CHADEMA business as usual

CHADEMA business as usual

gstar

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2011
Posts
814
Reaction score
1,490
Sisi wana CHADEMA tulio kipigania chama kwa damu na kuwa tayari kutoa uhai wetu kwa ajili ya chama tunasikitika na mfumo wa chama kinavyo endeshwa hasa katika ugawaji wa nafasi za viti maalum.

Viti maalum vimegawanywa kwa upendeleo wa kindugu kikanda pia kibaguzi na kuacha watu walio kipigania chama patupu, pia kuna baadhi ya mikoa ambayo imekuwa mstari wa mbele kuleta mabadiliko imetupiliwa mbali katika viti maalum.. Shame.

Wamepata mahawara na ndugu zao pamoja na watoto wao na jamaa wa kabila zao. Makamanda wa kweli wameachwa!

Hivyo mimi binafsi nikiri wazi kuwa CHADEMA tuliokuwa tunaamini itatuletea mabadiliko sasa haina dhamira ya kweli ya kuleta mabadiliko.

Tumekuwa tukihamasishwa tuandamane sisi ilhali inajulikana maandamano yalizuiwa lengo lilikuwa vijana waumie kwa manufaa ya watu wachache.

Mimi nasema sasa itakuwa ni vigumu kuing'oa CCM madarakati hata baada ya miaka 100 ikiwa chama tulichokuwa tunakishabikia hakina dhamira ya kweli ya kutuletea mabadiliko tuliyo yaamini.

Pamoja na majonzi makubwa niliyokuwa nayo tangu kutangazwa kwa mheshimiwa Magufuli kuwa Raisi wa Tanzania lakini sasa nashawishika kusema HAPA KAZI TU.
 
So ulikuwa unapigania chama ili upate Ubunge kupitia viti maalum au una lingine?

Hamia kwenye Kazi TU kwa sababu mpaka sasa umechelewa mpaka viti maalum vimeshaisha
 
Karibuni sana! Tulijua kuwa njia ya walaghai ni FUPI.... CHADEMA waliwalaghai manyumbu wakaingia Mkenge.... hawa jamaa hawana mapenzi mema na Tanzania kumbuka jina la chama ni CHAgga DEvelopment MAnifestor.....what do you expect???
 
Wajanja walishtukia muda mrefu kuwa Chadema ni genge la wasaka-fursa. Hamia ACT Wazalendo au Jahazi Asilia
 
Hizi ni blabla hazina facts unasema mahawara wamepewa viti maalum ila husemi ni akina nani. Hebu eleza wewe ungevigawaje ili kila mtu aridhike.
 
gstar
CHADEMA ni taasisi na kila kukicha inazidi kukuwa wewe nenda tu huwezi kuongea pumba kama izo ulitaka uteuliwe wewe au
 
Last edited by a moderator:
ha ha ha bungeni kutamu bana .. hakuna mtu anayetafuta kazi ili afaidike zaidi jirani yake.... lazima ashibe yeye kwanza ndipo agawe kwa majirani.... japo wapo wachche wenye hekima anaweza gawana na jirani hata kama bado hajashiba.... weka akilini hilo
 
Usishange ya Masha na Mahanga!!! Sumayi, Kingunge, Lembeli na Msindai chali wanazisoma namba kwa kirumi!
 
Hizi ni blabla hazina facts unasema mahawara wamepewa viti maalum ila husemi ni akina nani. Hebu eleza wewe ungevigawaje ili kila mtu aridhike.

JOYCE MUKYA,ANATROPIA
CC
mbowe,john mrema
 
Sioni sababu kulalamika kuhusu viti mahalumu sijui mbowe kapendelea inaoteu ni kamati kuu ya Chadema ili 2020 nawo wagombea kama wabunge wengine
 
nyie ndio mliopokea kipondo heavy baada ya kuandamana ati mnapinga maamuzi ya kupejwa dr mla ...
 
Back
Top Bottom