CCM 'yapoteza' viti 2,600 Serikali za Mitaa

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
Na Habel Chidawali na Rachel Chibwete, Mwananchi

Posted Alhamisi,Decemba18 2014 saa 9:53 AM

KWA UFUPI
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Tamisemi), Khalist Luanda alisema jana kwamba wakati CCM ikifanikiwa kupata ushindi wa jumla mitaa na vijiji 9,406, kwa pamoja vyama vingine vya upinzani, vimegawana nafasi 3,211.

Dodoma. Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) imetangaza matokeo ya awali ya uchaguzi wa Serikali za mitaa nchi nzima yanayoonyesha kuimarika kwa upinzani.

Kwa ushindi huo upinzani umeongeza viti 1,981 ikilinganishwa na uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliopita mwaka 2009 ambao kwa ujumla, ulipata nafasi 1,230 za wenyeviti wa mitaa na vijiji.

Kwa upande wake, CCM imepoteza nafasi 2,636 za uenyekiti wa vijiji na mitaa ikilinganishwa na uchaguzi wa mwaka 2009 ilipopata jumla ya viti 12,042.

Hata hivyo, uchaguzi mwa mwaka huu, umefanyika huku kukiwa na nyongeza ya mikoa, wilaya, mitaa na vijiji katika baadhi ya maeneo nchini.

Luanda alisema CCM kimepata vijiji 7,290 kikifuatiwa na Chadema yenye vijiji 1,248. CUF imeshika nafasi ya tatu kwa kuwa na vijiji 946, ikifuatiwa na UDP yenye vinne na TLP na NLD vyenye viwili kila kimoja.

Katika nafasi za wenyeviti wa mtaa, CCM kimechukua jumla ya mitaa 2,116. Vyama vingine na nafasi zao kwenye mabano ni Chadema (753), CUF (235), ACT (9), NCCR - Mageuzi (8) wakati vyama vya TLP, UMD, UDP na NRA vimepata mtaa mmoja kila kimoja.

Matokeo hayo yamejumuisha maeneo mengi ambayo CCM ilipita bila ya kupingwa.

Katika matokeo hayo, CCM imeendelea kufanya vizuri katika mikoa ambayo imekuwa ikitajwa kuwa ni ngome yake lakini kuna maeneo ambayo yalionekana kuyumba kwa kuzolewa na upinzani.

Mfano wa ngome ambazo CCM kimetikiswa zaidi ni Mkoa wa Dodoma katika wilaya za Kondoa na Chemba ambako vyama vya CUF na Chadema vimefanya vizuri tofauti na uchaguzi uliopita.

Kuhusu nafasi ya mwenyekiti ambaye alisimikwa na wananchi kibabe katika Mkoa wa Arusha, Luanda alisema Tamisemi haitamtambua, bali atakuwa ni mwenyekiti wa kimila tu.
 
UKAWA tujikikite vijijini zaidi,kina mama tujitahidi kundi la kina mama na vijana liwe lote la ukawa.Daftari la wapiga kura liboreshwe tuzisimamie kura zetu haya majizi yasiibe ccm inaondoka
 
Pongezi nyingi sana kwa upinzani hasa CDM Ila bado,huu ushindi uwe chachu ya kurudi vijijini kuwaambia wananchi asanteni kwa kutuamini na kutuelewa lkn Bado tunawahitaji zaidi katika uchaguzi Mkuu hapo 2015 tuwatoe Hawa majambazi madarakani.......CHAGUA UKAWA ILI TUKOMESHE WIZI NA KULIPELEKA TAIFA MBELE.
 
Kwa data hizo ni kwamba maccm yana 74% na sio 85% ya MwanaDiwan
 
ni kama ccm imepata 74.55% ikiwa imeporomoka kwa 18.15% na upinzani ukipaa kwa kupata 25.45% hii ni pamoja na mapingamizi ya ccm, sasa ukitoa mapingamizi ndiyo ccm inapitwa kabisa, huyu mwanadiwani ni vuvuzela huwa hajui kitu ni kushabikia ccm bila kutafakari,ccm mmeporomoka hautaki wewe mbishi.
 
Kwa data hizo ni kwamba maccm yana 74% na sio 85% ya MwanaDiwan
Hiyo 74 ya maescrow ukitoa waliyopita kwa mapingamizi yao , unapata km 34% tu.
Na hiyo 34% ni kwa kutumia dola, polisi, vitisho, rushwa , wizi n.k.
 
baada ya uchaguzi nimekuja kijijini nimeshangaa sana kukuta ccm imegalagazwa nikiuliza kulikoni wanasema wamechoka na ccm wanataka mabadiliko nikawauliza mnadhani ni chama gani kitawakomboa wanasema cdm kidogo huku hawajaijua UKAWA ombi viongozi wa cdm wafike vijijin wananchi wanashauku ya kuwafahamu makanda wao niko katika jimbo la mwibara kwa kangi lugola tena wengine wameenda mbali nakusema wanaimani nae ila akiendelea kubaki ccm hana chake tena kwa ujumla wanasema hawana imani tena na ccm
 
Hizi ni habari njema kwa upinzani kushangilia anguko la ccm.
 
