CCM Zanzibar yaipongeza ZEC kutangaza tarehe ya uchaguzi

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
1.jpg
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimeelezea kuridhishwa kwake na maamamuzi ya Tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC) kwa kutangaza siku ya kufanyika kwa uchaguzi wa marudio kwa nafasi ya Urais, Uwakilishi na Udiwani.

Kimesema maamuzi ya kufanyika uchaguzi huo Machi 20 mwaka huu, yanaenda sambamba na matakwa ya wananchi waliokuwa wengi katika kutekeleza haki yao ya kidemokrasia kwa mujibu wa miongozo ya katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar, Waride Bakar Jabu alisema kwamba CCM inaungana na vyama vingine vya kisiasa nchini vilivyobaini kasoro za uchaguzi mkuu uliopita kuwa na kasoro na kuunga mkono maamuzi ya ZEC kuwa ni sahihi kwani yamefuata hatua muhimu za Kikatiba.

Waride alisema msimamo wa CCM katika Mkwamo wa kisiasa uliopo Zanzibar ni kurudi katika uchaguzi wa marudio ili kila chama cha kisiasa kinachoshiriki katika uchaguzi uliopita kipate haki ya kungia madarakani kwa njia halali na zinazokubalika kisheria.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo Waride alieleza kwamba maamuzi hayo ndiyo kipimo sahihi cha kuweka uzani wa ukomavu wa kisiasa na demokrasia katika mfumo wa vyama vingi kwani lazima kila chama chenye haki ya kushiriki katika uchaguzi kiridhike na hatua zote zinazofanywa mpaka kupatikana kwa mshindi anayeongoza kwa wingi wa kura halali.

“ Tunachukua fursa hii kuwaomba wananchi wote wenye haki ya kupiga kura hasa wafuasi wa CCM pamoja na wananchi wote wajitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura Machi 20 mwaka huu.

"Tukumbuke kwamba maamuzi hayo yamefanywa na Chombo chenye Mamlaka ya kusimamia masuala yote ya Uchaguzi nchini baada ya kujiridhisha kuwa kuna kasoro zilizotokea katika uchaguzi uliofutwa na kuona kuna haja ya kila mwananchi kupata haki ya kuwachagua viongozi wanaowataka kwa njia huru, wazi na zinazokubalika kisheria”. Alifafanua Waride na kuongeza kuwa uchaguzi huo ndiyo njia mwafaka ya kumaliza mkwamo wa kisiasa Zanzibar.

Katibu huyo aliongeza kwamba pia wanaunga mkono msimamo wa vyama vya vyote vya kisiasa vilivyokubali kushiriki uchaguzi wa marudio pamoja ushauri wa Msajili wa Vyama vya Sisasa nchini, Francis Mtungi kwa kuvitaka vyama vyenye usajili kushiriki katika mchakato huo ili kudumisha Demokrasia na malengo na malengo ya vyama kutumia uchaguzi kushika Dola.

Akizungumzia suala la CUF kususia Uchaguzi wa marudio alisema kwamba walichofanya ni mwendelezo wa migomo na kususa kwa mipango ya maendeleo inayofanywa na mamlaka za serikali katika kufanya mipango mbali mbali ya maendeleo kwa maslahi ya wananchi, hivyo hakuna jipya wala athari inayoweza kuathi hali ya kisiasa Zanzibar.

Alisema kwamba upinzani wa aina hiyo hauna nia njema ya kujenga maendeleo ya nchi bali una nia malengo ya kukwamisha na kudumaza maendeleo ya nchi kwa maslahi binafsi ya baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaoweka mbele tamaa ya madaraka kuliko maisha ya wananchi.

“ Kila chama kina sera zake na misimamo yake sasa wao kama wameona kususia uchaguzi wa marudio ndiyo njia ya kumaliza mkwamo wa kisiasa Zanzibar hiyo ni juu yao, lakini sisi tutashiriki kikamilifu ili chama chetu kipate ridhaa ya wananchi kurudi madarakani ya kidemokrasia."

Aidha alisema chama hicho kinaamini kwamba Uchaguzi Mkuu uliofanyika Octoba 25 mwaka 2015 ulikuwa na kasoro nyingi zilizosababisha uchaguzi huo kukosa sifa ya kuwa uchaguzi huru na wa haki na hatimaye kufutwa.

Kupitia taarifa hiyo Waride wamewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi katika mkutano wa hadhara wa mikoa minne kichama ya Unguja katika uzinduzi wa miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM itakayofanyika katika Afisi kuu ya CCM Kisiwandui, January 31 mwaka huu.

Alisema Mgeni rasmi katika uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein.
 
Huyo mama kada wa CCM asiseme kuwa wanaipongeza ZEC kwa kutangaza tarehe ya marejeo, bali aseme wanampongeza mtu wao Jecha kwa kuamua kuibaka demokrasia, kwa kuwa maamuzi ya kuufuta uchaguzi ule yalikuwa yake binafsi ambapo hakuwahusisha makamishna wenzie wa ZEC baada ya 'kuanriwa' na chama chake kuufuta ule uchaguzi mkuu wa tarehe 25/10/2015 uliofanyika kwa uhuru na haki.

