Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,242
- 34,903
BARAZA la Vijana wa Chadema (BAVICHA) Wilaya ya Bahi, Dodoma wamemshauri Rais John Magufuli kufanya kazi kwa manufaa ya Watanzania wote.
Vijana hao wametoa kauli hiyo leo walipokuwa katika kongamano la vijana lililolenga kuwajengea uwezo ili kufanya siasa zenye mafanikio.
Malambaya Manyanya, Mwenyekiti wa BAVICHA Mkoa wa Dodoma amesema, ni wakati sasa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kung’olewa kutokana na kulewa madaraka pia kujaa kiburi.
Amewataka vijana wa Chadema na wale katika vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kuunganisha nguvu kwa lengo la kuiondoa CCM.
Mbali na hilo vijana hao wamesema, Serikali ya Awamu ya Tano ni kati ya serikali zenye utawala mbaya kuliko zilizopita kwa madai, inaendeshwa kwa kuvunja Katiba ya Nchi sambamba na kukiuka haki za binadamu.
Hata hivyo, vijana hao wamelani Serikali ya Rais Magufuli kuzuia vipindi vya Bunge kuoneshwa moja kwa moja.
Vijana hao kwa pamoja walisema kitendo cha serikali ya awamu ya tano ya kuzuia bunge lisioneshwe moja kwa moja ni kitendo cha kuvunja katiba ya nchi.
Katika hatua nyingine vijana hao wamedai kitendo cha Rais Magufuli kujidai anatumbua majipu ni usanii mtupu.