Na Habel Chidawali na Rachel Chibwete, Mwananchi

Posted Alhamisi,Decemba18 2014 saa 9:53 AM

KWA UFUPI
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Tamisemi), Khalist Luanda alisema jana kwamba wakati CCM ikifanikiwa kupata ushindi wa jumla mitaa na vijiji 9,406, kwa pamoja vyama vingine vya upinzani, vimegawana nafasi 3,211.

Dodoma. Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) imetangaza matokeo ya awali ya uchaguzi wa Serikali za mitaa nchi nzima yanayoonyesha kuimarika kwa upinzani.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Tamisemi), Khalist Luanda alisema jana kwamba wakati CCM ikifanikiwa kupata ushindi wa jumla mitaa na vijiji 9,406, kwa pamoja vyama vingine vya upinzani, vimegawana nafasi 3,211.

Kwa ushindi huo upinzani umeongeza viti 1,981 ikilinganishwa na uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliopita mwaka 2009 ambao kwa ujumla, ulipata nafasi 1,230 za wenyeviti wa mitaa na vijiji.

Kwa upande wake, CCM imepoteza nafasi 2,636 za uenyekiti wa vijiji na mitaa ikilinganishwa na uchaguzi wa mwaka 2009 ilipopata jumla ya viti 12,042.

Hata hivyo, uchaguzi mwa mwaka huu, umefanyika huku kukiwa na nyongeza ya mikoa, wilaya, mitaa na vijiji katika baadhi ya maeneo nchini.

Luanda alisema CCM kimepata vijiji 7,290 kikifuatiwa na Chadema yenye vijiji 1,248. CUF imeshika nafasi ya tatu kwa kuwa na vijiji 946, ikifuatiwa na UDP yenye vinne na TLP na NLD vyenye viwili kila kimoja.

Katika nafasi za wenyeviti wa mtaa, CCM kimechukua jumla ya mitaa 2,116. Vyama vingine na nafasi zao kwenye mabano ni Chadema (753), CUF (235), ACT (9), NCCR - Mageuzi (8) wakati vyama vya TLP, UMD, UDP na NRA vimepata mtaa mmoja kila kimoja.

Matokeo hayo yamejumuisha maeneo mengi ambayo CCM ilipita bila ya kupingwa.

Katika matokeo hayo, CCM imeendelea kufanya vizuri katika mikoa ambayo imekuwa ikitajwa kuwa ni ngome yake lakini kuna maeneo ambayo yalionekana kuyumba kwa kuzolewa na upinzani.

Mfano wa ngome ambazo CCM kimetikiswa zaidi ni Mkoa wa Dodoma katika wilaya za Kondoa na Chemba ambako vyama vya CUF na Chadema vimefanya vizuri tofauti na uchaguzi uliopita.

Kuhusu nafasi ya mwenyekiti ambaye alisimikwa na wananchi kibabe katika Mkoa wa Arusha, Luanda alisema Tamisemi haitamtambua, bali atakuwa ni mwenyekiti wa kimila tu.

Samahanini sana wana jf msinicheke. Naomba kama **** mtu anaweza kunipa brief za matokeo s/mtaa zanzibar
 
Haa haa ccm inaondoka kama mzaha vile. Jamani kwa mwenye matokeo ya moshi manispaa tunaomba atuwekee hapa!
 
toa kabisa mkuu maeneo ambayo ccm waliweka mapingamizi
 
Amani kwetu sote,hivi ccm kupoteza viti vingi kwenye uchaguzi wa s/mtaa,vijiji na vitongoji ninini sababu iliyopeleka hali kuwa hivyo?naomba tuchambue sababu kwa umakini ukiona huna chakuchangia bora upite tu.nawasilisha.
 
Tatizo hawa jamaa wamefikia hatua wanajiamini saana na kufikiria kuwa Watanzsnia wa leo ni wale wale wa1980s ambao hawajuwi kusoma wala kuandika kwa sababu hiyo ndiyo capital yao hao watu,lakini wajue kuwa wananchi wamechoka saaana juu ya udhalimu wa hawa jamaa,tuache ushabiki lakini hawa jamaa ni hatari sana
 
Back
Top Bottom