umeeleza vizuri sana lakini kwa sisi wa mjini huwa junajibu hivi:-
- hakuna kitu kama hicho mambo ya ukoo wala nini tunadanganyana kinachtusumbua ni stress zilizoletwa na utawala huu kafanya kila jambo kuwa gumu.
- hayo unayotueleza is just imagination na upotoshaji ili watu waangaike makanisani na huenda umetumwa kwa kuwa sadaka zimepungua.[emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144]
yapo mengi lakini ukweli ndio huo na ukitaka kuona angalia kwa mambo manzuri mfano kijijini kunaweza kuwa na familia iliyoanzishwa na baba mwalimu na mama mwalimu kuna uwezekano mkubwa watu hawa kuwa waalimu au tuangalie hata kwa nafasi za juu karume baba yake rais na yeye akawa rais pia hata kwa kenyata pia.
hivyo yanapotokea lazima kurudi nyuma na kuangalia kuna nini na kwa nini hili limetokea maisha tuanyoishi leo tunayatengeneza kwanza kwa binadamu wa ndani na ndipo binadamu wa nje anafanya hivyo kama ndani hakuna utulivu na kunavurugu kunalia kisasi,laana maagano ya kafara zinazodaiwa na mizimu hakuwezi kuwapatikana utulivu.
changamoto tulionayo maisha yetu yamekuwa vugu vugu unaenda kanisani ukitoka unawahi kwa mganga kisha ndo unarudi nyumbani.
zipo changamoto za usiri hata kuzaliwa kwetu mfano kunauwezekano mama kakuzaaa lakini baba uliyenaye sio baba yako mzazi na wewe umefichwa baba yako kafichwa lakini mtu wa ndani unajua kila kitu kwakweli mtu wa namna hii kufanikiwa inaweza kuwa shida kwa kuwa wakati mwingine hana kibali kwa familia husika katika ulimwengu wa roho.
mwisho wa siku ni kukataliwa na kujikataa na matokeo inaweza kuwa kufanya umalaya uliopitiliza, au chochote kinachoweza kufikia hata kuwa kichaa au kujiua.