Lakini wahafidhina wa CCM wanapaswa kukumbuka kuwa makosa ya jinai huwa hayafutiki.

Mfano halisi ni huyu Gbagbo wa Ivory Coast ambaye mashitaka yake yameanza kusikilizwa huko The Hague Uholanzi wiki hii, ambapo huyo jamaa aliyekuwa Rais wa Ivory Coast 'aliyapindua' matokeo ya uchaguzi uliofanyika mwaka 2010 ambapo yeye alishindwa uchaguzi huo hadi kusababisha machafuko makubwa nchini yaliyogharimu maisha ya wananchi zaidi ya 3,000 wa nchi hiyo.

Ingawa akina Dr Shein na wenzake akina Balozi Sefu Iddi wanafurahia 'uharamia' wanaowafanyia wananchi wa Zanzibar, lakini watambue kuwa mkono wa sheria hautawaacha, hata kama itapita miaka 10!
 
HIVI kwanini wa zanzibar wanachelewesha hili
Mpaka Leo ma ccm yanacheza na akili za watu
CUF kinukisheni sababu mnayo
Nia mnayo
Nguvu mnayo
Mwishowe mtaonekana maboya
CCM wenyewe mnaleta uchochez watu wkiamua mtakoma
 
Huyo mama kada wa CCM asiseme kuwa wanaipongeza ZEC kwa kutangaza tarehe ya marejeo, bali aseme wanampongeza mtu wao Jecha kwa kuamua kuibaka demokrasia, kwa kuwa maamuzi ya kuufuta uchaguzi ule yalikuwa yake binafsi ambapo hakuwahusisha makamishna wenzie wa ZEC baada ya 'kuanriwa' na chama chake kuufuta ule uchaguzi mkuu wa tarehe 25/10/2015 uliofanyika kwa uhuru na haki.

Lakini wahafidhina wa CCM wanapaswa kukumbuka kuwa makosa ya jinai huwa hayafutiki.

Mfano halisi ni huyu Gbagbo wa Ivory Coast ambaye mashitaka yake yameanza kusikilizwa huko The Hague Uholanzi wiki hii, ambapo huyo jamaa aliyekuwa Rais wa Ivory Coast 'aliyapindua' matokeo ya uchaguzi uliofanyika mwaka 2010 ambapo yeye alishindwa uchaguzi huo hadi kusababisha machafuko makubwa nchini yaliyogharimu maisha ya wananchi zaidi ya 3,000 wa nchi hiyo.

Ingawa akina Dr Shein na wenzake akina Balozi Sefu Iddi wanafurahia 'uharamia' wanaowafanyia wananchi wa Zanzibar, lakini watambue kuwa mkono wa sheria hautawaacha, hata kama itapita miaka 10!
Um

Umesahau kitu kimoja, katika jicho la jumuiya za kimataifa Zanzibar siyo nchi..
 
I wish ningekuwa na mamlaka ya kiMungu kuna wanadamu ningekuwa nawapa adhabu za papo kwa papo especially wanasiasa wanao penda kuwaaminisha watu uwongo. Kweli Mungu si Athumani.
 
Hivi inawezekanaje huyo Jecha awe yeye ndiye mlalamikaji na wakati huo huo akajigeuza Polisi wa kuchunguza huo ukiukwaji wa 'kufikirika' wa uchaguzi na wakati huo huo akawa mwendesha mashitaka na hatimaye akawa Jaji wa 'kesi' hiyo na kuhukumu kuwa kutokana na kasoro nyingi za 'kufikirika' kwenye uchaguzi huo akaufuta uchaguzi huo!

Hakika siamini hiki kituko cha karne kilichofanywa na Jecha kinaweza kufanyika kwenye Taifa lingine lolote hapa duniani.

Ndoyo maana ulinzi anaopewa huyo Jecha huko mafichoni na vyombo vya usalama vya hapa nchini walikompeleka huko yanazidi ulinzi anaopewa Rais Obama wa Marekani!
 
Wanaingia gharama kutoa bilioni saba kurudia uchaguzi usio na haki,ni bora hizo bilioni saba wangewapa wananchi wa zanzibar wajiendeleze kiuchumi,alafu simple tu wangejitangaza washindi
 
Kwanini CUF wanaogopa kurudia kama walishinda kihalali
 
View attachment 320107 CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimeelezea kuridhishwa kwake na maamamuzi ya Tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC) kwa kutangaza siku ya kufanyika kwa uchaguzi wa marudio kwa nafasi ya Urais, Uwakilishi na Udiwani.

Kimesema maamuzi ya kufanyika uchaguzi huo Machi 20 mwaka huu, yanaenda sambamba na matakwa ya wananchi waliokuwa wengi katika kutekeleza haki yao ya kidemokrasia kwa mujibu wa miongozo ya katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar, Waride Bakar Jabu alisema kwamba CCM inaungana na vyama vingine vya kisiasa nchini vilivyobaini kasoro za uchaguzi mkuu uliopita kuwa na kasoro na kuunga mkono maamuzi ya ZEC kuwa ni sahihi kwani yamefuata hatua muhimu za Kikatiba.

