CCM yaihenyesha CHADEMA Mitaani

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
40,613
Reaction score
26,253
Ndugu zangu watanzania,

Utendaji kazi uliotukuka wa serikali ya CCM chini ya uongozi shupavu na madhubuti wa Rais Samia Ambaye ndiye kiongozi mwenye ushawishi zaidi Barani Afrika kwa Sasa na ambaye anachukuliwa Kama mtetezi na sauti ya Afrika umeiipoteza na kuihenyesha chadema Mitaani.

Kwa Sasa Chadema haina ushawishi Wala kupata watu wa kuwasikiliza,kwa Sasa Chadema imebaki inatumia kiasi kikubwa Sana Cha pesa kuwalipa boda boda na waendesha bajaji ili waongoze misafara anapopita Mbowe na kupiga picha ili ionekane chama kipo mitaani ,maana wanajuwa hakuna wakufanya kazi hiyo kwa hiyari au kwa kujitolea Kama ambavyo vijana kwa wingi wao hujitolea kwa bashasha na furaha kuwalaki na kuwapokea viongozi wa CCm wafanyapo ziara katika maeneo yao kwa kutambua kuwa hao ndio watetezi wao na wenye majibu ya kero zao.

Sasa Chadema wamegeuka na kuwa matapeli kwa kuwadanganya vijana wanaojitafutia Riziki mitaani kwa kuendesha bajaji na bodaboda kwa kuwapa mabendera Yao kwa ahadi kuwa watalipwa malipo baada ya ziara za viongozi wao waliojikatia Tamaa na kupoteza matumaini kupita, chadema hawana huruma Wala aibu kuwatapeli vijana na kuwapotezea muda wao, Sasa Chadema wanatumia ulaghai kwa vijana waliojiajiri kubeba abiria mitaani.

Hii yote inatokana na CHADEMA kukosa Sera na ajenda zinazogusa maisha ya watanzania,hii yoye ni kutokana na kukosa dira na kupoteza muelekeo,Hii yote ni kutokana na kuwa na safu ya uongozi isiyoaminika kwa watanzania ndio sababu ya kupuuzwa na kuishia kukodi waendesha bajaji na bodaboda ili wawe mbele kuonyesha wanakubalika,Hii yote Ni kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na serikali ya CCM katika kuwatumikia watanzania ,kugusa maisha Yao na kujibu kero zao.

Hii yote ni kutokana na serikali ya CCM kuwa katika mioyo ya watanzania Baada ya utendaji kazi wake kuwaridhisha watanzania na kuwapa matumaini,Sasa Chadema inahenyeka na kuhangaika mitaani,Sasa Chadema inakodi na kusombelea watu utafikiri waenda minadani, Sasa Chadema inafanya matangazo kila eneo utafikiri matangazo ya mlipuko wa ugonjwa wa kipindu pindu mitaani lakini mwisho inakosa watu na kuishia kukodi waendesha bajaji na bodaboda, Sasa Chadema imekata pumzi na ndio maana Lisu aliamua kukimbia nchi kukwepa aibu hii inayoikumba chadema kwa Sasa. Maana alishaona upepo wa kisiasa umebadilika na watanzania wameipuuza chadema na kuikumbatia CCM katika mioyo Yao.

Huo Ni mwanzo tu maana muda siyo mrefu viongozi wa chadema wataanza kurushiwa mawe na makopo machafu kwa kuwapotezea muda wao, wataanza kuzomewa mitaani Kama ambavyo tumeona wakipingwa na watanzania wanapoisema vibaya serikali yao watanzania, Muda siyo mrefu chadema inakwenda kujifungia kabatini.

Mama yupo kazini na anafanya mambo kisayansi zaidi ndio maana Taifa linaendelea kuwa lenye utulivu na Amani huku kazi zikiendelea na kusonga mbele kwa Kasi ya upepo,Ni miradi kila eneo, Ni mafanikio kwa kila kitu, Ni matumaini kwa kila Jambo. Ni kazi kila sehemu zinaendelea kutekelezwa na serikali ya CCM.

Kazi Iendeleee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627
 
Maandishi mengi YOTE takataka kabisa
Wewe malafyale najuwa huwezi kuelewa kitu maana mmepaniki na kupoteza muelekeo baada ya kukataliwa na watanzania mijini na vijijini, mmebaki mnakodi watu tu kwa malipo,muende mkawalipe waendesha bajaji like sumbawanga mliko watapeli,so umewasikia nankuwaona walivyo andamana?
 
Wewe kilaza ndiyo maana huteuliwi,huna akili,unatumia muda wote kuishambulia Chadema,siasa hizo zilishapitwa na wakati ,na zina mrengo wa Sukuma Gang kundi ambalo linampiga vita Rais Samia sasa hapo utapataje uteuzi? Umepoteza mwelekeo.
πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜† Sasa mbona unatukana, Au hasira za kuona mnapuuzwa na watanzania Ndio unazileta kwangu, Kwani Mimi ndio niliwakodi waendesha bajaji na bodaboda ambao mmekuwa mnawazulumu kila mnapopita?

Mtawazulumu Hadi lini? Je hamtarudi Tena kwao? Au ndio mnakwenda kujifungia jumla kabatini pale ufipa kilinge cha kutafunia Ruzuku?
 

Hata uandike nn teuzi hupati
Wewe sio miongoni mwao
 
CCM yajenga nchi....
CCM ndio chama kilichobeba matumaini ya watanzania,Ndio chama Bora Barani Afrika na mfano wa kuigwa,Ndio chama kilicho na mfumo imara na madhubuti usiotegemea mtu binafsi

Ndio chama chenye Sera na ajenda zinazogusa maisha ya watanzania wa makundi yote,ndio chama chenye uchungu na maisha ya watanzania,

Ndio chama kilicho dhamiria kuipaisha nchi yetu kimaendeleo,ndio chama kinachohakikisha keki ya Taifa inatua katika mlango wa kila mtanzania,Ndio chama kinachomsaidia kila mtanzania kutimiza na kufikia ndoto zake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…