VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,007
Gazeti lenyewe mwanahalisi ambalo ni uchochezi na uzushi.Waraka wa Pongezi toka kwa Kamati Kuu ya CCM kuelekezwa kwa Watendaji wa chama hicho umenaswa. Waraka huo unapongeza kufikiwa malengo ya kumiliki Mabaraza ya Katiba ya Wilaya.
Katika Mabaraza hayo Tanzania nzima CCM ina wajumbe asilimia 90. Waraka husika una jedwali linaloonesha mikoa,idadi ya wajumbe wa CCM,vyama vya upinzani na wale wasio na vyama. Alipoulizwa Mwigulu juu ya waraka huo,aliruka bila kutoa hoja ya msingi.
Waraka huu unathibitisha tuhuma zilizotolewa na CHADEMA kupitia Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria,Tundu A. Lissu(Mb) pamoja na Jukwaa la Katiba linaloongozwa na Bwana Deus Kibamba kwamba CCM imeuingilia na kuuharibu mchakato mzima wa uundwaji wa Katiba mpya hasa katika uchaguzi wa Wajumbe waMabaraza ya Katiba.
Chanzo: Gazeti la Mawio la Alhamisi tarehe 30/5/2013;Toleo Nambari 0045
Mimi: Waungwana wa Tanzania, hapa patapatikana Katiba ya nchi au ya chama tawala?
Cc Mwigulu Nchemba Nape Nnauye Ritz Sumu MwanaDiwani et al
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Mkuu mbona unaongea ubwabwa mkuu hayo unayosema unauhakika nayo.Hivi hao CCM tu ndiyo Wataipigia kura ya NDIYO au HAPANA hiyo katiba mpya, mbona wanajidanganya!
Au matumanini yao yapo kwenye NEC kwamba itachakachua KURA YA MAONI.
Kama rasmu ya katiba mpya haitakidhi maoni ya WATANZANIA tutapiga kura ya HAPANA. CCM msijidanganye, hurumieni kodi zetu mnazotumia sasa kutengeneza hiyo katiba ya ki-CCM, CCM
hoja za upinzani nyingi huwa zinafanyiwa utafiti wa kina kabla hazijaletwa hadharani,hili swali limeanza kupigiwa kelele mda sana,na hata cuf nao wamelisemea sana,lakini warioba kaziba pamba masikioni,ubinafsi na wa viongozi wetu hasa wa chama tawala ndiyo umetufikisha hapa tulipo,kwa kuamini wao wako perfect kwa kila kitu,kuna watu wanaweka utaifa mbele kimuonekano ila kimatendo ni tofauti kabisa.
katiba hii haikutakiwa kuingiliwa na chama chochote cha siasa,na wajumbe wa tume hii pia walitakiwa wawe huru na wengi watoka kwenye taasisi kama jukwaa la katiba,ama asasi za kiraia na sio vyama vya siasa,vyama vingetoa wawakilishi tu,lkn leo kumejaa waasisi wa Tanu na badae ccm unadhani tutakuw na katiba nzuri plus tume huru ya uchaguzi?<tutaitamani katiba ya kenya mpk kufa kwetu ila daima hatutafikia ubora wake labda kizazi cha watoto wetu not us>
Mwigulu,asha rose migiro,nape,kinana,mnakoipeleka nchi hii siko mnakodhani nyie,kizazi chenu kitawalaani sana kwani mawazo yenu hayawezi kuiwakilisha Tanziania nzima na wala hayataendana na kasi ya ukuwaji wa ubongo wa kazazi kijacho
Waraka wa Pongezi toka kwa Kamati Kuu ya CCM kuelekezwa kwa Watendaji wa chama hicho umenaswa. Waraka huo unapongeza kufikiwa malengo ya kumiliki Mabaraza ya Katiba ya Wilaya.
Katika Mabaraza hayo Tanzania nzima CCM ina wajumbe asilimia 90. Waraka husika una jedwali linaloonesha mikoa,idadi ya wajumbe wa CCM,vyama vya upinzani na wale wasio na vyama. Alipoulizwa Mwigulu juu ya waraka huo,aliruka bila kutoa hoja ya msingi.
Waraka huu unathibitisha tuhuma zilizotolewa na CHADEMA kupitia Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria,Tundu A. Lissu(Mb) pamoja na Jukwaa la Katiba linaloongozwa na Bwana Deus Kibamba kwamba CCM imeuingilia na kuuharibu mchakato mzima wa uundwaji wa Katiba mpya hasa katika uchaguzi wa Wajumbe waMabaraza ya Katiba.
Chanzo: Gazeti la Mawio la Alhamisi tarehe 30/5/2013;Toleo Nambari 0045
Mimi: Waungwana wa Tanzania, hapa patapatikana Katiba ya nchi au ya chama tawala?
Cc Mwigulu Nchemba Nape Nnauye Ritz Sumu MwanaDiwani et al
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Kama wameweza kuchakachua mchakato wa katiba hadi hapa tulipofikia na wananchi tumetulia, usitegemee huko mbele ndo watashindwa kuchakachua. Lets see ila CCM watatuletea kizaazaa hapa Tanzania kwa uchu wao wa Madaraka.Hivi hao CCM tu ndiyo Wataipigia kura ya NDIYO au HAPANA hiyo katiba mpya, mbona wanajidanganya!
Au matumanini yao yapo kwenye NEC kwamba itachakachua KURA YA MAONI.
Kama rasmu ya katiba mpya haitakidhi maoni ya WATANZANIA tutapiga kura ya HAPANA. CCM msijidanganye, hurumieni kodi zetu mnazotumia sasa kutengeneza hiyo katiba ya ki-CCM, CCM
Wkati watu wako busy na mchakato wa katiba, CHADEMA ilkuwa busy na maandamano! Mnategemea nini?
Well, katiba haizungumzii CCM bali mustakbali wa wananchi wote na sio kwamba wakishaamua hao wajumbe wa mabaraza ya katiba basi katiba inapitishwa kuwa sheria.
Katiba ni mchakato na mwisho wa siku itakuja tena kwetu kwa ajili ya kuipigia kura. Ni mapema mno kukata tamaa kwamba tuliyoyataka hayatakuwemo.
Hao wajumbe wa CCM walichofanikiwa kupata ni ajira ya muda tu si vinginevyo.
Nyumba huwa ni Msingi.Msingi ndio unaodefine nyumba.au mwenzetu kwenu mnaanza kujenga juu halafu ndio unamalizia msingi?
"Nyota njema huonekana asubuhi"