Waride alisema msimamo wa CCM katika Mkwamo wa kisiasa uliopo Zanzibar ni kurudi katika uchaguzi wa marudio ili kila chama cha kisiasa kinachoshiriki katika uchaguzi uliopita kipate haki ya kungia madarakani kwa njia halali na zinazokubalika kisheria.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo Waride alieleza kwamba maamuzi hayo ndiyo kipimo sahihi cha kuweka uzani wa ukomavu wa kisiasa na demokrasia katika mfumo wa vyama vingi kwani lazima kila chama chenye haki ya kushiriki katika uchaguzi kiridhike na hatua zote zinazofanywa mpaka kupatikana kwa mshindi anayeongoza kwa wingi wa kura halali.

“ Tunachukua fursa hii kuwaomba wananchi wote wenye haki ya kupiga kura hasa wafuasi wa CCM pamoja na wananchi wote wajitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura Machi 20 mwaka huu.

"Tukumbuke kwamba maamuzi hayo yamefanywa na Chombo chenye Mamlaka ya kusimamia masuala yote ya Uchaguzi nchini baada ya kujiridhisha kuwa kuna kasoro zilizotokea katika uchaguzi uliofutwa na kuona kuna haja ya kila mwananchi kupata haki ya kuwachagua viongozi wanaowataka kwa njia huru, wazi na zinazokubalika kisheria”. Alifafanua Waride na kuongeza kuwa uchaguzi huo ndiyo njia mwafaka ya kumaliza mkwamo wa kisiasa Zanzibar.

Katibu huyo aliongeza kwamba pia wanaunga mkono msimamo wa vyama vya vyote vya kisiasa vilivyokubali kushiriki uchaguzi wa marudio pamoja ushauri wa Msajili wa Vyama vya Sisasa nchini, Francis Mtungi kwa kuvitaka vyama vyenye usajili kushiriki katika mchakato huo ili kudumisha Demokrasia na malengo na malengo ya vyama kutumia uchaguzi kushika Dola.

Akizungumzia suala la CUF kususia Uchaguzi wa marudio alisema kwamba walichofanya ni mwendelezo wa migomo na kususa kwa mipango ya maendeleo inayofanywa na mamlaka za serikali katika kufanya mipango mbali mbali ya maendeleo kwa maslahi ya wananchi, hivyo hakuna jipya wala athari inayoweza kuathi hali ya kisiasa Zanzibar.

Alisema kwamba upinzani wa aina hiyo hauna nia njema ya kujenga maendeleo ya nchi bali una nia malengo ya kukwamisha na kudumaza maendeleo ya nchi kwa maslahi binafsi ya baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaoweka mbele tamaa ya madaraka kuliko maisha ya wananchi.

“ Kila chama kina sera zake na misimamo yake sasa wao kama wameona kususia uchaguzi wa marudio ndiyo njia ya kumaliza mkwamo wa kisiasa Zanzibar hiyo ni juu yao, lakini sisi tutashiriki kikamilifu ili chama chetu kipate ridhaa ya wananchi kurudi madarakani ya kidemokrasia."

Aidha alisema chama hicho kinaamini kwamba Uchaguzi Mkuu uliofanyika Octoba 25 mwaka 2015 ulikuwa na kasoro nyingi zilizosababisha uchaguzi huo kukosa sifa ya kuwa uchaguzi huru na wa haki na hatimaye kufutwa.

Kupitia taarifa hiyo Waride wamewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi katika mkutano wa hadhara wa mikoa minne kichama ya Unguja katika uzinduzi wa miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM itakayofanyika katika Afisi kuu ya CCM Kisiwandui, January 31 mwaka huu.

Alisema Mgeni rasmi katika uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein.
kwani ccm wao wanaruhusiwa kufanya mikutano?
 
Kwanini CUF wanaogopa kurudia kama walishinda kihalali

Wewe Mchovu nitakusaidia hapo! Kwenye elimu ya juu kuna kanuni ya kurudia mitihani (supplementary examination) kama umeshindwa kupata alama za kutosheleza kufaulu mtihani. Mazingira ya uchaguzi wa Zanzibar wa tarehe 25, oktoba, 2015 yanaonesha ya kwamba CUF ilishinda matokeo ya uchaguzi kwa hio haihitaji kurejea uchaguzi. Ila CCM wao walishindwa uchaguzi ndio maana wanaiomba tume ya uchafuzi iwapangie uchaguzi wa supplementary. Kwa ufupi ni kwamba kama umeshinda uchaguzi huna haki ya kufanya supplementary election lakini kama umeshindwa uchaguzi basi ni lazima ufanye supp yake! Nadhani utakuwa umeelewa mantiki yote ya uchaguzi wa marejeo hapo .
 
kwanini hawa watu wanapenda kungangania madaraka kinguvu???????
mana zanzibar live wanaforce.,.
huku bara waliiba live na full evidence za upinzani waliongoza,..
Hivi hii nchii haya mambo yataendelea hadi lini??????
na watu tunaona2 watu wanaongoza kwa wizi
 
Back
Top Bottom