CCM yaachwa solemba

tunajua chadema wanataka serikali tatu ili moja iwe inatumikia wachaga tu hii nyingine ndiyo iwe ya wote hiki ni chama cha ajabu kabisa.

JF ni taasisi inayoheshimiwa sana lkn tukiacha maandiko kama haya yatawale humu wote tutaonekana mahayawani!

Hata uhuru wa kuongea una mipaka yake
 
Ni wajibu wako kutoa maoni yako ya serikali tatu hata tano ukitaka, naheshimu sana mawazo yako. mimi maoni yangu ni serikali mbili tu, hakuna sababu ya kuwa na miserikali miiingi, huo ni uroho wa madaraka na ni mzigo kwa walipa kodi

kwa sasa tuna makamu wa rais 1bara 2 zanzibar hio wewe huoni na gharama kwa mlipa kodi?
mie hata sioni waziri mkuu na makamu wa rais kazi yao nini...tatizo likitokea mpaka wamsubiri jk refer jairo issue
 
Para-kagamba na wajumbe wote wa tume wanapaswa kuelimisha wajumbe wa mabaraza kwa mtindo huohuo
 
ufipa fc, kinondoni makao makuu
 
vuta nikuvute, nenda ukale au kama umefunga nenda msikitini, hii kazi uliyotumwa kutumika humu imekushinda, huna hoja zaidi ya vioja
 
kwa sasa tuna makamu wa rais 1bara 2 zanzibar hio wewe huoni na gharama kwa mlipa kodi?
mie hata sioni waziri mkuu na makamu wa rais kazi yao nini...tatizo likitokea mpaka wamsubiri jk refer jairo issue

hivyo ni vyeo na pengine unachanganywa na majina tu, sio serikali wala sio nchi vile. dogo uko wapi??
 
Uwezo wako katika kuelewa na kujadi hoja ni mdogo sana. Hakuna sababu ya kusema tujadi hoja then wewe tena unaanza kuleta maneno ya kwenye kanga. Nilitegemea wewe ungejenga hoja zako based kwenye ukweli kwamba chama chako kinasimamia serikali mbili ili hata sisi tusio na vyama tuchuje mbivu na mbichi za serikali mbili. Vivyo hivyo kwa wale wanaotaka serikali tatu.
Sasa wewe posts zoote ni kejeli tuu.
Hazitasaidia chama chako.
Kumbuka watanzania waleo utawa-win kwa hoja tuu sio matusi wala kejeli. Hizo zilishapitwa na wakati.
Amini usiamini waweza kuwa mmoja wa wanaosambaratisha chama kwa haya unayo andika. Refer Nchemba, hoja zake alizokua anazitoa wakati wa kuwanadi wagombea kwenye chaguzi za marudio,
Watu walikataa natusi na kejeli wakachagua hoja na ukweli. Badilika kijana.
 
Nadhani kuna mpango wa kuleta upinzani mkubwa kwenye mchakato ili ifike 2015 bila kuwa na katiba mpya. Kabudi and others are simply playing their part.
 
Swala la serikali 3 HALIKWEPEKI.

( 1)Zanzibar walishajitenga kwa kujitangazia mipaka yake na muundo wa serikali ya Pamoja kwenye katiba yao mpya.
( 2) TANZANIA ni muungano wa TANGANYIKA na ZANZIBAR ili muungano uwepo ni lazima Tanganyika ife na ZANZIBAR ife ibaki TANZANIA.Hamna mahala popote pale DUNIANI ambapo kuna muungano halafu kuna nchi imesalia nje ya ule muungano mfano: Marekani,EU nk. huwezi kusema muungano wa EU na uingereza ama ujerumani muungano wao unabaki 1 bila nchi pembeni.
( 3) Ili MUUNGANO UDUMU ni lazima Tanganyika iwepo. ( G55 ) waliliona wakabezwa sasa limerudi waziwazi.
( 4 )Muungano hauwezi kuwa na DOLA 2. shirikisho ndio unaweza kuwa nao.

sababu zipo nyingi sana ambazo zinaufanya huu tunaoita muungano sio muungano.
 
Tuambie ni uongo gani VUTA-NKUVUTE kasema kwani si kweli Prof.Kabudi kasema hivyo? serikali tatu hazikwepeki.

CCM msitake kuwalisha watu maneno ya kusema waacheni wananchi waamue hatma ya katiba yao hii si katiba ya CCM.
 
