Mwanza ni sehemu sensitive sana kisiasa. Polisi fanyeni kazi yenu watu wa Kanda ya Ziwa huwa hawapigwi. Wanapigana.
Msiwaache wakapigana.
Ni vizuri na wagombea wote wakemee jambo hili kwa haraka sana. Na pale Mh. Highnes Kiwia anapo pata taarifa kuwa wanachadema wanapigwa basi awe mwepesi kushughulikia swala hili kwa kuwapigia polisi na kuna wakati vijana wa ccm wanawapiga vijana wa chadema na kuwakamata na kuwafunga kamba na kuwaingiza kwenye buti ya gari kwa kisingizio cha kuzomewa bila hata kuwapeleka Polisi.
Sasa hivi kumezuka mtindo mbaya sana, Chadema wakifanya mkutano maeneo ya mjini, Ccm hawaruhusu kupita barabara ya Nyerere road kwa kisngizio kuwa kuna Jengo lao maeneo ya Natta na hata wakati mwingine wana wapiga wale wote wanaopita na Bendera au kofia.
Leo muda wa saa moja jioni maeneo ya Nyakato sokoni Ilemela Mwanza. Wana CCM wakiwa wanatoka kwenye kampeni, waliamua kupiga kila waliye kutana naye njiani akiwa na Bendera ya UKAWA na hata kupiga magari na baadhi ya magari kuharibiwa na kusababisha vurugu/foreni kubwa eneo hilo bila hata kuzuiwa na Jeshi la polisi ambalo lilionekana eneo hilo.
Kitendo hiki kisipo kemewa kwa nguvu zote kitatuharibia Amani yetu tulio nayo. Na kwa sasa umezuka mtindo wa wanaccm kupiga watu hasa katika Wilaya ya Ilemela pale wanpo kuwa wanatoka katika kampeni bila sababu yoyote pale wanapokuona una kitu chochote kilicho na Maandishi ya vyama vingine (ukawa).
Tafadhali sana tunaomba Jeshi letu tukufu la Polisi lidhibiti hali hii kabla ya uchaguzi kufanyika.

haa haa ina maana wanachadema hawawezi kujitetea mpaka waite polis haa haa...