CCM yakiri kubebwa na Dk MWAKYEMBE

CCM yakiri kubebwa na Dk MWAKYEMBE

SIMON CONDRAD

Member
Joined
Oct 16, 2012
Posts
9
Reaction score
10
KATIBU Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, amekiri kuwa Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, amekipa chama chake mradi wa kifisadi wa mamilioni ya shilingi wa upanuzi wa eneo la bandari jijini Dar es Salaam, kinyume cha taratibu.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana jijini Dar es Salaam, Nape alisema ni kweli kuwa kampuni ya Jitegemee ni mali ya chama chake, na kwamba iko mbioni kuingia ubia na mamlaka ya bandari nchini (TPA) kwa ajili ya mradi wa maegesho; mradi ambao utatekelezwa katika eneo la Mto Msimbazi, Tabata, jijini Dar es Salaam.

Kauli ya Nape imekuja siku moja baada ya Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA), Benson Kigaila, kuanika kile kinachoitwa “Ufisadi wa Dk. Mwakyembe”.

Kigaila alidai kuwa CHADEMA imepata nyaraka kadhaa zinazoonyesha Mwakyembe akishinikiza bodi ya TPA kujifunga katika mkataba wa kinyonyaji wa mamilioni ya shilingi na kampuni ya CCM ya Jitegemee Trading Company Limited ambayo ni mali ya CCM.

Nyaraka zinaonyesha katika mwaka huu wa fedha 2013/2014, serikali kupitia TPA imetenga kuilipa Jitegemee kiasi cha sh bilioni 10 kama malipo ya awali ya ujenzi wa eneo la mradi.

Aidha mamilioni hayo ya shilingi yanalipwa bila kutangazwa zabuni, kufanyika upembuzi yakinifu na bila kuwapo uchambuzi wa mradi iwapo kama utaingiza faida, jambo ambalo ni kinyume cha sheria za nchi.

Wakati CHADEMA wakisisitiza kuwa mradi huo haukufuata taratibu, Nape alisema, “Wanachokiita wenzetu wa CHADEMA kuwa ati ni zabuni iliyotolewa kwa kampuni ya Jitegemee na Mamlaka ya Bandari ni barua ya TPA kwenda Jitegemee wakiomba ridhaa ya kushirikiana kuliendeleza eneo la kampuni hiyo ya Jitegemee lenye ukubwa wa zaidi ya ekta 100, katika mfumo wa ushirikiano yaani ‘Joint Venture’ kupitia utaratibu wa PPP (Public, Private Partnership) jambo ambalo ni la kawaida sana kwani linafuata utaratibu na sheria zote husika.”

Hata hivyo, hii ni kawaida ya CCM kukana mikataba inayofungwa yenye harufu ya ufisadi. Mwaka 2008, aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, alikana kuingia mkataba wa aina hii katika jengo la Umoja wa Vijana wa CCM (UV-CCM), lililoko Lumumba, Dar es Salaam.

Uchunguzi unaonyesha kuwa tayari mradi huo umepitishwa na bodi ya bandari na kuingizwa katika bajeti kuu ya serikali ya mwaka 2013/ 2014, jambo ambalo linathibitisha kuwapo kwa mkataba.

Mradi wa Mwakyembe unafanyika kuikabidhi kazi ya maegesho kampuni ya CCM ambao unakwenda kinyume cha kusudio la mradi huo la kuondoa msongamano wa magari yanayosubiri kuingia bandarini katika Barabara ya Kurasini.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya TPA, mradi uliohamishiwa Mto Msimbazi ulipangwa kufanyika katika eneo la Kurasini, na kwamba wadau wakuu wa usafirishaji waliupitia mradi huo katika bajeti ya mwaka 2010/2011.

CHADEMA inapinga mradi huo kwa kuwa umefanywa kinyume cha sheria na kwamba eneo lililotengwa halifai kwa matumizi hayo. Inasema eneo hilo liliwahi kufugwa nguruwe, lakini waliishia kusombwa na mafuriko.
Source Tanzania daima ya tarehe 5/4/2013 Nawasilisha
 
Nape a.k.a Alsahaf anafahamika , kama anadai Mchakato huo ni halali , yale Mapovu aliyokuwa anamtolea Lowasa kwenye lile jengo la Uvccm lenye Mkataba wa Miaka 99 yalikuwa ya nini ?
 
Nape hajitambui naona wanajaribu kukusanya hela kwa ajili ya kuprint tshirts na kofia za kutosha lakini mwaka 2015 hela zenu tutakula na kura hampati,mwaka 2010 mlitumia kilimo kwanza mkaiba kule hela za kampeni awamu hii tunakwenda kwa lula kabisa na ninyi hamdokoi hata shiringi!!!!!
 
duh kumbe ndio maana alimuhujumu Mkurugenzi Mkuu wa BANDARI (TPA) Bw. Mgawe ili afanye ufisadi vizuri...kweli huyu ni fisadi papa naye anajiita kamanda wa ufisadi.....NAPITA
 
duh kumbe ndio maana Huyu Mwakyembe alimuhujumu Mkurugenzi Mkuu wa BANDARI (TPA) Bw. Mgawe ili afanye ufisadi vizuri...kweli huyu ni fisadi papa naye anajiita kamanda wa ufisadi.....NAPITA
 
Mwakyembe akishinikiza bodi ya TPA kujifunga katika mkataba wa kinyonyaji wa mamilioni ya shilingi na kampuni ya CCM ya Jitegemee Trading Company Limited ambayo ni mali ya CCM.
alaa kumbe CCM ina makampuni ya kibiashara eee, chama cha siasa kinaruhusiwa kinamiliki makampuni, je sheria za manunuzi ya umma PPRA zinasemaje hasa kwenye suala la conflict of interest? Maana mzee mzima mwakyembe amenasa kwenye hii sheria.

Mwageni hapa bid analysis tuone vigezo gani vimetumika kumpatia hii tender huyu Jitegemee?
 
KATIBU Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, amekiri kuwa Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, amekipa chama chake mradi wa kifisadi wa mamilioni ya shilingi wa upanuzi wa eneo la bandari jijini Dar es Salaam, kinyume cha taratibu.

.
Source Tanzania daima ya tarehe 5/4/2013 Nawasilisha

...kweli Tanzania Daima nalo limeingia kwenye list ya magazeti ya udaku, taarifa hii na ile ya Nape ni kama usiku na mchana...
 
Mwakyembe jitu ambalo lilipewa sumu na wakataka kuliua na bado linang'ang'ania ccm mi sina imani nalo tena.msomi wa ajabu sana huyu
 
Back
Top Bottom