Kwanini walaumu kwa k7ulishwa kasa tu? wangelishwa na Tango pori kabisaaaaaaa, CCM bhana ammbo yakiwaendea vibaya wanatafuta pa kutokea
 


Passport zetu za Tanzania.....Taifa la kusadikika tutazifanya nini?
 

how much do you get paid per day per this vapour
 
Hata hvo wanaotaka serikali ya serkal 2 bdo hawana uelewa wa kutosha coz ht huo muungano wanaokazania bdo ni batili xana kwa mujibu wa aticle of agreement ya muungano iliyoxainiwa na waacc wetu tar 22 mwak 1964 inaonesha ni muungano wa jamhuri ya watu wa zanzibr na jamhur ya wa2 wa tanganyika. Je hilo jina la tanzania limetoka wapi' ikiwa hata baadh ya vifungu vya muungano kwny katib vinaeleza hvy ht muungano wa sasa ni ubatili mtupu
 
utakoma na ujinga wako. msimamo wenu ni serikali nyingi, sisi tunasiamamia kwenye serikali mbili. twendeni kwenye hoja.

...ukisikia kufilisika kisiasa ndo huku,warioba kajaribu kuwapa picha halisi ya utafiti wake kwamba sera ya ccm ya serikali tatu haikubaliki kwa wananchi, bado wanakomaa tu. kwa maneno rahisi warioba anasema majority ya watanzania hawataki mnachotaka ccm na ndo itakavyo kuwa 2015...
 
Anaeogopa Serikali Tatu anakusudia kuichakachua Rasimu ya Sasa ya Katiba, na hana lengo zuri na Taifa hili la Tanganyika ambalo kimsigi liko hewani hlina Rais, Halina Serikali, Halina Jeshi wala vyombo vya Dola kama sehemu mojawapo ya muungano, aana muungano lazima uwe wa serikali au mataifa mawili! maana vyote tulivyonavyo ni vya muungano, na ni Muungano wa Zanzibar ambayo ina serikali na misingi migni tu ya Dola ikiwemo bendera, rais, bunge n.k. ila upande mwingine?

Tusidanganyane, tuache ushabiki hebu tufikiri kidogo zaidi ya ushabiki. Maana haijalishi nani anaunga mkono hoja gani swala la katiba si la CCM wala CHADEMA wala CUF wala chama chochote ni swala la Kitaifa.

Hebu tizama, CCM Kamati Kuu ilikaa wakajadili hawakufikia muafaka, na mara nyingi huwa muafaka haufikiwi kwakuwa Mwenyekiti na wajumbe wanashindwa kukubaliana msimamo. Cha ajabu walikubaliana wapeleke Rasimu kwa wanachama, sasa sijui kikao gani hivho kilichokaa kikanyumbulisha maoni ya Wanachama na kuaj na msimamo huo unaoropokwa na baadhi ya viongozi wa CCM bila aibu kwa kutumia hisia zao na kulazimisha uwe msimamo wa chama??? Tena kwa Kiburi kuna walioandaa Waraka na kuusambaza kwa wananchi, Waraka huo haujakanwa na hatuna uhakika umeandaliwa na kubarikiwa na nani maana bado viongozi wanahaha na kujichanganya.

Cha msingi hapa bwana waliopo madarakani wanaogopa Mzimu wao na Kivuli chao kinavyowafuata hata chenyewe hawakiamini. Raimu ya Katiba kama ilivyo inatoa mwanga mpya wa matumaini na Uwajibikaji kwa Wananchi kwa wale wanaotaka kuchukua madaraka. Wengi wa hawa walioko madarakani sasa hawafurahishwi na jambo hilo na wangependa kutu-manipulate na kutuhadaa kwa hoja zao ambazo nyingi kwa sasa zina shida sana, hazina maslahi ya watu bali ya kwao binafsi. Viongozi Hawa hasa baadhi ya wale wa CCM wa ngazi ya juu wanaogopa kupteza madaraka mengi waliyojilimbikizia. Mfano wabunge wenye vyeo lukuki na mishahara na marupurupu kupitiliza ambayo hayalingani na uwajibikaji wao. Wewe ni Mbunge, wewe nni Waziri, wewe ni Mmiliki wa Kampuni fulani ya Biashara, wewe unahisa kwenye Kampuni ya Mwekezaji ambaye Mradi wake uko chini ya Wizara yako, achilia mbali kamati na tume, sielewi na haiingii akilini.

Ili kufanikisha hilo la kulinda maslahi yao, wanaficha hoja yao ndani ya Serikali Tatu! ili Rasimu isipite, isipopita watatumia kila hila kushinikiza matakwa yao.

Kwani mara ngapi tumewasikia baadhi yao wakiropoka kuhusu viti vyao walivyonavyo sasa ambavyo ni wazi Rasimu inavipiga chini? Wanahaha hawaoni mwanga mbele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…