TandaleOne
JF-Expert Member
- Sep 4, 2010
- 1,644
- 709
- Thread starter
-
- #21
Huwa mara nyingi ninapokuwa ninapost kitu (kiwe cha aina yeyote) kihusu siasa ya ndani ya CCM ama nje.,kiwe kinahusu upinzani ama siasa za Dunia kwa Ujumla wake, huwa natarajia kuwa ujumbe unaokuwemo ndani ya post hiyo unawafikia walio wengi, naamini wengi wanajifunza na kujihabarisha mengi, lakini kingine ambacho huwa sikuwa nakitegemea na ambacho kimekuwa kikijitokeza kila mara ninapopost kitu kiasi sasa kufanya nione ni miongoni mwa mambo ambayo natakiwa kuyategemea pindi nikipost kitu hapa JF ni mfululizo wa comment zenye matusi ya kila aina, juu yangu, chama changu na wakati mwingine hata wazazi wangu.
Nikiwa kama binadamu wengine ambao wanafikra na hisia.,wanaumizwa na kujihisi vibaya nami naumia na kupata hisia mbaya na wakati mwingine ghazabu hunipanda. Lakini najiuliza ni kwanini vijana wanakuwa na aina hii ya ufikiri, ni nani anawafunza haya na kwanini wayapokee mafunzo hayo.? Nasema ni vijana kwani ni imani yangu kuwa watumiaji wa mitandao hii ya kijamii wengi wao ni vijana.,lakini simaanishi ni vijana wote watumia social media ni watu wa matusi bali wapo vijana hasa vijana wa upinzani hususani vijana wa Chadema ambao kwao matusi ndio lugha ya hoja.
Ni katika kuendelea fikra butu, ni katika mlolongo wa kufuata fikra za uongozi wa ki-imla ambao chadema wanao ni katika ufuasi wa kinguruwe ambao vijana hawa wanafanya haya. Mimi nasema neno moja kwao kuwa jamii hii haiwezi kupata nafuu ya maisha ikiwa katika sehemu yake wapo vijana (ambao ndio nguvu kazi na tegemezi la taifa) ambao hawajifikiri wala hawajilazimishi kufikiri nje ya umbile wanaloliona mbele yao.,vijana ambao wamekubali upotevu na kuukana uongofu. Vijana ambao hawajui kujisimamia na hawawezi kuijiongoza.,wanafanya lolote kwa yeyote kwa kuwa tu wameagizwa kufanya hayo.
Ni hatari kwa jamii lakini hatari zaidi kwa muendelezo wa siasa za chuki na uchonganishi.,ni hatari sana...!