo spika Marehemu Sitta, Chadema walimchukia na kumlaumu sana, akawepo Makinda Chadema wakamzodoa sana, Mama tulia ndio hawaelewani kabisa na sasa Ndugai washakorofishana.
Chadema mna tatizo jichunguzeni mjirekebishe.hata Remmy alishaimba ukiwa mtenda mabaya kila siku utadhani unaonewa. Haiwezekani kila mtu mbaya kwenu. Kikwete alikuwa mbaya kwenu amekuja Magufuli naye mbaya vile vile, kwa hiyo ninyi ndio wazuri tu au?